Kwa muda mrefu sasa Naota sana kurudishwa kurudi shule, kama leo nimeota nachapwa parade

Kwa muda mrefu sasa Naota sana kurudishwa kurudi shule, kama leo nimeota nachapwa parade

Kuhusu waganga mimi ni muoga sana. Kuhusu maombi, mimi sio mtu wa kusali nilishaacha nilipogundua wachungaji wananeemeka kupitia sisi. Sadaka huwa natoa kwa kuwasaidia wale watoto wa familia zisizojiweza
Sawa mkuu
 
Hizo ndoto ni ishara kuna mipango yako umeipanga vibaya...tena ni mipango ya msingi....mm zilinisumbua sana ila nilivyojua siri hiyo nikawa najua jinsi ya kukabiliana nazo....yan nikipanga mambo yangu alafu nikianza kuota hizo ndoto nabadilisha mpango bhas nazenyewe zinakata....
 
Hii maana yake Kuna jambo kubwa na gumu lipo mbele yako......na bahati nzuri umeshafanya Kila kituo kulitatua au kuksbiliana nalo(umeshamaliza shule) kwa hiyo usiogope kula maisha...mambo yamesja jisort
 
Daaah means huwa tunafungwa na kurudishwa nyuma, shuleni hatukumaliza japo tulipenda kusoma, na tuliomaliza kazi hakuna..

dawa ni kusali sana au kufanya mengine ya kimaendeleo tofauti na shule ila wasijue watu hayo mengine ufanyayo maana adui yako kakublock kwenye shule yaani hataki umalize shule, hataki upate kazi kwa kisomo chako, wanajua kwamba wewe ni kichwa na wanajua uwezo wako ni mkubwa kama ulivosema wewe ni mbunifu (siku zote wachawi wanapenda kuangusha mtu chuma yaani kucheza na mwenye nyota nzuri).

Wewe fanya reverse yaani fanya mengine kama biashara na lazima utafanikiwa japo iwe siri, usikae karibu na wanao kujua, mara nyingi huu mtego ni mtu wa karibu kakufanyia yaani ndugu, waambie bado maisha yako ni taabani, ili wafikiri wamekuweza kumbe ushawasoma.

Siku zote mchawi ukimwona kakuzidi mwache kaa kimya maana wanafikaaga mahali wanachoka, wanazeeka na wanakufa, huwezi logwa milele.

Mimi haya yako yamenitokea nimeota nasoma msingi, sekondari mpaka chuo kikukuu, that means kuna tego wamelicheza......wengine wanakufukuza kwenu kwa kutegewa uchawi wa kiatu, kwamba ukienda Dar, ardhi ya kwenu hutokaa urudi tena wala kufikiri kuiwaza kuirejea.....
Duh ndugu ni hatari sana na haya yapo sana kwenye koo zetu
 
Ndoto ni matokeo ya ubongo kuchakata taarifa na kumbukumbu zilizopo akilini wakati upo usingizi. Ndoto hazina tafsiri yoyote kama inavyosemekana na wengi
S kweli kuna. Siku unaweza muota ambaye hamjaonana siku nyingi mara paap asubuhi huyo ndo anakuwa wa kwanza kuonana nae
 
Inategemea kama Unaota unachapwa fimbo za makalio! 🤔(chunga sana yas yako)

Kama ni fimbo za mikono, maana ake uongeze bidii sana kwenye njia za ufanyaji kazi, aidha unalega lega au ubadilishe mapema baadae usije Pata mkwamo

Mwsho, kama ni fimbo za miguu, angalia watu unaoambatana, je ni watu sahihi, mahali unapopendelea kwenda🙏
 
Inbox umeweka kufuli nimeshindwa reply ngoja nikupe time table kila siku saa 4 kuna maombi mtu mmoja utapata muongozo mzuri njoo hapa lutheran church kkkt kimara korogwe jumamosi kuna maombi ya pamoja saa 5 asubuhi mpk saa 8 na kila siku jioni saa 12 na nusu mpka saa 2 usiku njoo usiteseke hiyo misingi na huyo anaekutest ashindwe
Mbona halipo dada
 
Uongo mtupu.
Sio uongo,Bora huyu kaweka wazi Mimi nimewahi kuwa naota hivyo hivyo mara kadhaa Niko Chuo nafanya mtihani wa SoMo ambalo sikuwa nlimudu vizuri na kiasi nahofia sitopata cheti ,severa times lakini Cha kushangaza huko nilishavuka na cheti ninachi ila Sasa Huwa zinanitesa sana na sielewi manake ni nini but wengi niliojaribu kuwashilikisha Huwa wanasema Kuna kauzibe umewekewa na nani hapo ndio mtihani kujua.
 
Kuhusu waganga mimi ni muoga sana. Kuhusu maombi, mimi sio mtu wa kusali nilishaacha nilipogundua wachungaji wananeemeka kupitia sisi. Sadaka huwa natoa kwa kuwasaidia wale watoto wa familia zisizojiweza
Ukiniuliza Mimi siwezi kushauri.kwenda Kwa waganga au sijui wachungaji Kwa sababu wengi wao wamekuwa matapeli.

So ni Bora kukomaa na Imani Yako kuomba mwenyewe Kwa sababu hata wao unaotaka kuwaendea sio Mungu ni watu kama wewe.
 
Sisi waafrika bado hatujaqualify kuwa binadamu.
Hatujawa na uelewa au ufahamu wa kufikiri kama binadamu anavyotakiwa kuwa, bado tuna akili zinazofanya kazi kama wanyama, mjusi, ng'ombe au nyani.

Bado tunaamini kuna mapepo, maruhani, miujiza, ulimwengu wa roho, mapopo bawa na mizimu. Wote huo ni ukosefu wa elimu, uelewa, na matokeo ya kuwa na fikra duni kama za wanyama.

Ukweli ni kwamba, ndoto ni matokeo ya ubongo.

Ubongo unafanyia kazi vitu ambavyo umewahi kuviona, kuvifanyia kazi ama kuviwaza, na ndio maana ni vigumu sana mtu kuota anafanya mapenzi na mama yake mzazi kwa sababu hajawahi kuwaza hivyo.

Sababu inayomfanya mtu aote mara kwa mara yuko shuleni ni kwa sababu ndipo sehemu pekee aliyotumia muda mrefu kuliko sehemu yeyote ya maisha yake.

Kila ukilala, ubongo ukitaka kurecall, unakutana na sehemu hiyo iko restored mara nyingi.

Lakini kwa sababu kuna watu wasio wema, wezi na matapeli, wanatumia uelewa wetu finyu, kutudanganya na kututapeli, watakuambia kuna watu wamekuroga, au wanakuzibia nyota usifanikiwe.

Post hii aione Intellectual Kiranga dada mrembo Joanah na mganga wa kienyeji Mshana Jr

Hahahahhh mkuu mbona umetoa mfano mgumu sana wa mama
 
Back
Top Bottom