Kwa muda mrefu sasa Naota sana kurudishwa kurudi shule, kama leo nimeota nachapwa parade

😅🤣😂 Mkuu unaonekana una experience sana na hawa watu kwa hiyo wanachoka sana kwa maana akitoka kumroga juma akaenda kwa shabani na rashidi anakuta juma amesha pata matibabu inabidi aanze upya kumroga juma.kazi inakuwa nyingne tena😅
 
Pia ndoto za shule humaanisha kuna jambo umekosea mahali,kuna mtu umemfanyia baya ,umezini, umedanganya , hivyo unakumbushwa kutubu na kuacha jambo lolote ovu maana ndo chanzo cha anguko lako,Hata hayo manung'uniko ni dhambi badilika na fuatilia wapi ulipokosea kila jambo litarudi sawa
 
Ndoto za kuota hupo shuleni ni mbaya sana inawezekana unaota upo form 4 au darasa la Saba upo na wenzio inawezekana unaota unafanya mtihani si ndio? Ndoto hii inazuia maarifa yako ili usifanikiwe
Basi ndoto hii inamaana kwamba Kuna maagano babu zako waliweka maagano na mizimu au baba yako alikuwa anapenda kwenda kwa waganga kupata msaada majini huwa yanataka kuendelea kupewa sadaka na kizazi chenu
 
Sasa nifanyeje mkuu wangu kwa ushauri wako?
 
Katika ulimwengu wa kiroho bado haujamaliza kusoma still upo shule ndo maana issue za maendeleo hazisogei
 
Wa-Tanzania mna fikra za ajabu Kinoma!
 
Usiamini sana katika hayo mambo ya ndoto Mkuu, utapoteza robo tatu ya maisha yako ukifuatilia. Tia Bidii, Fanya kazi. Utasogea Mbele tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…