Kwa nini kuupinga Mkataba wa Bandari inaitwa "udini" lakini kuunga mkono sio udini?

Usipoteze nguvu na akili zako kumtetea mtu mweusi yule ni mtumwa na masikini watu weusi wote wanaopinga mkataba ni wanafiki kwani zikitangazwa nafasi za kazi dp world wataomba kazi sisi watu weusi nimesha gundua tunapenda utumwa na umasikini pamoja na kutawaliwa

Bandari ibinafsishwe kwa waarabu maisha yaendelee usimuonee huruma mtu mweusi acha ateseke
 
Hayawezi kuisha hadi mkataba wa bandari ufutwe au urekebishwe.

Kwenye waraka wa TEC kuna
kipengele kimezungumzia dini?
Wao tec ni watu wa dini tayari
Tanzania yetu haihitaji wadini wa aina yeyote kusukuma serikali kwa kuwa dini ya taifa ni katiba yetu ya jamhuri haiendeshwi kwa ukristo wala uislamu yeyote atakayepanda kwenye majukwaa ya siasa na afanye hivyo baada ya kustaafu uongozi wa dini la sivyo sheria na kanuni za jamhuri zisimamiwe ki sawa sawa dhidi ya wale wanaochezea tunu zetu suala la umoja na ustawi wa taifa sio la kucheka cheka na watu hata kidogo , leo wakianza tec kesho kutwa watakuja wale wa kujitoa mhanga tutajenga taifa gani sasa.
 
Kuunga mkono ukandamizaji siyo udini

Kuwatetea wanaokandamizwa ndo udini wenyewe🤣
 
Katiba ambayo ndio dini yetu leo inavunjwa hadharani.
Tusimame kuitetea bila kuangalia dini wala kabila au jinsia
 
Katiba ambayo ndio dini yetu leo inavunjwa hadharani.
Tusimame kuitetea bila kuangalia dini wala kabila au jinsia
Ikivunjwa mahakama ndio sehemu sahihi ya kutafsiri hayo ila sio kwenye majukwaa ya taasisi za kidini.
 
Hawa waliingiza tende na halua!!??
 
Na hapo ndipo mnapojifichia, wajingawajinga wanatekwa hapo. Ni lini ziliingiliwa mbinu za kiuchumi za huyo jiwe wako na wengineo?!!! Wanazunguka huko na kujifanya kuililia demokrasia ili kuwafumba macho msione mamia ya mikataba ya kinyonyaji ya madini kwa wazungu. Mkapa ametawanya rasilimali kibaaao za nchi na hadi anamaliza hakupewa waraka. Jiwe hivyo hivyo. Kwanini mbinu za kiuchumi zinaonekana kuingiliwa pale tu kiongozi anayedhaniwa kuwa muislamu akiingia madarakani?!!!

Uchumi ndo kila kitu, wakifanikiwa kukudhibiti katika uchumi basi uongozi wako umekwisha.......ndo wanalolifanya hilo na ndipo hapo hisia za kidini zinapoibuka, hakuna pengine!!!
 
Ikivunjwa mahakama ndio sehemu sahihi ya kutafsiri hayo ila sio kwenye majukwaa ya taasisi za kidini.
Haya, wewe nenda mahakamani sisi tutaongelea popote cha msingi tunaitetea katiba ifuatwe.
Katiba hiyo hiyo ndio inayowaongoza hadi maaskofu na masheikh.
Na kuongelea katiba ni kuzungumzia sheria mama za nchi, sio siasa.

Ndio maana kila mTZ anapaswa aisome na kuielewa katiba ya nchi yake. Imependekezwa humu mara nyingi katiba ifundishwe kuanzia darasa la tatu.
Kuijadili katiba sio siasa bali ni uzalendo
 
This is really pathetic!

Sheikh Mussa Juma amesema Wapinzani na Maaskofu wanaomsaka Rais Samia Suluhu Hassan hawana shukrani wanaendekeza Udini na maslahi yao binafsi nakusahau hisani waliyowafanyia kipindi walipokuwa hawana kitu.

Akizungumza huko visiwani Zanzibar katika mawaidha Sheikh Mussa Juma amesema Rais Samia ni kiongozi wenye huruma na uadilifu ndani yake hivyo wanaomsakama wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi.

"Hapa kwetu ndio kabisa madudu haya ya kisiasa sijui wakina Mbowe kina Lissu waliyoyaficha ndani ya mioyo yao yalikuwa ni makubwa zaidi kuliko wanayoyadhihirisha, angalia sasa hivi wanavyotapika maneno yale angalia ni udini tu ule, kama huyo Dkt. Slaa yeye ndio kamaliza mchezo mmemsikia mwenyewe Udini tu ule hakuna kitu kingine Udini tu..sasa yale ndio yaliyokuwa yamejificha hawana shukrani hata kidogo" alisema

Sheikh Mussa Juma amesema Rais Samia ni mtu mwenye imani wanaomuanda wanapaswa kumshukuru na kumheshimu kutokana nakuwafanyia hisani kwa kuwarejeshea vitu vyao walivyopoteza kipindi cha awamu ya Tano.

