Kwa nini kuupinga Mkataba wa Bandari inaitwa "udini" lakini kuunga mkono sio udini?

Kwa nini kuupinga Mkataba wa Bandari inaitwa "udini" lakini kuunga mkono sio udini?

Hizo ada zinawahusu wasio wakatoliki tu au ni kwa wagonjwa wote? Kama ada ziko juu kwa uende huko?

Kuhusu kupitisha mizigo kwani wenye mamlaka bandarini ni wakatoliki pekee. Usividhalilishe vyombo vyombo vinavyoendesha na kudhibiti shughuli za bandari

Hiviii huuu mkataba una dini gani mpaka watu wanakesha wanaimba watu wasiuguse? Maana ukiugusa unagusa dini. Kuna vipengele gani katika mkataba huu vyenye udini ndani yake ili visigushwe? Kumbe kwa mkataba huu uwekezaji umegeuzwa kuwa ni siasa, waachiwe wanasiasa pekee ndiyo waujadili? Jamani tunaelekea wapi mbona watu wanatulazimisha tusiongelee vipengele vyenye utata tunambiwa faida tu, hasara je mbona hatuambiw
Tuache kuchanganya dini na siasa
 
Kwa Rais Mstaafu @jmkikwete na mnaosema Baraza La Maaskofu wana chuki za kidini. Naombeni mnieleweshe:

[emoji3578]Baraza hili la maakofu (TEC) mwaka 2018 lilipotoa waraka wa Pasaka wa kupinga mauaji na utekaji wa watu uliofanywa na Serikali ya Jiwe walikua na vhuki ya Kidini na 'Mkatoliki' Mwenzao Magufuli?

[emoji3578]Mmesahau Askofu Severine Niwemuguzi alinyang’anywa Passport na kuambiwa sio raia kwa sababu ya kupinga uonevu wa
Jiwe, alikua na chuki na Mkatoliki mwenzake?

[emoji3578]Wakati wa COVID Baraza La Maaskofu lilipotoa waraka wa kumpinga Magufuli kuwa COVID haipo na kutaka serikali iruhusu watu wapewe chanjo, walikua na chuki za kidini na Magufuli Mkristo mwenzao?

[emoji3578]Walivyo kemea madudu ya uchaguzi wa 2020 walikuwa na chuki za kidini na Magufuli Mkristo mwenzao?

[emoji3578]Kama kila wakati kukiwa na mjadala wa kitaifa wanatoa Waraka, na hamkuwai kuona shida, kwanini mnataka sasa wasitoe?

[emoji3578]Kwahiyo wakitoa kwa Mkristo mwenzao sio chuki? Wakitoa sasa kwa Muislam ndio wana chuki?
Hapa umeweka kisu kwenye mfupa. Kwa bahati mbaya wanadhani bado tuna ujinga huo wa kupotezwa maboya kwa hizo dini zilizoletwa na majahazi.
 
Ndio haya mambo yaishe sasa viongozi wa dini wabakie kwenye field zao ni hatari wao kuingia kwenye siasa na nyakati zinaonyesha hivyo kwa sasa tunahitaji serikali imara leo kesho na keshokutwa sisi na viongozi wa dini na waumini na waamini yetu ni kwenye sanduku la kura na kutoa maoni yetu tu ila sio kuiendesha serikali kwa rimoti na kupush agenda zenye maslahi na taasisi zetu.
Yenu kwenye sanduku lipi la kura? Ama unadhani huwa hatuoni ule uhayawani unaofanyika kwenye box la kura? Serikali ya majizi ya kura hai a uhalali wowote wa kufikiwa kutokukatazwa kuuza rasilimali za nchi.
 
Wananafasi ya kutoa ushauri ila hawanafasi ya kuweka political presha kupitia majukwaa yao ya taasisi zao kwa kuwa wakifanya hivyo wanahatarisha umoja kwa kuwa dini zipo nyingi italeta mtafaruku heri ya Zambia wanadini ya taifa ila hapa kwetu hatuna .
Na pia jamani kama wao wanatufundisha uvumilivu basi na wao waanze kuyatenda wale wanayotufundisha ukitoa ushauri usiposikilizwa kuwa mvumilivu na sio kuleta ukaidi kwa kuwa unameans za kufanya hivyo.
Serikali iliyoko madarakani kwa wizi wa kura ni lazima ipewe pressure, sisi hatuangalii wingi wa dini, tunaangalia hoja za ukweli bila kujali dini ziko ngapi . Watu wametoa maoni yao, kisha wanaona hayafanyiwi kazi, bali sheria zinataka kubadilishwa ili kuendana na huo mkataba wa kihuni. Huo ukimya wa taasisi za dini ndio umechangia serikali kuingia mikataba isiyo na tija kwenye mali nyingine za umma.

Tunawapongeza TEC kwa kujitokeza hadharani na kupinga mkataba wa utata kwa mali za umma. Watu wanajificha kwenye kichaka cha dini, wakati wako madarakani kwa mauji, wizi wa kura na uhayawani wa wazi kisha wajifanye habari za dini uchwara!
 
