Kwa namna hoja ya No Reform No Election ilivyo na mashiko, Tutarajie kuwaona vibaraka wote wakiji-expose

Kati ya jambo ambalo Wapinzani wa nchi hii hawakuwahi kulijua huko nyuma ni kwamba sehemu pekee ya kushikilia kwenye nchi hii ili tupate mabadiliko ya kweli kwa maslahi mapana ya Taifa ni KATIBA MPYA.

Uzoefu wangu katika kuwa mwanachama hai wa CCM kwa takriban Miaka 30 umenionesha vizuri sana kuwa kitu pekee kinachowapa nguvu ya kufanya walitakalo CCM na kuikosesha Tanzania Mabadiliko ya kweli ni hii KATIBA tuliyoanayo sasa.

Baada ya CHADEMA mwaka kuja na huu msimamo wa NO REFORM NO ELECTION napenda kuwahakikisha wana JF kuwa, tutarajie kuona kila sarakasi kutoka CCM, Tutarajie kuona matumizi ya kila aina ya silaha kutoka CCM mpaka kuibuliwa kwa mamluki wote ( Ku expose cover zao)

Kwa wale msiofahamu. Ni heri nchi hii tusiwe tunafanya uchaguzi kuliko kufanya maigizo kwa fedha za walipakodi yanayoitwa Uchaguzi ili kuwahaa wafadhili waendelee kutoa pesa ambazo zinaendeleza ufisadi nchini. CCM ni baba wa uongo kama alivyo shetani na wamekuwa wakiishi kwa huu uongo kwa miaka mingi sana.

Ninayasema haya kwa sababu nchini Tanzania sio kura za wananchi zinazoamua mshindi wa Uchaguzi. Wanaoamua kura ziweje yaani wapinzani wapewe ngapi na sisi tuwe na ngapi ni CCM na watu wao waliowaweka kwenye kinachoitwa TUME YA UCHAGUZI pamoja na Halmashauri zetu (Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ni Wasimamizi wa Chaguzi). Ushahidi wa hili ni maneno aliyoyasema Nape Nnauye( akiwa Waziri wa Habari jimboni kwa Byabato Mkoani Kagera). Ushahidi wa hili ni maneno aliyosema aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Longido.
Ushahidi wa haya ni maneno aliyowahi kuyatamka Rais Magufuli kuwa inakuwaje nakuteua Mkurugenzi na kukulipa Mshahara alafu Wapinzani washinde kwenye Uchaguzi unaosimamia?

Napenda kuwapongeza CHADEMA maana kiuhalisia kwa nini tufanye uchaguzi wakati sio kura zetu zinazoamua mshindi wa uchaguzi? Kwa nini tufanye uchaguzi wakati kuna watu wanakaa wanaamua tu saivi embu tuondoe majina ya wagombea wote wa upinzani ili chama chetu kishinde kwa asilimia 90?

Kwa wana JF! Tusishangae sana kuona mtiririko wa nyuzi humu kuyaponda maamuzi haya ya CHADEMA, tena kutoka kwa influential people! Kusema ukweli lazima watakuja wengi maana sehemu kuu ya CCM kuwalaghai Watanzania imekuwa ni hizi Chaguzi ambazo wanazichezea wapendavyo.

Mwisho. Napenda kuwaambia Watanzania, tuwaunge mkono CHADEMA kama tunataka kweli kulijenga vizuri hili Taifa letu.

Watu wanaoiba uchaguzi hawawezi kuwa na moral authority ya kukemea wizi wa mali zetu na fedha zetu zinazoibwa kila kukicha na kutuacha Wananchi tukiishi maisha magumu na kukosa huduma muhimu.

Watu wanaoiba uchaguzi hawawezi kuacha kuiba na kutumia vibaya kodi zetu ambazo zinapaswa kutumiwa vizuri kutujengea miondombinu mizuri ya barabara hadi majumbani kwetu, miundombinu bora ya maji na madawa ya uhakika katika hospitali zetu.

Tusimame sasa na CHADEMA ili kuitengeneza TANZANIA bora kwa vizazi vingi vinavyokuja. Kwa maslahi mapana ya nchi yetu, sote tuseme NO REFORM NO ELECTION.

