Kwa mujibu wa Standing Orders, DAS ni mtumishi wa Umma

Kwa sasa Raia Namba Moja wa Tanzania anafanya chochote atakachokukifanya kukifanya. Iwe kwa majibu wa Katiba au kinyume, anajifanyia tu.

Hakuna kuhoji.Ukihoji utahojiwa.Utazingirwa.

Kama Mkurugenzi anaweza kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya nafasi maalumu kwa makada wa CCM, isitarajiwe tofauti kwenye uteuzi hata wa hao ma-DAS?

Katiba ya nchi kwa sasa ni ilani ya CCM....
 
Nani kakudanganya? Msiishi kwa mazoea. Katika awamu hii, mtu sahihi huwekwa mahala sahihi.
Mazoea yalikuwa ni kwamba mtu anawekwa kwa upendeleo bila kufanya interview. Ili kuondokana na mazoea, ikaanzishwa Public Service Recruitment Secretariat ambayo iliamua kuja na mfumo wa wazi wa ajira, na malalamiko ya 'kuwekana' yakapungua sana, ikabaki ni ushindani wa waomba ajira.

Sasa nashangaa tunarudi tena kwenye utaratibu wa kuwekana, tena unasema kabisa 'mtu sahihi anawekwa', aisee! Anawekwa na nani? Sekretarieti ya ajira yenye wataalamu wa kuchuja candidates inaachwa kando, anaibuka mtu mmoja tu na kusema eti fulani akae mahali fulani, na Jumatatu apeleke CV yake Utumishi! Ajabu sana! Yaani badala ya mtu kupeleka kwanza CV ndio aitwe kazini, eti anaitwa kwanza kazini halafu ndio anapeleka CV! Ngoja tusubiri watu wale pilau kwanza
 
Naombeni taratibu zinazotumika kuchagua hao DAS
DAS hachaguliwi,heteuliwa miongoni mwa watumishi wa umma
DAS huteuliwa miongoni kwa watumishi waandamizi wa serikali tena waliosomea masomo ya sheria , utawala na fani zinazoendana na hizo sasa hii iliyotokea naona kama ni " surprise " haya twendeni lakini
 
Mmeumia sana kwa Mtela kupewa nafasi ya UDAS. Nikuulize swali mleta mada. Kwani Mkuu wa Wilaya ni Mtumishi wa Umma ama siyo?
Lizaboni, Lizaboni, Lizaboni! please usilewe siasa kiasi hicho, huyu bwana kaleta hoja ya msingi kabisa. Tusiruhusu ukiukwaji huu wa sheria za utumishi wa umma kwani ni hatari kwa afya ya nchi. Hata kama unapeda chama chako kiasi gani, wanapokosea bora ukae kimya kuliko kuchangia mambo yasiyoeleweka.
 
All in all

Huu uteuz wa madas barua haina logo ya serikal na imeandikwa bila kuzingatia maadili ya uandishi wa kaz za serikali no sahihi huu utakua mchezo wa vijana wa mjini.

Pia haiwezekani kuacha watendaji wote wenye uzoefu naona waliobaki hawazid kumi.
 
Inawezekana kumetokea mabadiliko katika kada hii ambayo huko nyuma ilikuwa ni kwa civil servants (watumishi wa serikali) wenye ujuzi, uzoefu na utaalam wa utawala wa umma (public administration & finance). Equivalent wao kwa ngazi ya mkoa ni Regional Admnistration Officers (RAO). Wao ndiyo washauri wakuu wa kitaalamu katika masula ya utawala chini ya maafisa masuluri wa wilaya zao (DEDs) ambao kwa kawaida si watalaamu wa utawala. Hawa ni professionals wa utawala katika wilaya kama walivyo afisa mifugo, elimu, kilimo, afya nk wa wilaya. Zamani walijulikana kwa jina la Mabwana shauri. Wizara yao mama ni Wizara ya utumishi wa umma. Unaweza pia kuwaita maafisa utumishi wakuu wa wilaya. Si wanasiasa na hawapasi kuwa wanasiasa kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma.

Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ni wanasiasa wakimuwakilisha rais katika maeneo yao. Kunapotokea mabadiliko ya rais nao hubadilishwa kwa rais mpya kuteuwa watu wake anaopenda na kuwaamini wakamuwakilishe maeneo hayo ya wilaya na mikoa.

