tunduma001
JF-Expert Member
- Jun 7, 2021
- 795
- 1,267
Labda ni misimu tofauti vinginevyo alikuwa anadanganyaInawezekana alivuna kwa misimu tofauti tofauti. Watu wengi kijijini wanafanya hivo. Unakuta mtu anajifungia shambani kwa misimu yake kama 6 kwa miaka mi 4 au mi 3 akitoka hapo unakuta kakusanya gunia kama 500.
Kwahuyu mdau wa gunia 1400, kwa ekari hizo 60 kama angeweza kupata hata gunia 7 kwa ekari basi hapo ni misimu mi 3 tu anakuwa amekamilisha gunia 1400
Mkuu Mimi Nakaa Hapo Mwaka JanaHahahahaa... umenikumbusha kauli ya, "kuchamba koo," alipenda sana kuitumia rafiki yangu mmoja, akimaanisha Bia. Mbona zipo tu bia huku...
Au una maanisha maji kama maji? Ambayo pia yapo tele milima ya uluguru kuna mito kule ya mwaka mzima haikauki, uzembe tu wa serikali. Plus wanasiasa wa Morogoro wamelala usingizi mzito.
2014 Nililima na mkuu wa mkoa sitamtaja jina, maeneo hayo ya Kipingu, Jamaa alilima hekari 100, alipiga mpunga akavuna hadi akachoka, akawaachia na wananchi kuvuna buuuleHii ni chai hakuna kitu kama hichi umedanganya mchana kweupe huko ulipo pataja napajua vizuri sana. Kweli moro ni kuzuri lakini hapa umeongeza chumvi mkuu
Hoja zako ni dhaifu mno na ambazo hazikufanyiwa utafiti wa kina.Unajua serikali ishatoa motisha na mazingira wezeshi kiasi gani mpaka sasa kwa ujenzi wa viwanfa mkoani Morogoro? Bro fanya utafiti utaliona hilo kiko wazi kabisa.Fanya utafiti kujua skimu za umwagiliaji zinavyojengwa mkoani Morogoro,yote hayo ni maendeleo,tafiti uone barabara,vyuo,mahospitali yalivyojengwa mkoani Morogoro.Kama nia yako ni njema,tulia rudia huo utafiti wako na upanue wigo wa utafiti,utagunfua mengi sana ya maendeleoNina mwaka wa nne kwenye huu mkoa sasa. Tangu nifike hapa kwa mara ya kwanza nilikuwa mtembezi sana, ili kufahamu maeneo, uchumi, na tabia za wenyeji wa huu mkoa.
Niligundua mambo yafuatayo:
1. Wenyeji ni watu wasio na makuu na waungwana (kama tu tabia za Wazaramo na makabila ya Pwani), ni wavivu (hilo nilithibitisha mara nyingi. Lakini huu uvivu wa hawa watu unafanya mkoa uwe na ombwe la fursa nyingi za kiuchumi, nitaieleza kwa kina)
2. Una vivutio vingi sana vya kitalii ambavyo vingeweza kuufanya huu mkoa kuwa na volume kubwa ya shughuli za kitalii kama ilivyo Arusha, lakini hali haipo hivyo.
3. Ni mkoa ambao biashara zinakuwa kwa kasi sana. Mahoteli mengi ya Morogoro yanatengeneza pesa sana na biashara nyingine zinazotesa huku ni chakula, bidhaa za mavazi, na vitu vya nyumbani. (Kwenye chakula, hii imechochewa zaidi na tabia za waluguru kuwa wavivu wavivu, kwahiyo wao kupika mara kwa mara inakuwa ngumu kidogo--wanapenda kula migahawani). Hizo biashara zimetengeneza pesa sana.
4. Ni centre nzuri sana ya kufanya manufacturing ya viwandani, kwasababu mbili kubwa kwamba ipo jirani na masoko yanayochipukia kama Dodoma, Iringa, na Mbeya. Na kuna faida ya nguvu kazi nafuu, ipo ya kutosha. Wenyeji wanazaliana kama panya.