Tunahitaji sasa hizi Reforms kuliko wakati wowote ule maana linapoelekea Taifa letu sio kuzuri kabisa.

Lord denning
Dubai
Tunashambulia Toka ndani,

HOJA ya kupata Tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wa 2025 inashika Kasi sana.
 
Nasema hivi, angalia usije ukaliwa jicho. Ungekuwa unajiheshimu usingekuwa unaongea ukhanithi muda wote huu. Kama mumeo kashindwa kashindwa kihalali, ila unajiliza tu hapa kama bwabwa la lungalunga.
Hahahahaha hizi hasira elekeza barabarani dada acha ramli mi siwezi kulia kwaajili ya CHADEMA mi nimekaa kipembeni nione ngom yenu watoto inaishia wapi 😂😂😂😂
 
Utasubiri sana.
 
Ntasubiri sana kuwaona mnaingia barabarani ama?? Halafu ushachangia sh ngapi chamani kwanza au ndo debe tupu lisiloacha kutika?
Tuko barabarani kila siku, unataka baranara ipi tena. Kwenye NIMO nimeahaweka 55,000, na bado nitaendelea kuchanga nyingine kadiri muda unavyooenda.
 
Kati ya jambo ambalo Wapinzani wa nchi hii hawakuwahi kulijua huko nyuma ni kwamba sehemu pekee ya kushikilia kwenye nchi hii ili tupate mabadiliko ya kweli kwa maslahi mapana ya Taifa ni KATIBA MPYA.

Uzoefu wangu katika kuwa mwanachama hai wa CCM kwa takriban Miaka 30 umenionesha vizuri sana kuwa kitu pekee kinachowapa nguvu ya kufanya walitakalo CCM na kuikosesha Tanzania Mabadiliko ya kweli ni hii KATIBA tuliyoanayo sasa.

Baada ya CHADEMA mwaka kuja na huu msimamo wa NO REFORM NO ELECTION napenda kuwahakikisha wana JF kuwa, tutarajie kuona kila sarakasi kutoka CCM, Tutarajie kuona matumizi ya kila aina ya silaha kutoka CCM mpaka kuibuliwa kwa mamluki wote ( Ku expose cover zao)

Kwa wale msiofahamu. Ni heri nchi hii tusiwe tunafanya uchaguzi kuliko kufanya maigizo kwa fedha za walipakodi yanayoitwa Uchaguzi ili kuwahaa wafadhili waendelee kutoa pesa ambazo zinaendeleza ufisadi nchini. CCM ni baba wa uongo kama alivyo shetani na wamekuwa wakiishi kwa huu uongo kwa miaka mingi sana.

Ninayasema haya kwa sababu nchini Tanzania sio kura za wananchi zinazoamua mshindi wa Uchaguzi. Wanaoamua kura ziweje yaani wapinzani wapewe ngapi na sisi tuwe na ngapi ni CCM na watu wao waliowaweka kwenye kinachoitwa TUME YA UCHAGUZI pamoja na Halmashauri zetu (Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ni Wasimamizi wa Chaguzi). Ushahidi wa hili ni maneno aliyoyasema Nape Nnauye( akiwa Waziri wa Habari jimboni kwa Byabato Mkoani Kagera). Ushahidi wa hili ni maneno aliyosema aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Longido.
Ushahidi wa haya ni maneno aliyowahi kuyatamka Rais Magufuli kuwa inakuwaje nakuteua Mkurugenzi na kukulipa Mshahara alafu Wapinzani washinde kwenye Uchaguzi unaosimamia?

Napenda kuwapongeza CHADEMA maana kiuhalisia kwa nini tufanye uchaguzi wakati sio kura zetu zinazoamua mshindi wa uchaguzi? Kwa nini tufanye uchaguzi wakati kuna watu wanakaa wanaamua tu saivi embu tuondoe majina ya wagombea wote wa upinzani ili chama chetu kishinde kwa asilimia 90?

Kwa wana JF! Tusishangae sana kuona mtiririko wa nyuzi humu kuyaponda maamuzi haya ya CHADEMA, tena kutoka kwa influential people! Kusema ukweli lazima watakuja wengi maana sehemu kuu ya CCM kuwalaghai Watanzania imekuwa ni hizi Chaguzi ambazo wanazichezea wapendavyo.

