Kwa Mzozo huu wa Congo DR na Rwanda nani ananibishia kuwa EAC haiendi kufa na Wazungu kufurahia?

Kwa Mzozo huu wa Congo DR na Rwanda nani ananibishia kuwa EAC haiendi kufa na Wazungu kufurahia?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Tayari Tanzania, Burundi na Nusu ya Wakenya wanaisapoti Congo DR huku pia Uganda na Nusu ya Wakenya wakiisapoti Rwanda.

Wazungu ambao Siku zote hawataki Kuiona Jumuiya hii ya Afrika Mashariki ikistawi wamefanikiwa Kutugombanisha na kwa Uzuzu wa Wanaogombanishwa wamekubali Kuingia katika huu Mtego wa Kimkakati.

Hivi kwa Miradi mingi ya Kimaendeleo na Kimkakati Iiliyoko katika Jumuiya hii ya EAC mnadhani Congo DR na Rwanda (Wanachama wa EAC) zikiingia Vitani hawa Marafiki zao wakubwa Tanzania hatomsaidia Congo DR au Uganda haitomsaidia Rwanda?

Mnaacha kuwa Neutral katika huu Mzozo sasa Tanzania imeamua kuchukua upande kwa Kuisaidia Kisiri Congo DR kwa mategemeo ya kupata Tenda na Fursa nyingi za Kibiashara na hata Kumegewa kidogo Madini ya Congo DR Ili yawasaidie.

Na Uganda nayo vile vile (japo Kisiri) imeamua kuwasaidia Rwanda kwa ahadi ya Kufaidika na Madini ambayo kwa 60% yako upande wa Jirani na Taifa la Rwanda na chini ya Udhibiti mzuri wa Jeshi la Rwanda.

Saaa ni rasmi kuwa Vita ya Panzi huwa ni Furaha kwa Kunguru hivyo basi Mzozo huu wa Congo DR na Rwanda na kwa nchi za Tanzania na Uganda nao kuchukua upande wa Kuzisaidia ni Ushindi mkubwa kwa Wazungu ambao wametumia Akili Kubwa Kutugombanisha ili Jumuiya ya EAC isifanikiwe na waendelee Kutugawa ili tuendelee Kuwategemea huku Wao Wakitunyonya (hasa katika Rasilimali zetu) kutokana na Upan'gang'a (Upumbavu) tulionao.

Tulianza na Free Trade, kisha Customs Union, tupo njiani kwenda katika Monetary Union kisha tumalize na Political Federation ili EAC ikamilike kwa 100% ila kwa huu Upuuzi uliochanganyika na Unafiki wetu na Chuki zetu sioni Ukamilifu huu wa Kimalengo kwenda Kutimia na baadae kila nchi itaamua kuendelea na yake.

Wenye Akili tuliliona hili zamani mno.
 
[QUOTE="GENTAMYCINE

Na Uganda nayo vile vile (japo Kisiri) imeamua kuwasaidia Rwanda kwa ahadi ya Kufaidika na Madini ambayo kwa 60% yako upande wa Jirani na Taifa la Rwanda na chini ya Udhibiti mzuri wa Jeshi la Rwanda.

Nashukuru umekiri kua Rwanda ana jeshi lake DRC ambalo limekalia rasilimali ya congo ikiwamo madini na wizi wa magogo wanayoexport Ulaya na China na kufanya wanajeshi wa Rwanda na wanausalama kumiliki ukwasi kwa dhulma wanayowafanyia wakongoman tatizo linaanzia hapo huwezi kuikalia nchi nyingine kimabavu halafu useme tuwe neutral how?
 
Mpaka sasa sijajua nini EAC inafanya katika kutatua mgogoro huu!
Mpaka sasa sijajua nini EAC inafanya katika kutatua mgogoro huu!
EAC ipi hii ya Rais Samia wa Tanzania na Rais Ndayishimiye wa Burundi kumsaidia kwa Siri Rais Tshisekedi na Congo DR yake huku Rais Museveni nae wa Uganda akimsaidia kwa ukaribu mno Mdogo wake na Nduguye Rais Kagame wa Rwanda?
 
[QUOTE="GENTAMYCINE,

Na Uganda nayo vile vile (japo Kisiri) imeamua kuwasaidia Rwanda kwa ahadi ya Kufaidika na Madini ambayo kwa 60% yako upande wa Jirani na Taifa la Rwanda na chini ya Udhibiti mzuri wa Jeshi la Rwanda.

