Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kati ya jambo ambalo Wapinzani wa nchi hii hawakuwahi kulijua huko nyuma ni kwamba sehemu pekee ya kushikilia kwenye nchi hii ili tupate mabadiliko ya kweli kwa maslahi mapana ya Taifa ni KATIBA MPYA.
Uzoefu wangu katika kuwa mwanachama hai wa CCM kwa takriban Miaka 30 umenionesha vizuri sana kuwa kitu pekee kinachowapa nguvu ya kufanya walitakalo CCM na kuikosesha Tanzania Mabadiliko ya kweli ni hii KATIBA tuliyoanayo sasa.
Baada ya CHADEMA mwaka kuja na huu msimamo wa NO REFORM NO ELECTION napenda kuwahakikisha wana JF kuwa, tutarajie kuona kila sarakasi kutoka CCM, Tutarajie kuona matumizi ya kila aina ya silaha kutoka CCM mpaka kuibuliwa kwa mamluki wote ( Ku expose cover zao)
Kwa wale msiofahamu. Ni heri nchi hii tusiwe tunafanya uchaguzi kuliko kufanya maigizo kwa fedha za walipakodi yanayoitwa Uchaguzi ili kuwahaa wafadhili waendelee kutoa pesa ambazo zinaendeleza ufisadi nchini. CCM ni baba wa uongo kama alivyo shetani na wamekuwa wakiishi kwa huu uongo kwa miaka mingi sana.
Ninayasema haya kwa sababu nchini Tanzania sio kura za wananchi zinazoamua mshindi wa Uchaguzi. Wanaoamua kura ziweje yaani wapinzani wapewe ngapi na sisi tuwe na ngapi ni CCM na watu wao waliowaweka kwenye kinachoitwa TUME YA UCHAGUZI pamoja na Halmashauri zetu (Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ni Wasimamizi wa Chaguzi). Ushahidi wa hili ni maneno aliyoyasema Nape Nnauye( akiwa Waziri wa Habari jimboni kwa Byabato Mkoani Kagera). Ushahidi wa hili ni maneno aliyosema aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Longido.
Ushahidi wa haya ni maneno aliyowahi kuyatamka Rais Magufuli kuwa inakuwaje nakuteua Mkurugenzi na kukulipa Mshahara alafu Wapinzani washinde kwenye Uchaguzi unaosimamia?
Napenda kuwapongeza CHADEMA maana kiuhalisia kwa nini tufanye uchaguzi wakati sio kura zetu zinazoamua mshindi wa uchaguzi? Kwa nini tufanye uchaguzi wakati kuna watu wanakaa wanaamua tu saivi embu tuondoe majina ya wagombea wote wa upinzani ili chama chetu kishinde kwa asilimia 90?
Kwa wana JF! Tusishangae sana kuona mtiririko wa nyuzi humu kuyaponda maamuzi haya ya CHADEMA, tena kutoka kwa influential people! Kusema ukweli lazima watakuja wengi maana sehemu kuu ya CCM kuwalaghai Watanzania imekuwa ni hizi Chaguzi ambazo wanazichezea wapendavyo.
Mwisho. Napenda kuwaambia Watanzania, tuwaunge mkono CHADEMA kama tunataka kweli kulijenga vizuri hili Taifa letu.
Watu wanaoiba uchaguzi hawawezi kuwa na moral authority ya kukemea wizi wa mali zetu na fedha zetu zinazoibwa kila kukicha na kutuacha Wananchi tukiishi maisha magumu na kukosa huduma muhimu.
Watu wanaoiba uchaguzi hawawezi kuacha kuiba na kutumia vibaya kodi zetu ambazo zinapaswa kutumiwa vizuri kutujengea miondombinu mizuri ya barabara hadi majumbani kwetu, miundombinu bora ya maji na madawa ya uhakika katika hospitali zetu.
Tusimame sasa na CHADEMA ili kuitengeneza TANZANIA bora kwa vizazi vingi vinavyokuja. Kwa maslahi mapana ya nchi yetu, sote tuseme NO REFORM NO ELECTION.
Tunahitaji sasa hizi Reforms kuliko wakati wowote ule maana linapoelekea Taifa letu sio kuzuri kabisa.
Lord denning
Dubai