Kwa nilichokiona Morogoro, ni sahihi kusema Serikali ya CCM inachelewesha maendeleo ya huu mkoa kwa makusudi kabisa!

Nimepita dutumi juzi, mbele kidogo ya kona ya kolelo, kuna wachina wamezungusha uzio mkubwa mno, wenyeji wananiambia ukikatiza ndani ya huo uzio unakula shaba,

Nimeambiwa wachina wanachomba dhahabu ma madini mengine ambayo wenyeji hawayajui, nimetamani na mimi niombe kibali cha kufanya utafiti upande wa pili wa mlima huo ili kama nikiona panafaa nikaanzishe mgodi huko, nilipita pia mvuha, pana mto pale mwisho wa centre ya kijiji(mji mdogo) pembeni ya mto kuna tangazo kuubwa, "Mto huu una mamba wengi, epuka kufanya shughuli zozote ndani ya mto hasa kukiwa na maji mengi" lakini cha ajabu nilikuta watoto kama wote wakiogelea humo bila hofu, ntarudi moro.
Mkuu, hapa ndiyo pale wanapopasua yale mawe meupe? Naona pia mchina amepiga kambi hapo, ila wenyeji wanasema ni mradi wa Vigogo.
 
Kinachonishangaza mimi ni kwamba, wachina huwa wanakuwa na taarifa kama hizi mapema sana. Nadhani zile tenda za ujenzi wa mabarabara zimewasaifia sana kufanya intelligence ya ni wapi nchi hii kuna madini.

Always, wapo on-target kuliko sisi wazawa. Wana taarifa nyingi sana kuliko sisi. Naipa kongole intelligensia yao ya kiuchumi. Wapo mbele ya muda siku zote.
 

Mkulima hata akifautu kulima na kupata mazao vzuri, Anapigwa kwenye bei kwa sababu serikali haitaki kuweka sera nzuri za bei, Ambazo zitapandisha bei ya chakula na iufanya wapiga kura walalamike.

Mataifa yenye kuthamini kazi ya mkulima, Serikali ikitaka kushusha bei ya Mazao ina fanya subsides, ila hapa kwetu ni kufunga mipaka tuu vyakula vilundikane bei ishuke
 

Nimekaa Morogoro 2017 - 2023, Hakuna barabara kubwa potential Imejengwa huko.

Zilizopo zinaaanza kubomoka tu hovyo, Labda kikuu kilichofanyika ni kuhamisha stand ya dara dara.

Serikali haijautendea haki mkoa wa morogoro.
 
Moja kati ya upumbavu wa CCM ni kuishi kwa akili na fikra za enzi za cold war.

Uwanja wa ndege kutokuwepo Morogoro kisa kuna uwanja wa ndege wa kijeshi ni ujinga wa hali ya juu.

Marekani ina military bases sehemu nyingi tu duniani na zinajulikana na hakuna zuio la eneo fulani kutokua na uwanja wa ndege za kiraia.
 
Wakifungua hizo fursa Machawa watawapataje?
 
Siku zote wakulima wa mazao ya chakula huitwa wavivu kwa sababu ni kilimo kisicho na faida kubwa.
Utakuta mtu wa kanda zenye ukame na njaa, kanda zisizo na hela yeyote kwenye mzunguko anawakanda Watu wa Morogoro kubwa ni wavivu.
 
Siku zote wakulima wa mazao ya chakula huitwa wavivu kwa sababu ni kilimo kisicho na faida kubwa.
Utakuta mtu wa kanda zenye ukame na njaa, kanda zisizo na hela yeyote kwenye mzunguko anawakanda Watu wa Morogoro kubwa ni wavivu.

Ndo nichokisema siku zoote.

Umasikini wa Wilaya zoote zinazo jihusisha na kilimo unaletwa na Serikali Makusudi, Yaani inawadidimiza wakulima kwa bei mbovu za soko, huku wafanyakazi na Madalali wakipeta tu

Asilimia kubwa wanao faidika na Kilimo ni Madalali au watu wanaofanya kilimo kama second business.
 
Pamoja na kukaaa Morogoro na kuwa na hoja nzuri lakini umeshindwa kuitetea

Mkoa wa Morogoro una nafasi ya kipekee kijiografia na kiikolojia kiasi cha kuweza kuilisha Tanzania nzima na kubakiwa na ziada ya kuuza nje ya nchi. Ukiwa na ukubwa wa takriban kilomita za mraba 70,624, mkoa huu umebarikiwa ardhi oevu, mabonde yenye rutuba, na mvua za uhakika.