Nashukuru umekiri kua Rwanda ana jeshi lake DRC ambalo limekalia rasilimali ya congo ikiwamo madini na wizi wa magogo wanayoexport ulaya na china na kufanya wanajeshi wa Rwanda na wanausalama kumiliki ukwasi kwa dhulma wanayowafanyia wakongoman tatizo linaanzia hapo huwezi kuikalia nchi nyingine kimabavu halafu useme tuwe neutral how?
Na nani Kakudanganya kuwa Tanzania nayo kwa Msaada wa aliyekuwa Rais wa Congo DR Swahiba Joseph Kabila, Rais wa sasa Tshisekedi na kwa Maafisa, Wanajeshi wake walioko MONUSCO na Wafanyabiashara Wakubwa nao hawaibi Madini ya Congo DR?

Huna unachokijua tulia tukufahamishe.
 
Kundi la M23 ni cover ya jeshi la Rwanda, na wazungumzaji wa lugha ya kinyarwanda ambao Rwanda inadai kuwapigania kimsingi ni Raia Wa Rwanda ambao wako Congo, kimsingi hata M23 wanapata full support kutoka Kigali, na Rwanda ni mwizi wa Rasilimali za DRC na ili hali itulie ni kupigana vita Rwanda afurushwe DRC ambapo ameikalia kwa kivuli cha waasi huku wakiwa ni full trained soldiers, ifike hatua kagame aelezwe ukweli.
 
Na nani Kakudanganya kuwa Tanzania nayo kwa Msaada wa aliyekuwa Rais wa Congo DR Swahiba Joseph Kabila, Rais wa sasa Tshisekedi na kwa Maafisa, Wanajeshi wake walioko MONUSCO na Wafanyabiashara Wakubwa nao hawaibi Madini ya Congo DR?

Huna unachokijua tulia tukufahamishe.
Saga ya maziwa makuu mtani naijua kuliko wewe, unavodhani, najua unampenda sana kagame lakini kwenye hili mimi sitaki unafiki wowote kagame aiche Congo sio kuikalia kijeshi.
 
Tunaanzia miaka ya 1999 kwenye mkataba wa Lusaka ambapo Rwanda ilitakiwa itoe majeshi yake nchini Congo, ambapo ilikua ikiwasaka iliowaita waasi wa kihutu, na baadae tuangalie Mkataba wa Rwamagana
Hao waasi wa kihutu wanatajwa kama sababu ya kuzorotesha kwa usalama huko Kivu.....Ila tukubali tu hakuna suluhu ya kijeshi kwenye huu mzozo itafanikiwa.
mtu chake
 
IMG_0719.jpg

IMG_0718.jpg

Pitia kidogo agreement ya Lusaka ili tuendelee mbele na mjadala
 
EAC ipi hii ya Rais Samia wa Tanzania na Rais Ndayishimiye wa Burundi kumsaidia kwa Siri Rais Tshisekedi na Congo DR yake huku Rais Museveni nae wa Uganda akimsaidia kwa ukaribu mno Mdogo wake na Nduguye Rais Kagame wa Rwanda?
Ndiyo hii hii, vinginevyo haina sababu za kuwepo kama viongozi wanazungukana! Na kwa hali hii kamwe hatuji fikia lengo la kuwa na umoja wa kisiasa!
 
Hao waasi wa kihutu wanatajwa kama sababu ya kuzorotesha kwa usalama huko Kivu.....Ila tukubali tu hakuna suluhu ya kijeshi kwenye huu mzozo itafanikiwa.
mtu chake

FDLR ni kisingizio cha kuifunga FARDC isilinde amani ya nchi yao ili kuifanya M23 na RDF waendelee kuikalia Congo na kuiba rasilimali huku wakiumiza raia wasio na hatia
 
Diplomasia toka 1999 lakini haikuzaa matunda hivo tsheked anachofanya ni sahihi ifikie mambo yawe wazi na dunia ijue Rwanda ni sababu kuu ya kuvuruga amani ya Congo maana kama ni waasi vipo vikundi zaidi 40 lakini M23 ndio yenye nguvu ya kufanya full attack, popote ndani ya DRC kwakua ni jeshi la nchi nyingine ndani ya nchi nyingine
 
Rwanda anaiba rasilimali za Congo sasa mlitakaje?,wazungu wanachota matani ya mali ya Congo ampigi kelele.MUNUSCO,UN wote hao ni majeshi yapo Congo kuiba full stop.
 
Ni lini Uganda na Rwanda walisuluhisha migogoro yao, mpaka leo wawe marafiki!? Hivi mpaka wa gatuna ulishafunguliwa?
 
Hakuna kitakacho vunjika, wa kuivunja jumuiya hii ni
1. Kenya
2. Uganda
3. Tanzania

Walio bakia wana weza kuondolewa ktk uanachama

Pia hizi bilateral cooperations zina agreements nyingi tofauti baina ya nchi na nchi kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi hizo nje ya jumuiya

Watanzania tutafute maarifa zaidi kuliko story za nazalia na kutunga zisizo na mpango wowote...

Nchi yetu ipo Salama na mazoezi ya utayari kila pembe ya nchi ni mazuri zaidi kwa afya ya ustawi wa taifa
 
Back
Top Bottom