Nadhani yote haya yalizingatiwa kwenye uteuzi huu. Kuingiza wapya kwenye utumishi wa umma na kuwateua kwenye nyazifa kama hizi ni jambo la kawaida na mifano ni mingi eg Balali kwenye Bank kuu. Ni haki ya kila mtanzania mwenye sifa na uwezo. Kuwapata watu wa namna hii unaweza kutumia search committees, siyo lazima utumike utaratibu ulioutaja wa ushindanishi. Kwani si wakurugenzi kibao wameteuliwa kwa njia za search committees na hamukulalamika?
 
Na lakini wenye mamlaka ya kushauri wajue kabisa watakuja kulumiwa VIBAYA..pia wale wenye ndoto za KUUKWAA hapo baadae kama hawajui watakuja kulaumiwa kwa kushindwa kushauri ipasavyo!
 
Ni vizuri ofisi kuu ya utumishi wa umma ikatoa taarifa kamili ili kuondoa hii sintofahamu. Yaani wameteuliwa kwa vigezo gani.
 
Mie ni mara yangu ya kwanza kusikia teuzi za DAS nilizoea DC
 
Naombeni taratibu zinazotumika kuchagua hao DAS
Das ni mtumishi mostly ni afisa utawala au utumishi habari, tarafa, ambaye amefanya kaz kwa muda mrefu ndiyo anapelekwa kwenda kuendesha ofis ya mkuu wa wilaya na kuwa katibu wa kamat ya ulinz na usalama ya wilaya.

Mostly Ma DAS wanakuwa proposed na katibu tawala mkoa au katibu mkuu utumish kutoka katika list ya wataalam ambao wamefikia hatua ya kupata uteuz au waandamiz
 
angalizo muhimu
 
Na lakini wenye mamlaka ya kushauri wajue kabisa watakuja kulumiwa VIBAYA..pia wale wenye ndoto za KUUKWAA hapo baadae kama hawajui watakuja kulaumiwa kwa kushindwa kushauri ipasavyo!

Kwa sasa, ukitaka kushauri lazima uwaze Raia Namba Moja wa Tanzania anataka kusikia nini?

Ukisema asichotaka kukisikia, atakutumbua. Kwahiyo hapo sio kushauri ila kuwa kama muhuri tu-rubber-stamp:"Ndiyo Mzee".

Akimaliza muda wake mtawala mpya naye ataanza upya kuisuka nchi na kuziba nyufa zilizozijitokeza.

Katiba isipofuatwa hapo ijulikane kwamba mfumo umeshapoozwa, tutegemee "either a partial or total systemic paralysis."
 
Inasemekana hii list ni
feki.kwani imetangazwa
mahali pengine tofauti na
humu?
 
Mtoa mada uko sahihi, nadhani CV ndo hutangulia utumishi kabla ya mtu kupewa ajira sio mtu atangulie then CV ifuate.

DAS inabidi ateuliwe kati ya watumishi wa umma na sio atoke nje ya mfumo wa ajira ya serikali.
Na Mtumishi wa umma ni mtu aliyeajiriwa kupitia Sekretariet ya utumishi wa umma.
 
najua nakufundisha vitu hapa ukawaeleze na wenzio. Katibu Tawala wa Wilaya anateuliwa lakini miongoni mwa watumishi wa umma
Akirudi tena nitajua ni mwehu .
after five minutes
 
Wanaajiriwa kama watumishi wa umma tena kwa usaili kama maafisa tawala daraja la II then baadae miongoni mwao kuna wanaopata uteuzi kuwa MADAS mkuu Lizaboni.
 
Magufuri kwa kuvunja sheria za nchi hajambo.

Alimteua Mpanju kua naibu katibu mkuu wakati mpanju hakua mtumishi wa umma.

sasa anateua wanasiasa kushika nafasi za utumishi wa kudumu wa umma, DAS ni permanent & pensionable. Haya ndio matatizo ya kuteua watu kisiasa inapokuja kwenye mafao sheria zikafuatwa mtu anakosa mafao yake.

Mfano mrema aliteuliwa kua naibu waziri mkuu cheo ambacho hakikuwepo kwenye kada ya utumishi, alipostaafu hadi sasa analilia mafao yake lakini ni cheo ambacho hakikua kwenye utumishi.

Kesho mtu mwngine akitokea au ikafika muda wa kustaafu mifuko ya hifadhi ina sheria zake kwa watumishi kwenda kudai mafao akaambiwa hajatimiza vigezoa ua hajachangia muda unaomtosha aweze kupewa pension ataanza kulia.

Mshaurini mheshimiwa afuate sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…