"Alikuwepo Magufuli kawanyongesha watu, kawaadhibu watu, kawatesa watu hawana hatia wamenyamaza kimya, Mwenyezi Mungu kafanya Rehema zake katuletea mtu ana imani watu wanaishi kwa raha , watu wanapendana, wanasaidiana, mnyonge anasaidiwa leo hawa wakina Mbowe, Lissu hawana Shukrani mtu kama huyo alowafanyia hisani kama huyu Lissu alipofanyiwa mambo mazito mtu wa kwanza kwenda kumtizama ni Rais Samia wale waliobakia wote maaskofu ambao sasa hivi ndio wanamtukana Samia kwa sababu ya uislamu hakuna kingine na maslahi yao waliyokuwa wanaipata kwenye ile bandari wanamsaka hawana shukrani wote hao maaskofu walikuwa wameufyata wanamuogopa Magufuli , lakini tazama alichomfanya Rais Samia kamlipa kila kitu chake kamrejeshea ambavyo alikuwa kanyang'anywa na huyo Mbowe hivyo hivyo kila kitu chake karejeshewa kalipwa pesa chungu mzima ambazo zingewasaidia wananchi , Rais Samia anaonyesha huruma kwa rai wake alafu hawa wanakuja juu wanamtukana na kumkashifu kwa maslahi yetu wenyewe sisi wananchi lakini kwa sababu wao kuna maslahi yao ya dini pale wanahisi atakuja kuondoka , pamoja na maslahi yao walikuwa wanapitisha vitu pale...." alisema Sheikh huyo

Pamoja na yote Sheikh Mussa dunia ilipofikia sasa mambo mema yanaonekana mabaya huku mabaya yakionekana mema hata hivyo amemuomba Rais Samia aendelee kuishi maisha marefu kutokana na uadilifu na huruma alionao katika uongozi wake.

"Mbona mambo sasa hivi yanaanza kuchimbuka yaliyokuwa yamejificha na sisi ndio tunayasubiri kwa hamu kwa sababu tulipokuwa tunasema nyinyi mlituona sisi wabaya lakini sasa hivi Mwenyezi Mungu anayachimbua, mmemsikia Slaa alivyosema nyie waislamu mmekaa tu mmemsikia na uislamu wenu mnasikia wanavyomfanyia muislamu mwenzenu wanavyomwandama, wanaranda kwenye mikoa kwa kutumia pesa hizi hizi wanazopewa zetu wenyewe kama rai wanamsakama Mhe. Rais Samia lakini Mwenyezi Mungu atamuhifadhi, atamlinda na shari zao ataendeleza uadilifu, ni Rais pekee aliyekuwa hana mfano na waliyokuwa wamepita mwenye huruma mpaka na vilema tunamuombea dua na tutazidi kumuombea sasa kama wewe unanuna nuna"_ Sheikh Mussa Juma akizungumza msikitini Zanzibar
 
Umeona tofauti apo
 
Hapo mkuu hata kama utachukulia kanisa kuwa nyuma ya katika huo upingaji wao wa huo mkataba wa bandari ni kwa masilahi yao binafsi ila hiyo ni kwa sababu wameona upenyo, kwa maana waliyokosoa huo mkataba ni watu aina tofauti tofauti na makundi mbalimbali hivyo nao wamepitia humo humo na si kwamba Kanisa tu pekee ndio limeupinga huo mkataba. Hivyo muhimu kuangalia hoja tu na jambo kubwa ni watu kutaka baadhi ya vifungu virekebishwe ndio hoja yenye nguvu kuliko hao wasioutaka kabisa huo uwekezaji.

Hata hao masheikh wanaotetea huu uwekezaji na waarabu nao nyuma yao utakuta pengine kuna masilahi binafsi yasio ya kitaifa, ndio maana nasema muhimu kuangalia uzito wa hoja tu.
 
Tuwekee siasa aside,ila nchi yangu imezidi unafki ambao hata hawayani kama mbwa na mbuzi wanatushangaa.
Ni hivi karibuni nimeanza kusikia mfulilizo wa matangazo ya bandari redioni.
I can't recall tangu nazaliwa kama nlishawahi sikia matangazo ya bandari yetu hii isipokuwa siku mbili tatu hizi.Mara oooh bandari yetu fahari yetu mara lango la Africa mashariki.

Sijawahi ona ufanisi kama huu katika kuitangaza bandari yetu redion utadhani ni kampuni ya vodacoma (like we don't know the harbour exist.)

Wakuu hivi waarabu washaanza kazi?
 
Kukemea ufisadi wa CCM ni udini!!!!!!!! Ukisifia ufisadi wa CCM siyo udini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Amkeni watanganyika!!! Amkeniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,wezi haooooooooooooooooooooooooooooo, shetani amevaaaaaa bukta ameingia msambweni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Misamaha ya kodi kwa Taasisi na watu mbalimbali umeainishwa katika sheria ya kodi sio hisani. Swala la dili lipo tu kila mahali inategemea na uadilifu wa wahusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…