5. Miaka 3 iliyopita manispaa ya Morogoro imeshuhudia ongezeko kubwa sana la idadi ya watu, na hii pia imechangia pakubwa ukuaji mkubwa wa biashara kwa miaka hii mitatu ilopita.
Mambo hayo yakaifanya Morogoro ikue kiuchumi mpaka leo hii ipo nafasi ya tatu kitaifa nyuma ya Dar es salaam na Mwanza, ikiwa na mchango wa Trillioni 9... kama sijakosea.
Kwa karatasi inaonekana ni performance nzuri ya kiuchumi, ila ukilinganisha na potential ya huu mkoa, ingepeswa kuwa ya pili kitaifa ikiwa na uchumi usiopungua Trillion 15.
Kwahiyo unaweza kusema: mkoa wa Morogoro ni sleeping giant. Na mimi binafsi nailaumu sana serikali ya CCM kwa hilo.
Kwanini nailaumu CCM?
Uchumi wa Morogoro, pamoja na kuwa na potentials nyingi za rapid growth ila bado umefungiwa kwenye kichumba--kwenye minyororo.
1. Ni vigumu mtu kupanda ndege ukitokea Morogoro kwenda nje ya mkoa (kwasababu hakuna uwanja wa kutua ndege kubwa). Hii kitu ilinishangaza sana kwamba, mkoa wenye potential kubwa sana ya biashara ya utalii inakosaje uwanja wa ndege mkubwa?
Ikanibidi niingie chimbo kuchunguza ni kwanini. Nilichokigundua kikanifanya niamini kwamba, kuna baadhi ya maeneo nchi hii, umasikini unatengenezwa kwa makusudi na serikali ya CCM.
Niligundua ya kwamba Morogoro hakuna uwanja mkubwa wa ndege wa kiraia kwasababu kuna uwanja wa ndege wa kijeshi wa Ngerengere. Kwahiyo nikaambiwa kwamba, ili kuzuia mgongano wa rada za kijeshi na ndege za raia basi hakutakiwi kuwe na uwanja wala ndege za abiria kukatiza hapo.
Kwakuwa sababu yenyewe ilikuwa imekaa ki-usalama basi sikutaka kuendelea kuhoji zaidi.
Lakini swali moja nililibakiwa nalo najiuliza ni hili: ina maana serikali ya CCM wanaona ni sawa tu kuifungia potential ya zaidi ya Trillioni 6 (ambayo ingeweza kuongezeka kwenye mkoa wa Morogoro), kwa kukataa kujenga uwanja mkubwa wa ndege ambao utaufungua mkoa wa Morogoro?
Ni kwanini basi uwanja huo wa kijeshi na amana zake zisihamishiwe mkoa wa Lindi ambao upo jirani na Morogoro?
Ili huo uwanja wa kijeshi wa Ngerengere ufanyiwe expansion na kuanza kutumika kama uwanja wa ndege wa kiraia. Na jeshi wao wahamie Lindi kujenga uwanja wa ndege.
Na jeshi wanaweza kufanya leasing ya huo uwanja wa Ngerengere na ikawa inakusanya mapato yote ambayo wanaweza kuyatumia ku finance huo uwanja huko Lindi.
Hilo likifanyika, uchumi wa mkoa wa Morogoro utafunguka kwa kasi sana. Sekta ya utalii, madini, kilimo na biashara vitakuwa kwa kasi sana, kwasababu hizo sekta, hapa Morogoro ndo nyumbani kwake.
Ila kwa akili ilotumika MO29, sina imani kama serikali ya CCM wataweza kufanya hili jambo kwa umakini na kwa wakati sahihi, kwasababu wakati ni sasa!
