Kwa nini kuupinga Mkataba wa Bandari inaitwa "udini" lakini kuunga mkono sio udini?

Tatizo elimu ndogo na inferiority complex
 
Wewe unasema tutapata wakati mkataba unasema hatupati, tutapataje na kutoka wapi. Umeusoma au unakariri yanayosemwa kwenye majukwaa?
 
Walio wengi husahau ya jana., na walio wengi niwavivu wa kusoma., watu hawa ni rahis sana kuwapotosha. Maana huamini kutoka kwa mtu aliyesoma nakuwasimlia wasiopenda kusoma, nao huyachukua kama yalivyo nakuanza kutembea nayo., daima akili yakuambiwa CHANGANYA NAZAKWAKO.
 
ccm ndio wapumbafu wanaangalia jana na sio kesho
 
Wewe unasema tutapata wakati mkataba unasema hatupati, tutapataje na kutoka wapi. Umeusoma au unakariri yanayosemwa kwenye majukwaa?
Kwa hio wewe ndio una akili nyingi kuwazidi watu wote wale yaani wao hawana uchungu kabisa hembu tuwape watu utulivu wafanyie kazi maoni yenu kadiri watakavyoona inafaa na kulifanyia kazi njema taifa letu na pia feedback si mtaiona kazi zikianza na wao pia ni watanzania na wanandugu watoto jamaa ,wajukuu pia na kizazi kitakachoendelea kuishi ktk taifa hili.
 
Hujalazimishwa kuchangia, michango ya kanisa sio kama kodi za serikali.
 
S
Sawa lakini si kwa masharti haya.
 
Usisahau kwamba imeanza kuitwa ni kosa la uhaini, kisha uchochezi na sasa udini, itaenda ukabila, ukanda na itikadi
 
S

Sawa lakini si kwa masharti haya.
Yasitutishe hakuna kisichozungumzika ktk ulimwengu huu tuwape nafasi bila kufanya hivyo tunapoteza muda wa kusonga mbele mwishowe tunakosa vyote sasa inakuwa hakuna hata lengo la kupiga makelele , maana hata mbwa unampigia kelele yenye malengo mfano kamata yule anakamata ila sasa ikiwa zogo huku na kule anashindwa ashike wapi, basi yanakuwa makelele tu yasiyokuwa na maana mwishowe kutupeleka kubaya .
 
Kikwete aliitwa na Cardinal Pengo "Chaguo la Mungu", akachekelea Wala hakumwambia Pengo anachanganya dini na siasa, lakini Waraka wa TEC umemtoa Mheshimiwa pangoni na kuwaambia TEC wanachanganya dini na siasa, hata hivyo, dini na siasa unazitenga vipi?
 
Umeongea point sana, Baraza la Maaskofu miaka yote hukemea maovu bila kujali anayeongoza ni nani, kazi ya viongozi wa dini ni kukemea maovu. Kwa Wakristo, Yohana mbatizaji alimkemea mtawala Herode kwa uovu wa kumuoa mke wa ndugu yake akakatwa kichwa, Yesu alikemea maovu hadharani mpaka akasulubiwa. Kwa Waislamu, Mtume Muhammad alipigana vita vingi vya Badr, Uhud, Khandak na Hunayn, je alichanganya dini na siasa? Viongozi wa dini wakemee uovu hadharani bila kujali nani anaongoza.
 
Dini unazitenga vipi na siasa? Dini inahudumia watu, siasa inahudumia watu.
 
Kitu cya ajabu ni kwamba, waliolichukua jambo hili kulitoa kwenye majukwaa ya siasa na kulipeleka madhabahuni na kulifanya kuwa ni sehemu ya ibada yao na kulifanya kuwa ni kampeni ktk dini yao hadi kwenye ngazi ya familia, hao hao wenyewe ambao kutwa nzkma kwenye dini yao walifanya kuwa ndio gumzo wenyewe ndio wapo mbele kila siku kusema tusilifanye hili jambo kidini wakati huo wanazidi kuchapisha nakala kwa waumini wao na kuendelea na kampeni yao. Waliokaa kimnya, ndik sasa wamekuwa wabaya na wanasemwa kuwa wao ndio wadini.
 
Wale waliopigiana simu na kumwita Magufuli mshamba ile haikuwa udini?Watu hao hao unakuja kuwapa tena vyeo
 

Sifa ni tamu Mkuu
 
Jibu rahisi sana sio udini sababu unaunga mkono jambo la serikali, serikali ambayo Haina dini.

Kingine watu hawakatazwi kukosoa tatizo unakosoa kwa misingi gani ? Kwanini hufati utaratibu ? Kama kweli viongozi walipeleka mashauri yao kwa raisi, hao Wakatoliki (Vilaza) walitakiwa wasubiri na hivi ndio dini inataka. Kiherehere Chao Cha kusoma Waraka lengo lao ni nini ? Kuleta taharuki na wao kama nani kwenye nchi hii ?

Kingine kwanini walichanganya dini na siasa ? Yaani kwao wao wametumia dini kufanya siasa na harakati, hawana tofauti na Wanasiasa na Wanaharakati wengine.
 
Hata wewe ni chagua la Mungu kwa kulifanya uishi.

Pili, kuitwa na kuambiwa jambo kwa siri kama kiongozi hii ndio namna nzuri na dini ndio inavyo taka. Ila kujitokeza na kutumia vifingu vya katika katika kivuli Cha siasa huku ni kuchanganya dini na siasa.

Kingine, kuandika uongo na kuwasemea wengine kwamba wanapinga mkataba, huu ni uzandiki na kuleta udini.
 
Lkn pia mwanzishi wa hiyo dhana ya udini na uzanzibar anafahamika, tuanzie hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…