KWA NINI KUUPINGA MKATABA WA BANDARI INAITWA "UDINI" LAKINI KUUNGA MKONO SIO UDINI? MSIWE WAPUMBAVU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Wanasiasa moja ya mambo yanayowashushia heshima ni kigeugeu na unafiki wao. Wanasiasa wakisifiwa na viongozi wa dini hawasemi dini imeingizwa kwenye Siasa lakini wakikosolewe hapo utasikia Dini imeingizwa kwenye Siasa.

Wanasiasa wakitaka kuombewa na viongozi wa dini hiyo hawaiti dini imeingizwa kwenye Siasa. Wao wanataka tuu Sifa na utukufu Kutoka Kwa dini lakini wakikosolewa na kupondwa hapo wanaleta shida.

Tabia hiyo ya hovyo na kinafiki imekomaa Sana katika Nchi yetu. Na sasa tupo kwenye sakata la mkataba WA Bandari.

Viongozi wa dini waliosifia mkataba huu wao hawaambiwi kuwa ni UDINI. Lakini wanaoukosoa wanaambiwa ni udini. Hivi tutaacha lini huo upumbavu.

Kwa nini tusiangalie hoja ya msingi. Huo mkataba kama ni mbovu Kwa nini usibadilishwe? Kama kweli nia ni yakweli ya kutetea maslahi ya nchi. Kwa nini huo mkataba usiboreshwe vifungu vyenye utata?

Kujitetea kwa kujificha kwenye kichaka cha udini hakutabadili Jambo lolote.

Hekima na busara zitumike, kama kweli lengo ni kulinda maslahi ya Taifa letu na maslahi ya Watu wetu na rasilimali zetu. Mtu akipinga Jambo kama anahoja ya msingi lazima asikilizwe.

Kwanza hizo dini zenyewe tumeletewa. Pili, tupo watanzania wengi ambao hatuamini Kati hizo dini zenu za kigeni. Ingawaje tunawatambua na kuheshimu wanaoziamini. Sasa msitake kuzifanya hizo dini zenu zinaumuhimu kuliko taifa letu.

Mnapojadiliana ishu za taifa msijifanye mnajificha kwenye udini. Oooh! Yule Mkristo ndio maana anakosoa. Lakini akisifia huwezi sikia Jambo Hilo. Angalieni kinachokosolewa, je kina uhalali wa kukosolewa? Kama jibu ni ndio,basi fanyieni maboresho.

Uwe Mkristo au muislam, uwe wakabila gani, uwe Mtibeli kama Mimi au mpagani. Kwetu haina maana yoyote Ile. Tunachotaka ni kulinda maslahi ya nchi yetu na sio genge Fulani la Watu. Ni lazima tuangalie kizazi chetu kilichopo na kinachokuja.

Dini yako, au Cheo chako au mamlaka yako haina maana yoyote kwetu ikiwa unataka kuliingiza taifa katika hasara na ubinafsi wa hovyo.

Acheni upumbavu! Mtu akitoa hoja isikilizwe hoja yake na sio ni wadini gani. Kama mkataba haufai, urekebishwe. Hiyo ndio hoja. Mambo ya sijui Amani, sijui mgawanyiko, hayo yote yataletwa na watu wabinafsi na wasiotaka kusikiliza wengine.

Mgawanyiko ni muhimu ikiwa tunatofautiana. Hiyo iwekwe wazi. Kama Watu hawataki wawe wamoja, kujaribu kuwaunganisha Watu wasiofanana ndio ukosefu wa Amani, mitafaruku, unyanyasaji na ukatili. Hatuwezi lazimisha umoja wa kinyonyaji, umoja wa wengine wanafaidi wengine wanasota, huo umoja haupogo labda kinafiki.

Nisikilizeni, umoja unaletwa Kwa kuangalia wengi wanasema nini, lakini pia Kwa kuzingatia maslahi ya taifa na kizazi kijacho.

Upendo, Haki, Ukweli na Akili hiyo ndio namna ya kuwaweka Watu pamoja. Utibeli.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
katika hili tuko pamoja sana ndugu Robert.
umetoa hoja zako kikomavu na kisomi.
safi sana kwa kazi nzuri.
bandari zetu zitabaki iwe kwa heri au kwa shari
 
Waislamu tunategemea mwarabu akichukua bandari tutapata dili za kazi kama ilivyo kwa bakhresa au kwa dewji. Kampuni zote za kiislamu huwezi kuta mgalatia ovyo ovyo ovyo, na hilo nenda hata uarabuni iko hivyo hivyo.
 
Huyo mwanasiasa mwenyewe anapinga siasa kuchanganywa na dini huku akiwa kwenye mimbari ya kanisa ama shuguli za kidini.

Ni upumbavu sana Hapo ndipo unapoona wale wajinga wanaosema dini isichanganywe na siasa hawana akili, huwezi kuacha kuchanganya dini na siasa kama vyote viwili vinahusisha watu wale wale.