Wenu
MC
Naona shida labda ni miundo mbini haiendi na kasi ya mahitaji. Maana yake kwa hapa Moro vyanzo vya maji ni vya kutosha ila shida ni miundombinu haijajiweka tayari. Maana yake unaambiwa kuna ukame lakini ukicheki milimani bado maji kwenye mito yapo tu. Ndo tatizo hiloMkuu Mimi Nakaa Hapo Mwaka Jana
Mji Ulikuwa Unapata Litres Millions 20 Kwa Siki
Yalipokauka Juu Kwenye Vyanzo
Yakapatikana Millions 8
Vyanzo Vipo Ila Tunachezewa Tu
Serikali inatoa motisha na sikatai hilo; ila tambua kwamba motisha peke yake haiwezi kuchechemua uchumi wa eneo ikiwa kuna nguzo ya muundombinu ya kimkakati.Hoja zako ni dhaifu mno na ambazo hazikufanyiwa utafiti wa kina.Unajua serikali ishatoa motisha na mazingira wezeshi kiasi gani mpaka sasa kwa ujenzi wa viwanfa mkoani Morogoro? Bro fanya utafiti utaliona hilo kiko wazi kabisa.Fanya utafiti kujua skimu za umwagiliaji zinavyojengwa mkoani Morogoro,yote hayo ni maendeleo,tafiti uone barabara,vyuo,mahospitali yalivyojengwa mkoani Morogoro.Kama nia yako ni njema,tulia rudia huo utafiti wako na upanue wigo wa utafiti,utagunfua mengi sana ya maendeleo
Na madini kweli yapo ya kutosha. Ukiwa unaenda njia ya Iringa jioni unapishana na vijana wengi sana na vikarai vyao wakitafuta dhahabu. Wanapata sana.Morogoro ni Mkoa tajiri kuliko mikoa karibu yote!
Inavivutio vingi kushinda mikoa yote
Ina mito ya maji kushinda mikoa yote,
Ina mbuga za wanyama kuliko mikoa yote, Mkoa ule una dhahabu na madini kibao, unamaeneo makubwa ya kilimo n.k
Morogoro Umecheleweshwa kimaendeleo kwa maksudi na liccm
Maana yake hapo ulipata karibu gunia 20 kwa ekari ambayo ni kubwa.2014 Nililima na mkuu wa mkoa sitamtaja jina, maeneo hayo ya Kipingu, Jamaa alilima hekari 100, alipiga mpunga akavuna hadi akachoka, akawaachia na wananchi kuvuna buuule
Yule jamaa alitutengenezea na daraja la mto ambao ulikuwa ukisumbua kuingiza tractor ng'ambo ya pili
Kama kweli umewahi kuwepo huko, bila shaka unalikumbuka tukio hili
Mwaka 2014, Kipingu wakati naingia, niliingia kwa majaribio nikaanzana hekar 10 na mwaka uliofuata ndipo nikapiga ekari 60,
Mkuu, nilipiga mpunga gunia 1400+ Hutaki Acha!
Morogoro ikifunguliwa zile mbuga zipewe wakulima, Morogoro inaweza kulisha Afrca mashariki yoote
Kwa mauzo ya kila mwaka ya korosho yale mabilioni ni mengi sana. Natumai maendeleo kwenye kaya yanaonekana maana si pesa zinarudi mfukoni mwa watu?Hata sisi wa huku Mtwara, Masasi ndo hivyo tu tunatuhujumiwa😁
Hela za Korosho zinazomwagika huku isingetakiwa tuwe nyumanyuma namna hii.. tunataka viwanda Kila Kona na Barabara njia nne Toka Mtwara to Masasi
Upo sahihi kabisa. Nahisi pia sababu nyingine ya uhalisia kutokuendana na potential ya mkoa ni kwamba kuna factor ya wenyeji kuwa na aina fulani ya uvivu, kwahiyo hawawekezi sana kwenye kilimo. Utagundua pia wengi wanaolima mashamba makubwa ya mpunga kule Ifakara ni wageni.Kuwa na mkoa kama Morogoro tu katika nchi hii ilipaswa kutufanya tusahau kabisa kitu kinachoitwa njaa hapa Tanzania, kwa sababu ni mkoa ambao una aridhi kubwa yenye rutuba inayokubali almost mazao yote ya chakula.
