Boss! Nakufahamu miaka mingi hapa JF. Ulikuwa mtu wa hoja. Leo hii ni wewe unayeishia kutetea Ushoga wa Us na mifano ya kupendwa kwenye komedi za US? Ni wewe au mjukuu wako kishajua kushika keyboard.
Kama ni wewe basi nikubali tu kwamba senility imekufuata mapema.
Kwanza kabisa mimi sihitaji validation yako, sihitaji popularity. Ningekuwa nahitaji validation ya mtu nisingeandika hoja nyingi ambazo watu hawazipendi.
Naomba tujadili hoja, usinijadili mimi kama mtu binafsi. Ukinijadili mimi kama mtu binafsi hiyo ni logical fallacy, inaitwa ad hominem attack.
Ni ishara ya kushindwa kujadili hoja.
Ushoga ni sehemu ya haki za binadamu za watu kujiamulia maisha yao wenyewe. Serikali yako ya Tanzania yenyewe imekubali kuwa pole Makonda alivyoshambulia haki za mashoga, tena wakati wa utawala wa Magufuli.
Makonda alikurupuka kuwaandama mashoga, mtu anayeijua dunia, Waziri wa Mambo ya Nje Dr. Augustine Mahiga akamkana, akasema hayo yalikuwa maneno yake binafsi, si msimamo wa serikali.
Magufuli mwamba wa kupambana na mabeberu akakubali kwamba ile ilikuwa kauli binafsi ya Makonda.
Hapo Tanzania watu wengi hamjui maana ya uhuru wa mtu binafsi, kitu ambacho ni uhuru wa kikatiba.
Halafu mnadai katiba mpya.
Yani uhuru wa katiba hii mliyo nayo mnauvunja, halafu mnataka katiba mpya yenye uhuru zaidi.
Wengi hamuelewi uhuru ni nini. Wengi hamuelewi haki za kikatiba ni nini.
Hamuelewi haki za kuruhusu ushoga ndiyo haki zilezile za kuruhusu vyama vya upinzani. Minority rights.
Hamuelewi kuwa jinsi wewe mtu usiye shoga ulivyo na haki ya kutopangiwa kuwa shoga ndivyo shoga ana haki ya kutopangiwa kutokuwa shoga.
Yani ni hivi, ukimuandama shoga kwa ushoga unaruhusu siku mashoga wakiwa wengi wakulazimishe wewe usiyependa kuwa shoga uwe shoga.
Utafurahia kuishi katika dunia ya mashoga wanaokulazimisha uwe shoga wakati wewe hutaki kuwa shoga?