Kwa nilichokiona Morogoro, ni sahihi kusema Serikali ya CCM inachelewesha maendeleo ya huu mkoa kwa makusudi kabisa!

Siku zote wakulima wa mazao ya chakula huitwa wavivu kwa sababu ni kilimo kisicho na faida kubwa.
Utakuta mtu wa kanda zenye ukame na njaa, kanda zisizo na hela yeyote kwenye mzunguko anawakanda Watu wa Morogoro kubwa ni wavivu.
Kuhusu uvivu wa watu wa Morogoro mbona halina ubishi hilo
 
Kwenye kilimo sikupungi, na sijagusia kilimo kwasababu kwa Morogoro inafahamika kwamba ina tija kubwa kwenye kilimo.

Kinachonikera ni Mkoa kutokuwa na uwanja wa ndege, na ndio hoja yangu imelala hapo kwamba inazuia fursa ya kukua kwa sekta ya utalii na madini ambayo kama kungekuwa na ungechechemua sana ukuaji wa uchumi wa huu mkoa.

Potential ya Morogoro imejadiliwa kwa miaka mingi ila vizuizi kufikia hiyo potential ni vingi sana, na kwenye hivo vizuizi huwezi kuacha kuitaja CCM
 
Mazao ya chakula mengi ni perishable kwa hiyo huwezi kutinga sana na hayahitajiwi na viwanda.
Na viwanda vya kusindika vinahitaji soko la vyakula vilivyosindikwa, hilo soko halipo Tanzania.
Matokeo yake, mtu atakula tembele chap na dagaa na kuacha mambo ya mboga za makopo.
 
Sekta zipi ni nafuu kwa uchumi wetu wa wazawa, na vipi kuhusu maeneo ya kuishi. Makazi mazuri ambayo huduma za kijamii zimefika ni wapi, na gharama za kupata viwanja zipoje.
Kwa wazawa kama kawaida huwezi kuiacha sekta ya uchuuzi wa fast moving consumer goods, na hii ni kwasababu mkoa unakua, sekta ya ujenzi kwasababu mji unapanuka kwa kasi.

Ila sekta ambayo bado ipo underdeveloped ambayo kama kukiwa na uwanja wa ndege, ni sekta ya utalii.

Halafu ingine iliyojificha ni minerals trading, Morogoro kuna madini mengi lakini hakuna soko wazi la madini, hivi biashara nyingi ya madini inafanyika kwenye black market.
 
Kuhusu uvivu wa watu wa Morogoro mbona halina ubishi hilo
Hiyo ni dhana tu kuwa Watu wa Pwani ni wavivu.
Sasa kabila la Watu wavivu ndilo limeisha Dar es salaam miaka nenda rudi na kama fundi ujenzi wako siyo mluguru achana nae.
Vivyo hivyo, Wakenya husema wa bongo ni wavivu, hiyo ni dhana tu.
Nenda vingi vya wasukuma au waha huko, ujionee njaa na uchafu, usipime.
 
Morogoro iko takriban km 200 kutoka Dar es Salaam, ambako kuna Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). Kibiashara, imeonekana kuwa rahisi na nafuu zaidi wasafiri kutumia Dar kisha kusafiri kwa barabara au reli kwenda Morogoro.

Kwa muda mrefu, idadi ya wasafiri wa ndege kwenda Morogoro imekuwa ndogo ukilinganisha na mikoa kama Arusha, Mwanza au Zanzibar. Serikali na sekta binafsi zimekuwa hazioni traffic ya kutosha kuhalalisha uwekezaji mkubwa wa uwanja wa ndege wa kibiashara.
 
I Ipo sana kama kawaida yake na mambo yake
 
Tanganyika ilivyo Kila mkoa narudia KILA MKOA una potential ya kuwatajirisha wakaazi wake. Tatizo CCM wanaona ni ufahari wananchi wengi kuwa wanyonge.

Ufukara wa wananchi ni mtaji kwa cartel iliyojificha ndani ya ccm.
Sasa wanasiasa watapata wapi watu wa kuwaahidi matundu ya vyoo
 
Kama ulivuna misimu tofauti tofauti na ukapata hizo gunia nakubali ila kama ni msimu mmoja nakataa
Ila inawezekana alipata hizo gunia. Hiyo si ni tani 2 kwa ekari? Kimahesabu inawezekana kama alilima kisasa
 
Huo utamaduni utabadilika. Vyakula vya makopo havitakwepeka huko tuendapo. Na hiyo ndo fursa kubwa sana ya kiuchumi itayochipukia miaka michache ijayo.
 
Unatetea hiyo sera lakini hai make sense, naona unajaribu kwa nguvu sana. Yaani mtalii umsafirishe masaa 5 hadi 6 kwenye barabara yenye foleni kubwa ili tu aende Morogoro kutalii, we huoni kwamba kuna watalii wengi tu wanabadili gia angani kwa hiyo factor?

Unasema Moro haina wasafiri wengi wa ndege nakataa, kwani chato ilithibitika kuwa na wasafiri wengi wa ndege kuliko Morogoro? Mbona wao wana uwanja mkubwa wa ndege?

Kubali ni sera mbovu za CCM
 
Ila inawezekana alipata hizo gunia. Hiyo si ni tani 2 kwa ekari? Kimahesabu inawezekana kama alilima kisasa
Mkuu sisi wengine tupo kwa ground kabisa achana na hesabu za makaratasi wala vipindi vya tv, hekari 60 kutoa gunia 1400+ ni uongo, kuna eneo linaitwa njage lina iyo irrigation scheme na wanalima kisasa kabisa ila hekari 1 inatoa gunia 15/17 sio 23+. Mkuu mambo ni tofauti kabisa kuna maeneo hekari 1 inatoa gunia 7/8 kwa hiyo sio rahisi kama wengi wanavyofikiria
Note:nna uzoefu na kilimo hizo sehemu za kipingu na maeneo mengine bonde la kilombero(wilaya za mlimba na malinyi)
 
Two wrongs don't not make one right. Je ndege bado zinakwenda Chato baada ya Magufuli kufa?

Nchi lazima iwe na priority. Yawezekana kuna mambo muhimu ya kufanya Morogoro kuliko huo uwanja wa ndege
 
Uzoefu kweli unaonesha wastani kwa aina ya namna tunavyolima mavuno ni kama gunia 12 kwa ekari (tani 1.2) na hii ni kwa wakulima wadogo wadogo. Ila kwenye vitabu inaonesha yield inaweza ikaenda mpaka tani 5 kwa ekari 1.

Kwa huyu mdau yeye inamaana alipata kama wastani wa tani 2.3 kwa ekari ambayo ipo ndani ya wastani wa makadirio ya vitabuni.

Ndo maana najiepusha kukataa moja kwa moja; hatujui ikiwa alitumia kilimo cha kitaalamu na aliotesha mbegu za kisasa. Kwahiyo mimi ni kama kwa kiasi kikubwa naamini ni kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…