Kwa nini huwezi kula ugali bila Mboga?

Kwa nini huwezi kula ugali bila Mboga?

Wanajukwaa habari zenu!
Hivi umewahi kujiuliza, Kwa nini Mboga ni za lazima au muhimu unapokula ugali?
Je, umewahi kula ugali bila mboga yoyote ile? Inawezekana? Haiwezekani?
Kuna makundi makuu ya virutubisho ya vyakula: (1)wanga (2) protein (3) madini Chumvi (4) fibers/roughage (5) vitamins.

Ugali wa Mahindi uko katika kundi la wanga wakati Kwa upande wa Mboga inaweza toka katika kundi la protein au vitamini (mbogamboga) na roughage (Mbogamboga).
Ugali ambao unatoka katika kundi la wanga siku zote lazima Mboga ziwepo. Kwa nini Mboga za aina yoyote ile lazima ziwepo?

Nimeuliza swali hilo Kwa kuwa Kuna vyakula vingine Vya wanga ambavyo vinaweza kuliwa bila mboga. Kwa mfano, Mihogo ya kuchemsha, wali, viazi utamu (sweet potatoes), viazi ulaya (Irish potatoes), magimbi, maboga, ndizi , n.k. Vyakula vyote hivyo Vya wanga unaweza kula bila mboga, isipokuwa ugali. Kwa nini?
Je, ni utamaduni?
Je, ni mitazamo yetu?
Je, wewe ulishawahi kula ugali bila mboga?, ilikuwa poa?
Kuna mwamba nilikutana naye shule, yeye hatumii maharagwe sasa hela za kununua mboga zikimuishia alikuwa anachukua ugali halafu anaukata mkubwa na mdogo anatenganisha.

Anaanza kula ule ugali huku mboga ikiwa ni ule ugali mdogo.
 
Kuna mwamba nilikutana naye shule, yeye hatumii maharagwe sasa hela za kununua mboga zikimuishia alikuwa anachukua ugali halafu anaukata mkubwa na mdogo anatenganisha.

Anaanza kula ule ugali huku mboga ikiwa ni ule ugali mdogo.
Yeah! Kama ambavyo wengine Hutumia uji kama mboga. Hizo ni shida ndizo zimepelekea hivyo. Lakini Kwa maisha ya kawaida, ugali bila mboga ni ngumu kidogo.
 
Ukila ugali bila mboga unakuwa hauna tofauti na msukule, unakula unga tu.
 
Kihalali kabisa, ugali siyo chakula cha binadamu, bali ni cha wanyama na ndege.
 
hata wali huwezi kula bila mboga
Wife huwa ananikatia embe ilio iva vizuri au nanasi lililo iva vizuri ,halaf anavimwagia juu ya wali, aisee huwa kwangu binafsi ni burudani sana.
Ukitoa wali maharage, bas hii ndio namna ya pil nayo enjoy kulia wali
 
kuna Jamaa namfahamu yeye hajaoa halafu ni mvivu kupika mboga, bas huwa anaenda anaagiza supu tu au anaenda kwa wakaanga samaki ananunua samaki halafu anamtafuna hukohuko.

Akirudi geto kwake anapika ugali anakula hivyo hivyo mboga ndo ilishatangulia anasema vitachanganyikia tumboni.
😆😅🤣
 
Back
Top Bottom