Kwa nilichokiona leo kuna maafa mengine yananukia tarehe 8, kitakachowaokoa ni sangoma. Yanga wanaanzia walipoishia

Kwa takwimu YANGA wamekosa sana... Nafikiri pia wajerumani hawakupania kama YANGA
 
Kwani kocha wao bado mgunda au wamemuiba Nabi airport?
 
Na hivi hawa makolo wanafungwaga kwa mujibu wa tarehe ya siku ya mechi, SUBIRI..!! Mtu anaenda kula kuanzia 8.
 
Diara ni wa 5imba?
 
Swali fikirishi je alikuwa hapewi mgao wa wazee kama upo, swali jingine je ni mwanachama hai?, Kama siyo mwanachama hai ana swali la kujibu
 
Ahmed anawajaza tu. Msijitumainishe sana kwa timu iliyoacha wachezaji 17 na kusajili wengine 17. Hiyo sio project ya mwaka mmoja kama Ahamed anavyowadanganya.
Umesoma comment kiushabiki bila kusoma ukaelewa maana. Mashindano ni mchezo wa kufukuzana, huwezi kusema upo bora kuliko wote wakati hao wenyewe unaoshindana nao hujawaona uwanjani wapoje. Mimi ni shabiki wa Yanga na wengi hapa jukwaani wananijua. Nilichoongea sio kwasababu ya maneno ya Ahmed Ally bali nimeongea uhalisia. Ni muhimu kuwaona Azam uwanjani timu yao ipoje maana na wao wameongeza quality players na pia kuona Simba nao uwanjani kisha unapata majibu juu ya wapinzani wako kuhusu mbio za ubingwa.

Kuhusu hoja ya wachezaji kuwa wengi kutokuwa project ya muda mfupi, hilo nakukatalia. Kama umefanya replacement ya wachezaji kwa usahihi (wachezaji wenye viwango) na kocha akaja mwenye kiwango sahihi (mbinu na ufundi) kuna uwezekano wa kuanza kuyaona matunda ya project yako kwa muda mfupi.

Katika wachezaji 17 waliochwa Simba, wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cha kwanza ni Chama, Saidoo, Kanoute, na Inonga hilo pia likumbukwe.

Yanga ya Nabi msimu wa 2021/2022 kuna wachezaji 10 waliachwa na 11 wakasajaliwa wapya na ubingwa akabeba. Ishu kubwa ni kusajili wachezaji wenye viwango na kocha mwenye viwango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…