Kwa namna hii upinzani Tanzania bado sana. Wanatakiwa wajifunze siasa sio propaganda uchwara. Siasa ni sayansi

Kwa namna hii upinzani Tanzania bado sana. Wanatakiwa wajifunze siasa sio propaganda uchwara. Siasa ni sayansi

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Natoa hii hoja sababu inasikitisha sana kuwa Chama cha siasa ambacho kina umri zaidi ya miaka 15 au zaidi lakini bado hakijitambui na wala hakitambui kufanya mikakati ya siasa.

Na hapa nalenga hichi chama cha Chadema ambacho sasa ni chama kikuu cha upinzani.
Inaonyesha dhahiri kuwa wao mikakati yao kisiasa ili wapate kick au umaarufu ni lazima waibue ufisadi au ubadhirifu.

Pia mkakati mwingine ni kuwa wao kujifanya kama wanaharalati fulani ambao wapo kwa ajiri ya kupambambana na wenye mamlaka.

Ninachotaka kuwaambia wana Chadema siasa ni science, ndio maana watu wanaenda kusomea hadi wanapata madegree. Siasa sio propaganda uchwara. Maana wamekariri kuibua ufisadi na uanaharakati ndio mtaji.

Mfano CAG ametoa ripoti yake ya 2019-2020 kila mwana Chadema au mpinzani utasikia anaropoka mara Ufisadi wizara ya ulinzi, mara ufisadi TPA ,mara waziri atumia bil 2.5 kula bata.Siasa za kukariri na za kishamba.Audit query ni ufisadi?

CAG anapotoa ripoti huibua Audit queries ambazo huwa zinatakiwa kujibiwa na waliokaguliwa ili kufikia muafaka. Na bunge lina kamati zake zinazohusika kuhoji hizi queries ambazo ni LAAC na PAC.

Hivyo kama wako makini wangesubiri hizi queries zijibiwe kuliko kuropoka hovyo. Na bahati nzuri mwenyekiti wa PAC ni mbunge wa Chadema.

Kama wanahoja ilipaswa kuhoji je ndani ya miaka mitano CCM chini ya Rais wa sasa ameleta matokeo gani chanya ki maendeleo? Sio kukariri tu.

Siasa ni sayansi sio porojo.
 
Kwani hizo tuhuma za ufisadi wa serikali ya ccm zimetolewa na Chadema au CAG? Acha upoyoyo
Hizi sio tuhuma za ufisadi. Ni au Audit queries kama ile tril 1.5 mliosema imepigwa kumbe uongo. Ndio maana nawaambia tulieni taratibu zifuatwe ili tujue ukweli.
 
ccm ni chama cha majizi, usiwalaumu Chadema ambao hawakusanyi kodi
Kwaiyo kazi ya wabunge wa upinzani majimboni kwao nini au kula posho, allowance bungeni?
 
chagu wa malunde,
Iondolee CCM nguvu ya dola usikie kama watasema siasa ni sayansi. Unapaswa kuwapongeza wapinzani walipofikia katika mazingira tuliyonayo ya kisiasa. Kiukweli ni kwamba tuna superficial mult party system. Na kwa uungwaji mkono wanaoupata wapinzani ni dhairi chama tawala kimechokwa! Simple logic ni kwamba hata huyu Rais aliyeko madarakani aliiingia kwa kampeni za kiupinzani.
 
Iondolee CCM nguvu ya dola usikie kama watasema siasa ni sayansi. Unapaswa kuwapongeza wapinzani walipofikia katika mazingira tuliyonayo ya kisiasa. Kiukweli ni kwamba tuna superficial mult party system. Na kwa uungwaji mkono wanaoupata wapinzani ni dhairi chama tawala kimechokwa! Simple logic ni kwamba hata huyu Rais aliyeko madarakani aliiingia kwa kampeni za kiupinzani.
Ndugu, chama dola ni chama dola tu. Ccm wanatumia dola vizuri, Polisi wanalinda raia na mali zao.Ndio maana unaona usalama umeimarika sana. Takukuru wanadhibiti rushwa na ubadhirifu,leo tu wameokokoa zaidi ya bil 80 . Magereza nao wanatimiza wajibu wao, ndio maana watu wakiingia restricted area wanakula virungu mpaka wanakiona cha moto. Hao wengine Majibu unayo maana nafikiri unajua kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom