Kwa niliyoyashuhudia katika Uchaguzi huu, Poleni viongozi wa Upinzani

Kwa niliyoyashuhudia katika Uchaguzi huu, Poleni viongozi wa Upinzani

Futeni uchaguzi tusiharibu hela za walipa kodi.... Ni vyema kikabaki chama kimoja maisha mengine yaendelee.... Nilioyaona jana sitojishirikisha tena na kitu kinaitwa uchaguzi.
 
Mwenye akili kubwa, huwa haamini kama kuna mtu asiye kuwa na mazuri na madhaifu

Siasa za upinzani, haziami hivyo, wao wanaamini kuwa, nje ya Upinzani hakuna mtu aliye na mazuri Isipokuwa kuna mtu mwenye mabaya tu, yaani yeye ni wa mabaya tu siku zote hata angefanya nini, atafanya mabaya tu

Hiyo ndiyo leo imewaangushaa wapinzani,

Eti Magufuli hakufanya chochote kabisa, na kila alichokifanya hakifai na hakuna cha maana

Unaposema hivyo, ukumbuke unasema na watendewa, watu wanaona, wanasikia na wanashiriki kuyafanya hayo unayoyaita hayafai

Mtu makini na mwanasiasa mwenye ushawishi hawezi kuwa hivyo! Ni lazima Kwanza akubali mambo yanayofanyika na ayasifie Kisha aoneshe udhaifu wa hayo na Kisha aseme namna nzuri ya kuyaboresha zaidi Kwa manufaa ya Watanzania

Hicho kitu wamekosa Sana hao wapinzani na ndicho temu hii kimewagharimu Sana aisee
 
Back
Top Bottom