Hiyo ni propaganda ya kitoto inayotumiwa na wajinga, ili kuzuia maswali magumu wanayoshindwa kuyajibu pale wanapoulizwa kuhusu ule mkataba wa hovyo wa bandari, propaganda ambayo tayari imefeli

C & P
 
Waislamu tunategemea mwarabu akichukua bandari tutapata dili za kazi kama ilivyo kwa bakhresa au kwa dewji. Kampuni zote za kiislamu huwezi kuta mgalatia ovyo ovyo ovyo, na hilo nenda hata uarabuni iko hivyo hivyo.
mmekua misukule tu, unakubari kulipwa elfu sabini kwa mwezi sababu bosi wako ni mwarabu?
stupid kabisa
 
Askofu Gwajima alishiriki vikao viwili kupitisha Mkataba wa Bandari - Bunge na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. Pia, ameshiriki mikutano ya hadhara na kampeni kadhaa za CCM kuunga mkono mkataba. Wakati anashiriki vikao hivyo, hawakuona kuwa anachanganya dini na siasa.

Lakini sisi tunapotoa hoja na matamko kupinga na kutahadharisha juu ya mkataba wa bandari, lakini vigogo wa CCM wanakuja juu na kuanza kutupiga madongo majukwaani kutuonya kuwa tunachanganya dini na siasa.

Hakuna utawala uliowahi kudumu duniani hasa kama viongozi wameanza kuwa wanafiki kwa kuwa wanafiki huukataa na kuuchukia ushauri hata ule ambao una lengo la kuuokoa utawala huo usianguke.

Waache waendelee kutumia majukwaa kupiga madongo maaskofu wanaoonya, wanaoshauri na kukemea kwani CCM walio wengi hawajui kuwa meli yao imeanza kutoboka. Wanadharau boti za wokozi zinazopita kandokando ya meli yao kubwa ya kifahali iliyoanza kutoboka. Muda wa kuzama ukitimu watapiga kelele ili kutafuta msaada wasiweze kupata watu wa kuwaokoa.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 21 Agosti 2023; 02:38 Asubuhi
 
Serikali iliyoko madarakani kwa wizi wa kura ni lazima ipewe pressure, sisi hatuangalii wingi wa dini, tunaangalia hoja za ukweli bila kujali dini ziko ngapi . Watu wametoa maoni yao, kisha wanaona hayafanyiwi kazi, bali sheria zinataka kubadilishwa ili kuendana na huo mkataba wa kihuni. Huo ukimya wa taasisi za dini ndio umechangia serikali kuingia mikataba isiyo na tija kwenye mali nyingine za umma.

Tunawapongeza TEC kwa kujitokeza hadharani na kupinga mkataba wa utata kwa mali za umma. Watu wanajificha kwenye kichaka cha dini, wakati wako madarakani kwa mauji, wizi wa kura na uhayawani wa wazi kisha wajifanye habari za dini uchwara!
Udini tu unawasumbua hii nchi haina dini hili taifa letu wote ni kitu kimoja kama wanasiasa wameridhiana wamereconcile basi tusubirie uchaguzi ujao watapata tume huru kwa kuwa Tanzania ni yetu sote haijalishi uwe mpinzani au nani na pia hekima ya kushauri ni kukubali pia ushauri wako ukikataliwa kwa kuwa unayemshauri anahiari ya kukubali au kukataa au atachagua mwenyewe lini atekeleze ila sio kumuwekea presha za kisiasa na kidini hapo ndio ukosefu wa hekima unaingia mwisho kabisa ndugu yangu rafiki yangu hii nchi imetoka kuwa tegemezi kwa asilimia kubwa sana toka huko kwenye bajeti ya kutegemea donor kwa kiwango kikubwa hadi sasa ambapo bajeti inautegemezi wa chini ya 30% hii yote ni kutokana na kazi nzuri ya uwekezaji na ubinfasishaji uliochangia pato la taifa kuongezeka kuanzia kwa Mwinyi, Mkapa ,JK , Magufuli na sasa Samia tena huyu ataweka historia ya kufuta utegemezi kabisa,sasa kwa nini mradi kama huu wa bandari uwekezaji huu utatutoa kabisa ktk utegemezi na kuwa na bajeti ambayo tutajisupport wenyewe 100% why not , hapo ndio emotions tupa kule maslahi ya uhuru wa kiuchumi kwanza, waswahili wanasema baniani mbaya kiatu chake dawa.
 
Waislamu tunategemea mwarabu akichukua bandari tutapata dili za kazi kama ilivyo kwa bakhresa au kwa dewji. Kampuni zote za kiislamu huwezi kuta mgalatia ovyo ovyo ovyo, na hilo nenda hata uarabuni iko hivyo hivyo.

Duuh!

Mimi mbona nafanya biashara na hao Waarabu
 
Wanasiasa wenyewe ni kina nape na mwigulu. Mwigulu anakwendaga kanisan kuchangia harambee huko kwa wakwe zake na kutengeneza jina ili aje agombee uraisi,Hilo haoni ni udini, Ila limekuja Jambo lao la bandari, yeye, Nape and et al wanalia udini🤔
Elimu za kuungaunga
 
Back
Top Bottom