Morogoro tu peke yake inaweza kutulisha watu wote tuliopo hapa Afrika Mashariki mpaka tukawa tunavimbiwa na chakula kingine tukagawa.
Estimately africa mashariki nzima tunatumia mchele kama ton 5m kwa mwaka, yaan population nzima ya EAC karibu ya watu 180m tunakula wali usiozidi ton 6m tu.
Sasa basi kwa mujibu wa R&D INSTITUTE hii ni taasisi ya Israel inayojihusisha na researches za kilimo miaka fulani ya nyuma report yao ilionesha kuwa Morogoro pekee ina potential ya kuzalisha mchele zaidi ya tani 10m kwa Mwaka.
Morogoro ulipaswa kuwa moja ya mkoa tajiri sana hapa Afrika mashariki basi tu.
Ni suala la kuwa na watu makini tu wenye maono kitu ambacho tumekosa.
Maybe miaka ya huko mbeleni watakuja watu wenye maono na dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo watafanya mambo ambayo tunatamani kuyaona.
CCM ndio adui wa kwanza wa taifa hili.
Mkoa ukiikumbatia sana ccm hausongi mbeleNina mwaka wa nne kwenye huu mkoa sasa. Tangu nifike hapa kwa mara ya kwanza nilikuwa mtembezi sana, ili kufahamu maeneo, uchumi, na tabia za wenyeji wa huu mkoa.
Niligundua mambo yafuatayo:
1. Wenyeji ni watu wasio na makuu na waungwana (kama tu tabia za Wazaramo na makabila ya Pwani), ni wavivu (hilo nilithibitisha mara nyingi. Lakini huu uvivu wa hawa watu unafanya mkoa uwe na ombwe la fursa nyingi za kiuchumi, nitaieleza kwa kina)
2. Una vivutio vingi sana vya kitalii ambavyo vingeweza kuufanya huu mkoa kuwa na volume kubwa ya shughuli za kitalii kama ilivyo Arusha, lakini hali haipo hivyo.
3. Ni mkoa ambao biashara zinakuwa kwa kasi sana. Mahoteli mengi ya Morogoro yanatengeneza pesa sana na biashara nyingine zinazotesa huku ni chakula, bidhaa za mavazi, na vitu vya nyumbani. (Kwenye chakula, hii imechochewa zaidi na tabia za waluguru kuwa wavivu wavivu, kwahiyo wao kupika mara kwa mara inakuwa ngumu kidogo--wanapenda kula migahawani). Hizo biashara zimetengeneza pesa sana.
4. Ni centre nzuri sana ya kufanya manufacturing ya viwandani, kwasababu mbili kubwa kwamba ipo jirani na masoko yanayochipukia kama Dodoma, Iringa, na Mbeya. Na kuna faida ya nguvu kazi nafuu, ipo ya kutosha. Wenyeji wanazaliana kama panya.
5. Miaka 3 iliyopita manispaa ya Morogoro imeshuhudia ongezeko kubwa sana la idadi ya watu, na hii pia imechangia pakubwa ukuaji mkubwa wa biashara kwa miaka hii mitatu ilopita.
Mambo hayo yakaifanya Morogoro ikue kiuchumi mpaka leo hii ipo nafasi ya tatu kitaifa nyuma ya Dar es salaam na Mwanza, ikiwa na mchango wa Trillioni 9... kama sijakosea.
Kwa karatasi inaonekana ni performance nzuri ya kiuchumi, ila ukilinganisha na potential ya huu mkoa, ingepeswa kuwa ya pili kitaifa ikiwa na uchumi usiopungua Trillion 15.