Morogoro ni kinara wa uzalishaji wa mpunga, ukiwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 800,000 kwa mwaka, hasa kutoka Bonde la Kilombero. Bonde hili pekee lina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya mchele nchini ikiwa asilimia 100 ya ardhi yake itatumiwa kisasa.
Mbali na mpunga, mkoa huu unachangia kwa kiasi kikubwa katika zao la mahindi, ambapo uzalishaji unazidi tani 400,000 kwa msimu. Takwimu zinaonyesha kuwa mkoa una maeneo ya umwagiliaji yanayozidi hekta 500,000, lakini ni sehemu ndogo tu inayotumika kwa sasa.

Ili kufikia uwezo wake kamili, Morogoro inahitaji:
-Matumizi ya mbegu bora na mbolea kuongeza gunia kutoka 15 hadi 40 kwa ekari.

-Ujenzi wa maghala ya baridi na viwanda vya kusindika mazao ili kupunguza upotevu wa asilimia 30 unaotokea sasa baada ya mavuno.
Kwa kuwekeza kwenye miundombinu hii, Morogoro si tu itahakikisha usalama wa chakula, bali itakuwa injini ya uchumi wa viwanda nchini Tanzania.
 
Karibu sana Morogoro, hutojutia uwekezaji wako. In 10 years huu ndo mkoa pili wenye uchumi mkubwa hapa Tanzania.

So, sio mbaya ukianza kutega mitego sasahivi.
Sekta zipi ni nafuu kwa uchumi wetu wa wazawa, na vipi kuhusu maeneo ya kuishi. Makazi mazuri ambayo huduma za kijamii zimefika ni wapi, na gharama za kupata viwanja zipoje.
 
Hahahahaa... umenikumbusha kauli ya, "kuchamba koo," alipenda sana kuitumia rafiki yangu mmoja, akimaanisha Bia. Mbona zipo tu bia huku...
Nakumbuka miaka kama mitatu iliyopita wikiend moja hivi nilishawahi kufanya balaa zito sana pale samaki samaki. Kesho yake nikaondoka

Mwenyeji wangu niliyekua nae siku hiyo akawa ananiambia oya manager na wale mademu tuliokua nao siku ile kila siku wanakuulizia.

Hivi samakisamaki bado ipo?
 
Tanganyika ilivyo Kila mkoa narudia KILA MKOA una potential ya kuwatajirisha wakaazi wake. Tatizo CCM wanaona ni ufahari wananchi wengi kuwa wanyonge.

Ufukara wa wananchi ni mtaji kwa cartel iliyojificha ndani ya ccm.
 
Mkuu labda kama unafurahisha genge sawa ila unachokisema hakiwezekani kwa msimu mmoja yani hekari 60 utoe gunia 1400
Mkuu labda kama unafurahisha genge tu ila unachoandika hakiwezekani huko unapopataja yani hekari 60 zitoe gunia 1400+ mm nna miaka mingi tu nalima huko kipingu napajua vizuri na wilaya yote ya mlimba, kuhusu mawaziri kulima, huko wapo kibao ushawahi kusikia kuhusu mashamba ya balali?huyu huyu wa benki kuu yalileta shida sana, ushawahi kusikia kuhusu mashamba ya beno ndulu? Huyu alijenga mpaka daraja la chuma na kushikiza uletwaji wa umeme huko mlimba, mkuu gunia 1400+ kwa hekari 60 maana yake kila heka ulipata zaidi ya gunia 23+ hii kitu hata irrigation scheme ya hapo mbingu haitoi gunia hizo ndo maana nasema unadanganya
 
Kama ulivuna misimu tofauti tofauti na ukapata hizo gunia nakubali ila kama ni msimu mmoja nakataa
 
Kwenye upande wa soko, sera mbovu za serikali ni kutaka ku regulate soko kwa kuzuia wakulima kuuza nje au kupanga bei ambayo haiendani na uhalisia wa soko.

Subsidy kwa Tanzania hatuwezi ni gharama sana
 
Upo sahihi, kutokuwa na uwanja wa kiraia kwa sababu ya uwanja wa kijeshi ni sera mbovu. Ingekuwa ni hivo America na maviwanja ya ndege aliyokuwa nayo si miji mingi sana duniani ingeathirika, lakini haipo hivo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…