Sio kweli, shusha bei ya dizeli inayotumika kusafirisha vyakula, pandisha petrol ili kutoathiri matarajio ya bajeti, ruhusu wafanyabiashara waingize chakula bila kodi (kile tu chenye uchache sokoni), ruhusu ghala la taifa kuuzia wafanyabiashara wa ndani ili kuongeza supply sokoni kama hatua za muda mfupi, muda wa kati kusanya vijana wa SUA waliomaliza kilimo, say 10 kila group liundie kampuni kwa hisa wape hektas bure, wadhaminiwe wapewe matrekta na SUMA, mbolea, mbegu, na mashine za umwagiliaji kwa mkopo, wape wataalam wa fedha na masoko, kundi moja Rufiji Mpunga, jingine Rukwa Mahindi, jingine Mbulu Ngano uone matokeo