Kwa muda mfupi sana kiongozi wa Tanzania alipata maadui wengi sana

Kwa muda mfupi sana kiongozi wa Tanzania alipata maadui wengi sana

China na Tanzania kisera ni ardhi na mbingu usifananishe china na vitu vya kijinga kabisa mkuu
Wachina baada ya kuona population yao inavoongezeka kwa kasi, wakaja na sera ya kuzaa mtoto mmoja kwa kila wanandoa, lakini wakwetu sisi karuhusu wananchi wazaliane kwa kufyatua watoto kama matofali
 
Adakadabra nyingi tu ,tusiwe biased, tusiongee positive tuu as if hakuna negatives, huo ubadhirifu aliobaini CAG unatoka wapi kama wahusika wote wapo magerezani?
Yaani watakatifu ndio wamegeuka kuwa wabadhirifu?
Tuongee kwa kiasi wandugu.
 
Hata yeye hakutaka umpende...
Tuliomwelewa tulimpenda....

RIP mwamba
Motion ya huyo hayati wenu haikua na uelekeo wa kutupeleka uchina,ngoma ilikuwa inaelekea ZIMBABWE acheni kufananisha uharo na futari.
NIPO WAZI KABISA SIKUMPENDA JAMAA YENU HAKUWA KIONGOZI RAFIKI WA WATANZANIA.
 
Kwanza kabisa ni wanachama wenzake ambao walishazoea kupiga madili makubwa. Hawa walishazoea kukwapua mabil ya shilingi na wao huona kama wamekwapua shilingi elfu moja. Hawa walishamchukia sana kwa kuziba mianya yaou ya upigaji.

Pili ni wanasiasa wa upinzani ambao baada ya kusambaratisha vyama vyao nao wakawa hoi kisiasa. Na vyama vyao vikwa vimeyumba kisiasa na kiuchumi.

Tatu ni wananchi ambao wengi walimuona kama kiongozi ambae ni dikteta hawa wengi walidai kupoteza jamaa zao au ndugu zao kwa kile kilichodaiwa ni watu wasiojulikana.

Nne ni wafanyabiashara ambao walizoea kuhujumu uchumi kwa kutengeneza bidhaa bandia, kukwepa kodi, wengi walikamatwa na kukwepa kodi na walikuwa magerezani kwa kuhujumu uchumi

Tano ni matapeli na wapigaji hawa walishazoea kulipwa mabilioni ya senti kwa kuwa na kampuni za mfukoni na walikuwa wakilipwa hata kama hwajafanya kazi.

Kwa ujumla kiongozi alikuwa na maadui wengii sana kwa muda mfupi.

Hivi ndivyo Africa ilivyo.
Kabla huyu mwamba wenu hajaingia madarakani nilikuwa nikienda kumsalimia bibi kule nyanungu kwa kupita mbugani basi ilikuwa nalipa 30000 mpaka Tarime.
Alipoingia tu mwamba garama ikapanda ikafika 50000 eti wanaopita huko wote walipishwe kama watalii Wa ndani.
,utadhani anawakatia majani hao wanyama.kwa hili Mimi nkageuka kuwa adui wake.
 
JPM was kind of a leader.. Alikosea na Kuharibu reputation yake..
..Alipoendekeza ukabila.
..kuminya demokrasia
..kutotaka kosolewa
. ..Kuwachukia makabila ya kaskazini.
. ...Kukusanya kodi haramu kaskazini nakupeleka maendeleo chato wakati hakuna kodi inayokusanywa huko.
. ...Kuamuru critics wauawe.
. ....Kuwachukia wenye pesa hata Kama wamepata kihalali.
. ...Kuamini kwamba ninadamu wote wanatakiwa kuwa sawa kiuchumi wakati wamumbwa kwa uwezo tofauti wa kufikiri, bidii ya kazi, vipaumbele katika matumizi ya pesa wanazopata wakati wapo wanaospend vipato vyao na wengine wana invest nakuweka akiba ya baadaye.
. ...Kutokuwaamini watumishi wote wa serikali kwa Ku weka TISS kila sehemu ya kazi hata kama hawana uelewa wa kazi zinazofanyika sehemu husika.
. ...Kuvunja kifungu cha katiba kinachompa kila RAIA uhuru wa kwenda kokote anakotaka lli mradi havunji sheria. Hakuna kusafiri nje ya nchi bila kibali chake.
. ....Na mengine meeengi orodha ni ndefu.
 
Kabla huyu mwamba wenu hajaingia madarakani nilikuwa nikienda kumsalimia bibi kule nyanungu kwa kupita mbugani basi ilikuwa nalipa 30000 mpaka Tarime.
Alipoingia tu mwamba garama ikapanda ikafika 50000 eti wanaopita huko wote walipishwe kama watalii Wa ndani.
,utadhani anawakatia majani hao wanyama.kwa hili Mimi nkageuka kuwa adui wake.
Kila kitu tu kilipanda bei sio ilo tu wakati huo akuna ongezeko la mishahara, makampuni yanapunguza wafanyakazi, serikali Ajira hakuna.....uku serikali ikitangaza viwanda kuongezeka sjui maelfu mangapi nchini ndani ya miaka 5 😂😂😂😂
 

Pitia hizo nakala utaelewa kwanini binadam apendi mabadaliko na ndio maana kwenye course za management/uongozi module ya ‘change management’ inafundishwa jinsi ya kupambana na resistance na namna sahihi ya kuleta mabadaliko.

Watanzania wamezoea kuongezewa mishahara mara kwa mara hata kama nchi aina uwezo.

Wahitimu vyuoni wamezoea kupata ajira serikalini

Kuna watu wamezoea kufanya biashara na serikali tu

Wafanyabiashara awajazoea kufuata accounting procedures kwa mujibu wa sheria na wala awajui legal implication zake za kutofanya ivyo

Kuna watu wamezoea udokozi serikalini wa mali za umma, kutofuata government policies kwenye utendaji wa kila siku, uzembe makazini, viongozi wasiopewa targets; etc.

Kuna raia wa kawaida walishazoea kutapeli wenzao kirahisi bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria au kufanya biashara za magendo with ease.

Kuna vyama vya siasa ambavyo wanadhani mikutano ya hadhara ni haki yao hata baada ya uchaguzi.

Kuna vyombo vya habari vilizoea kuandika bias reports zenye kuutungia uongo upande fulani au kumchafua mtu au kutunga story tu ambayo aina ukweli wowote.

Mambo yote hayo hapo juu hayakubaliki hata nchi zilizoendelea sisi kwetu ni norm. Magufuli alianza kubadili hayo now change is not easy kama hizo nakala zinavyoelezea it takes time people to accept the new norm na watu walishaanza kukubali taratibu, mother naona kama vile anataka kurudi nyuma.

View attachment 1766941
Kwa maelezo ya kipuuzi uliyotoa siwezi kusoma upuuzi.
 
Back
Top Bottom