Kwahiyo unaweza kusema: mkoa wa Morogoro ni sleeping giant. Na mimi binafsi nailaumu sana serikali ya CCM kwa hilo.
Kwanini nailaumu CCM?
Uchumi wa Morogoro, pamoja na kuwa na potentials nyingi za rapid growth ila bado umefungiwa kwenye kichumba--kwenye minyororo.
1. Ni vigumu mtu kupanda ndege ukitokea Morogoro kwenda nje ya mkoa (kwasababu hakuna uwanja wa kutua ndege kubwa). Hii kitu ilinishangaza sana kwamba, mkoa wenye potential kubwa sana ya biashara ya utalii inakosaje uwanja wa ndege mkubwa?
Ikanibidi niingie chimbo kuchunguza ni kwanini. Nilichokigundua kikanifanya niamini kwamba, kuna baadhi ya maeneo nchi hii, umasikini unatengenezwa kwa makusudi na serikali ya CCM.
Niligundua ya kwamba Morogoro hakuna uwanja mkubwa wa ndege wa kiraia kwasababu kuna uwanja wa ndege wa kijeshi wa Ngerengere. Kwahiyo nikaambiwa kwamba, ili kuzuia mgongano wa rada za kijeshi na ndege za raia basi hakutakiwi kuwe na uwanja wala ndege za abiria kukatiza hapo.
Kwakuwa sababu yenyewe ilikuwa imekaa ki-usalama basi sikutaka kuendelea kuhoji zaidi.
Lakini swali moja nililibakiwa nalo najiuliza ni hili: ina maana serikali ya CCM wanaona ni sawa tu kuifungia potential ya zaidi ya Trillioni 6 (ambayo ingeweza kuongezeka kwenye mkoa wa Morogoro), kwa kukataa kujenga uwanja mkubwa wa ndege ambao utaufungua mkoa wa Morogoro?
Ni kwanini basi uwanja huo wa kijeshi na amana zake zisihamishiwe mkoa wa Lindi ambao upo jirani na Morogoro?
Ili huo uwanja wa kijeshi wa Ngerengere ufanyiwe expansion na kuanza kutumika kama uwanja wa ndege wa kiraia. Na jeshi wao wahamie Lindi kujenga uwanja wa ndege.
Na jeshi wanaweza kufanya leasing ya huo uwanja wa Ngerengere na ikawa inakusanya mapato yote ambayo wanaweza kuyatumia ku finance huo uwanja huko Lindi.
Hilo likifanyika, uchumi wa mkoa wa Morogoro utafunguka kwa kasi sana. Sekta ya utalii, madini, kilimo na biashara vitakuwa kwa kasi sana, kwasababu hizo sekta, hapa Morogoro ndo nyumbani kwake.
Ila kwa akili ilotumika MO29, sina imani kama serikali ya CCM wataweza kufanya hili jambo kwa umakini na kwa wakati sahihi, kwasababu wakati ni sasa!
Wenu
MC
MORO MSALABANIKule msalabani kwenye milima ya Uluguru, hauwezi kutembea 1 km bila kuvuka mto/mito. Mito ni mingi sana saana.
Kule wakilima hawajui mbolea ni nini, muda wote ardhi ni kijani. Mida ya usiku tu ukiingia ndani hasa saa 3 kwenda mbele, utasikia sauti za mito ya maji yanavyoteremka kutoka milimani.
Hapo kama una stress zako ukiangalia hiyo mandhari lazima zipoteeMORO MSALABANIView attachment 3533695
Ha ha haMORO MSALABANIView attachment 3533695
Na wasukuma wanajua kufanya kazi za kilima hatari sana. Anaweza kujifungia shambani miaka 5 akitoka hapo unakuta ameweka ndani magunia 700 akipiga bei hapo mtaji tayari. Ndo maisha ila inahitaji uvumilivu.Wasukuma wamekimbilia huku kulima mpunga
Mashine za kukoboa mpunga zimejaa wasukuma kweli huku pesa IPO shamba