Mwisho. Napenda kuwaambia Watanzania, tuwaunge mkono CHADEMA kama tunataka kweli kulijenga vizuri hili Taifa letu.

Watu wanaoiba uchaguzi hawawezi kuwa na moral authority ya kukemea wizi wa mali zetu na fedha zetu zinazoibwa kila kukicha na kutuacha Wananchi tukiishi maisha magumu na kukosa huduma muhimu.

Watu wanaoiba uchaguzi hawawezi kuacha kuiba na kutumia vibaya kodi zetu ambazo zinapaswa kutumiwa vizuri kutujengea miondombinu mizuri ya barabara hadi majumbani kwetu, miundombinu bora ya maji na madawa ya uhakika katika hospitali zetu.

Tusimame sasa na CHADEMA ili kuitengeneza TANZANIA bora kwa vizazi vingi vinavyokuja. Kwa maslahi mapana ya nchi yetu, sote tuseme NO REFORM NO ELECTION.

Tunahitaji sasa hizi Reforms kuliko wakati wowote ule maana linapoelekea Taifa letu sio kuzuri kabisa.

Lord denning
Dubai
Aisee...

Lakini safari hii, hata wawafukue nguchiro na kuwasambaza nchi nzima na kwenye mitandao yote ya kijamii, hawawezi kujibu hoja hizi kwa mipasho....

Kwani kwa kadiri wanavyoachilia mipasho yao, ndivyo wanayoonesha ujinga na upumbavu wao. HiI movement ya NO REFORMS, NO ELECTION imeshaeleweka kwa urahisi sana kwa watu karibu wote. Wanaojifanya hawaelewi ni wale tu walio upande wa dhuluma za kishetani...

Nimewaona kina Pascal Mayalla, Ansbert Ngurumo, Mzee Mwanakijiji, Nyani Ngabu na wengine kama vile tayari wameshakuwa contracted na serikali/CCM kujaribu kumshambulia Tundu Lissu na CHADEMA kama njia ya kujaribu kufifisha nguvu ya movement hii ya NO REFORMS, NO ELECTION...

Kinachosikitisha wanamshambulia mtu na kukosoa maneno ya kaulimbiu "NO REFORMS, NO ELECTION" kwamba eti hayaeleweki huku wakiacha kujibu mantiki na hoja zilizobebwa na kaulimbiu hii. Sasa watu wa namna hii watawezaje kuififisha movement hii zaidi tu kuwa wataonekana wajinga kwa kuupinga ukweli ulio wazi na unaowakodolea macho mbele yao...?

Ndugu Lord denning, hoja zilizobebwa na kaulimbiu ya harakati za NO REFORMS, NO ELECTION hazina majibu ya porojo za mdomoni au kuandika utumbo magazetini bali majibu yake ni KUTENDA KWA MAANA YA KUKAA CHINI WOTE KAMA TAIFA NA KUFANYA MAREKEBISHO YOTE MUHIMU...

Nimemtazama na kumsikiliza Tundu Lissu leo akitoa yale mapendekezo 8 ya kufanyiwa kazi ili tuingie kwenye uchaguzi ulio huru, wa wazi na wa haki, huyu jamaa wala hana tamaa kabisa ya kugombea u - Rais...

Maana kasema wazi kuwa, tukikubaliana kuwa kuna tatizo na tukaamua kufanya mabadiliko kurekebisha mfumo wetu wa uchaguzi na utawala, basi marekebisho yanaweza kuchukua hata miaka mitatu ndipo tutakapoweza kufanya uchaguzi wa kweli chini ya mifumo mipya kabisa...

Sasa Rais Samia Suluhu Hassan unataka nini tena maana CHADEMA wameshakufanyia endorsement ya kuendelea kuwa Rais hadi pengine 2027 au 2028 only if utaamua kwa dhati ya moyo wako kuwa unakubaliana na CHADEMA kufanyia mabadiliko mfumo wetu wa uchaguzi na utawala kwa kuwapa Watanzania Katiba mpya..?

Muhimu ni kuwa, do the needful before it's too late, madam president...

Lakini ukishupaza shingo mama, ukakubali kumtumikia shetani na dhuluma na kuipuuza haki, HAKIKA utakufa kabla ya wakati wako...!!
 
Back
Top Bottom