Kwa mwaka 1 na miezi 9 Serikali ya Samia imeokoa Trilioni 20

Hivi ilikuwaje kipindi cha Jiwe TRA ikitoaga report kuwa makusanyo ni Tril 1.3, 1.4, au 1.6 watu wakawa wanabisha kuwa jamaa anapika Data! ila sasahv wanasema wamepiga zaidi hatusikii zile story za ZItto kuwa wanaendelea kupika Data!!
Shida ya Jiwe Ni kwamba alikuwa anataka kulazimisha makusanyo ya kila mwezi yafanane kiasi kwamba kupika.data kulikuwepo..

Pia ukiangalia makusanyo ya mwisho wa mwaka baada ya kujumlisha na kugawanya kwa data za kila mwezi yalikuwa haya tally ndio maana walisema anapika.

Kuhusu awamu ya 6 ni.kwamba wao hitoa takwimu kila robo na ule mwezi wenye makusanyo mengi ndio huutaja peke yake,hii inasaidia kwamba Kuna Baadhi ya miezi makusanyo yanakuwa kidogo..

Mwisho Hadi Jiwe anaondoka Madarakani wastani wa makusanyo kwa mwezi ilikuwa Til.1.4.
 
Hilo sio swala la Uchumi Ni suala la uhalisia na ukweli.

Mkopo wa WB,

Mkopo dola.mil.500 za India,

Dola mil.460 za mradi wa HEET nk nk
 
Acha siasa, serikali yetu haiwezi na hakuna iliyowahi weza timiza bajeti kama ilivyopanga
 
Mimi mwenyewe nimeshindwa kuelewa matumizi ya hiyo trilioni 20 za Mkopo.

Kwani makusanyo yetu hizo trilioni 2/mwezi zinatumika kufanya Nini?
Duu una balaa,uwe unafuatilia Bajeti za Serikali ndio utajua zinachofanya.

Soma hapa mapato na matumizi 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220614-224601.png
    53.2 KB · Views: 2
Serikali bonanza na episode za mikopo wazuri hawafi wanaendelea kula nchi
 
Acha siasa, serikali yetu haiwezi na hakuna iliyowahi weza timiza bajeti kama ilivyopanga
Usikariri na kulinganisha failures wako.kina Mwendazake na Samia..

Mwaka wa fedha ulioisha wa 2021/22 Serikali ya awamu 6 imetekeleza bajeti kwa 95% na kuna wizara Kama ya Maji ilipewa mgao kwa 100%.

Soma hapa 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220628-120243.png
    153.7 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220628-115959.png
    129 KB · Views: 2
Hii ni wastani wa kukopa Trilioni 1.05 kwa mwezi, ama wastani wa kukopa Trilioni 13 kwa mwaka. Kwa miaka 4 atakayokua madarakani hadi 2025 ataacha deni la Trilioni 51 na jumla ya Deni la taifa litakua Trilioni
Ni dalili mbaya, tazama November 2022 walishindwa hata kulipa mishahara kwa wakati na walipolipa walilipa kwa vipandevipande
 
Hiyo miradi aliyoacha jpm aliacha na hela!? 500b ni mishahara tu kwa mwezi na hiyo ni zaidi ya miaka mi5 iliyopita,kuendesha serikali siyo mishahara tu,bajeti 41b makusanyo hardly 24b,17b inatoka wapi!?
 
Hilo sio swala la Uchumi Ni suala la uhalisia na ukweli.

Mkopo wa WB,

Mkopo dola.mil.500 za India,

Dola mil.460 za mradi wa HEET nk nk
Uhalisia upi?
Mkopo upi kutoka WB, amount ipi na iliombwa lini na imetolewa lini?

Dola milioni 500 za India bank gani, ziliombwa lini na zimetolewa lini?

Leta basi ushahidi, sio hadithi.
 
Mwaka wa fedha ulioisha wa 2021/22 Serikali ya awamu 6 imetekeleza bajeti kwa 95% na kuna wizara Kama ya Maji ilipewa mgao kwa 100%.
Ni wapi yanakotoka maji hivi leo, huyo waziri wa maji ni mtu hatari sana, hizo pesa zinapelekwa kwenye miradi anazunguka nyuma kwenda kuzichukua tena
 
Mimi mwenyewe nimeshindwa kuelewa matumizi ya hiyo trilioni 20 za Mkopo.

Kwani makusanyo yetu hizo trilioni 2/mwezi zinatumika kufanya Nini?
Bajeti 41tr,makusanyo 20tr...unauliza zimeenda wapi na kwa nini tumekopa?..unapoambiwa bwawa la umeme limefika 70+% na sgr inaenda nk unadhani pesa zinatoka wapi!?
 
Unaweza kutusadia ni taasisi gani ama kampuni gani ya serikali ambayo inapata faida na kupeleka hela ama gawio serikalini?

TPA sio kampuni ya serikali, ni taasisi inayokusanga pesa kwa niaba ya serikali, TPA haifanyi biashara yoyote.

Kwenye bajeti kuu ya serikali, makusanyo ya TPA, halmashauri nk na taasisi zake zote hua yanatajwa kama mapato yasiyo ya kikodi, non tax revenues.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…