Kwa mwenendo huu wa CHADEMA, Hayati Magufuli alikuwa sahihi kizuia siasa uchwara

Kwa mwenendo huu wa CHADEMA, Hayati Magufuli alikuwa sahihi kizuia siasa uchwara

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Mara baada ya kuingia madarakani Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli alitoa angalizo kwa wanasiasa na wananchi kwa ujumla kuachana na Siasa na wajikite kwenye maendeleo.

Mh Hayati Rais Magufuli alitoa angalizo hilo kwa nia njema ila likitafsiriwa kwa kupotoshwa na wafuasi wa CHADEMA.

Leo hii tunajionea tena Chadema ikigeuka kuwa gunia la kinyesi lisilobebeka yaani hata ukilimwagia marashi ya pemba.

Kwa muktadha huu Hayati Magufuli atakumbukwa kwa kutuwekea mustakabali wa kitaifa yaani kufikiri na kutenda maendeleo.
 
Maendeleo ya kodi ya mshikamano! Makato kwenye vocha? Yaani mmeshindwa kuongeza salary kwa miaka sita mfululizo, mmeshindwa kuzuia inflation, mpo kuiba tu na sasa mnachukua hata kidogo walichonacho hao mnaowaita wanyonge!

Amen Amen nawaambia, hakuna maana ccm hata mmoja atakayeionja mbingu.
 
CCM wakiiba chaguzi kwa nini wao hawataki kugeuza shavu la pili? Watageuza tu kwa matumia ya polisi na Msajili wa vyama na TISS...
Mara baada ya kuingia madarakani Hayati Dr John Joseph Pombe Magufuli alitoa angalizo kwa wanasiasa na wananchi kwa ujumla kuachana na Siasa na wajikite kwenye maendeleo...
 
Katiba haizuii kufanya siasa ..

Ndio maana yeye alikua anapopita anasimama na msafara wake kuhutubia ..

Hazikua siasa hizo kwa miaka yake 5?
 
Mara baada ya kuingia madarakani Hayati Dr John Joseph Pombe Magufuli alitoa angalizo kwa wanasiasa na wananchi kwa ujumla kuachana na Siasa na wajikite kwenye maendeleo.
Jiulize yeye na genge lake yuko wapi leo? Unavyosema alikuwa sawa wakati hakuna kizuri kimeyokana na hicho unachosema sio mafanikio na kushidwa. Kwenye miradi ipo poa lakini kwenye siasa na sera kama hizi za corona amefanya vibaya sana mpaka leo hatuko nao wapendwa huo ndiyo ukweli

ukweli ni kwamba hawa jamaa ni sugu hawaendi popote na kibaya hawategemei pesa za serikali tena! Huu utaratibu wa kuwazuia ni kuwapa mbinu mpya ambazo ni nzuri zaidi kwao mfano sasa wanaweza kujiendesha bila kuwa na wabunge wala ruzuku! Hii ni hatua kubwa sana ambayo watu wengi hawaielewa bado.

Hawa jamaa wanabadilika kama vinyonga. Kikinge kama hamkioni ni vijana wengi sana wameongezeka hili sio zuri kwa wanafikiri iko siku wataondoka. Kama sasa wapo hawata ondoka tena.

Ni kuamua njia gani ya kutumia yote itatufikisha kwenye maridhiano ya kifaifa. Hata NCCR Mageuzi wamesema hili msiko wasikiliza hata hawa mtapiteza taifa

1. Njia ya kenya au Zanzibar ya kuuana kwanza
2. Kukutana wakati huu na kuweka misingi ya kwenda mbele
 
Alitumia kifungu gani cha katiba kukataza siasa?
... hilo swali always hawana majibu!

Justification yao ni vijikauli vya kipuuzi visivyo na any legal support - "nia njema"; "ni wakati wa kazi"; "mikutano ni kwa wabunge na madiwani kwenye maeneo yao"; "ni wakati wa kujenga uchumi"; etc. Kana kwamba vijikauli hivyo vina-override matakwa ya kikatiba na kisheria.

Sijui ni kwanini CCM wameshindwa kabisa kuilinda Katiba kwa ujumla wake na kutii baadhi ya sheria za nchi.
 
Mara baada ya kuingia madarakani Hayati Dr John Joseph Pombe Magufuli alitoa angalizo kwa wanasiasa na wananchi kwa ujumla kuachana na Siasa na wajikite kwenye maendeleo...
Nchi haiendeshwi kama guest house. Maguguli alivunja katiba aliyo apa kuilinda. Na hilo halikubaliki. Litapingwa usiku na mchana. Hadi Yesu arudi.
 
Nchi haiendeshwi kama guest house. Maguguli alivunja katiba aliyo apa kuilinda. Na hilo halikubaliki. Litapingwa usiku na mchana. Hadi Yesu arudi.
Kipengele gani cha katiba!?
Usiwe kasuku
 
Back
Top Bottom