Kwa nini Rais Samia hajaenda New York kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa?

Kwa nini Rais Samia hajaenda New York kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa?

Izia maji

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
2,997
Reaction score
5,385
Tangu aapishwe Rais Samia amekuwa akihudhuria kila mualiko anaoupata kutoka nchi za nje na Jumuiya za Kimataifa. Lakini ajabu safari hii amemtuma Kassim Majaliwa kumuwakilisha na badala yake yuko Songea kuhudhuria tamasha la utamaduni!

Je ameogopa maandamano ya yule dada Mange ambaye alikuwa anamsubiri kwa hamu ampe makavu live?

Je ameogopa maswali magumu kutoka kwa waandishi nguli wa kimataifa wa habari kuhusu kuminya demokrasia nchini?

Je ameogopa viongozi wenzake wa kimataifa kuanza kumtilia shaka kuhusu uwezo wake wa kuongoza nchi?
 
Siyo kweli, mama Rais Samia mialiko anayohudhuria nchi za nje ni kidogo sana kuliko asiyohudhuria.
. Akisema ahudhurie mialiko yote hatutamwona Tanzania.

Nani alikudanganya?
 
Toka aingie madarakani vimefanyika vikao vingapi na amehudhuria vingapi?
Anzia hapo kama una D2
Vimefanyika vikao vitatu na amehudhuria vyote na hiki kingekuwa kikao cha nne kama angehudhuria.
 
Hajahudhuria ili mjuwe kwamba hii siyo serikali ya samaki.
 
Tangu aapishwe Rais Samia amekuwa akihudhuria kila mualiko anaoupata kutoka nchi za nje na Jumuiya za Kimataifa. Lakini ajabu safari hii amemtuma Kassim Majaliwa kumuwakilisha na badala yake yuko Songea kuhudhuria tamasha ...
Kwa sababu ana ziara ya Mkoa wa Ruvuma.

Mwaka wa uchaguzi ni muhimu kuliko Huko News York Kwa Mabeberu.

Mwisho awamu zote za Magu,PM ndio alienda na Sasa ameenda pia kuwakilisha Samia na Nchi.
 
Siyo kweli, mama Rais Samia mialiko anayohudhuria nchi za nje ni kidogo sana kuliko asiyohudhuria.
. Akisema ahudhurie mialiko yote hatutamwona Tanzania.

Nani alikudanganya?
Itakuwa wanakumbukia Baba Rais
 
Tangu aapishwe Rais Samia amekuwa akihudhuria kila mualiko anaoupata kutoka nchi za nje na Jumuiya za Kimataifa. Lakini ajabu safari hii amemtuma Kassim ...
Samia ana poteza interest na siasa za kimataifa na kujikita zaidi kwenye siasa za ndani. Hususan kwenye kipindi hiki anapojiandaa na uchaguzi na kuona anapata upinzani mkubwa nchini.

Amejiona hana ushawishi kwenye siasa za kimataifa, kwa sababu kujenga ushawishi kunataka akili kubwa. Hawezi kuongelea na kuongoza hoja kubwa za kimataifa kama Nyerere alivyoongelea uhuru wa Africa, au nchi za kusini kuungana dhidi ya udhalimu wa kibeberu wa power structure ya dunia.

Samia alipewa nafasi ya kipekee kuongoza mazungumzo ya climate justice kwenye kikao cha Sharm el-Sheikh, Egyot, Climate Change Conference (COP 27). Sio tu Samia alishindwa kusimamia hoja hii muhinu kimataifa, hata aliporudi Tanzania, alishindwa kuwaelezea Watanzania kwamba alichaguliwa kuongoza mazungumzo haya muhinu. Matokeo yake, wenzetu wa Zambia walichukua fursa hii kupata dola za kinarekani mabilioni, karibu dola bilioni kumi, huku Tanzania ikiondoa bila deal la muhimu licha ya rais wetu kuongoza mazungumzo hayo.

Hata Samia alivyorudi Tanzania, Mkurugenzi wa habari wa Ikulu wa wakati huo, Zahra Yunus, katika press conference yake ya kuelezea mkutano huo, alifanya kile waandiahi wa habari wanachoita "burying the lead" kwa kuweka kimstari kimoja kidogo ndaaani kabisa ya press conference kuelezea Samia alivyoongoza, kinyoonge, kama walikuwa wanaficha kitu vile.

Samia hana agenda ya kimataifa. Sasa hivi anahaha kupigana na kina Mbowe na CHADEMA, anajipendekeza kwa machifu ambao hawana hata legal mandate Tanzania.

Anazua vita zisizo na sababu na mabalozi wa nje walio Tanzania. Ukimsikiliza unaona kabisa huyu ni rais ambaye shule yake iko chini sana na uwezo wake ni mdogo sana, na hajui anafanya nini, anataka kushika madaraka kwa nguvu halafu hajui hayo nadaraka ayafanyie nini zaidi ya kupiga hela na kujikimbikizia mali, na kutukana watu kwa siasa za majitaka na hotuba za mipasho tu.

Akienda UN atasema nini? Kajikuta like vibe la UN ni la hotuba za kifalsafa na geopolitics, yeye anapenda vibe la kusifiwa na chawa wake ambao huko UN hawapo.

Sasa aende UN kufanya nini wakati chawa wake wapo TZ?

Alisema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Na alianza kama yuko tofauti na Magufuki, lakini sasa kafuata nyayo mbaya za Magufuli mpaka kukacha vikao vya UN.
 
Tangu aapishwe Rais Samia amekuwa akihudhuria kila mualiko anaoupata kutoka nchi za nje na Jumuiya za Kimataifa. Lakini ajabu safari hii amemtuma Kassim Majaliwa kumuwakilisha na badala yake yuko Songea kuhudhuria tamasha ...
Amewakilishwa na PM, kuna mwaka pia aliwakilishwa na VP
 
Tangu aapishwe Rais Samia amekuwa akihudhuria kila mualiko anaoupata kutoka nchi za nje na Jumuiya za Kimataifa. Lakini ajabu safari hii amemtuma Kassim Majaliwa kumuwakilisha na badala yake yuko Songea kuhudhuria tamasha la utamaduni!

Je ameogopa maandamano ya yule dada Mange ambaye alikuwa anamsubiri kwa hamu ampe makavu live?

Je ameogopa maswali magumu kutoka kwa waandishi nguli wa kimataifa wa habari kuhusu kuminya demokrasia nchini?

Je ameogopa viongozi wenzake wa kimataifa kuanza kumtilia shaka kuhusu uwezo wake wa kuongoza nchi?
hawezi kwenda kwa sababu hiyo
 
Samia ana poteza interest na siasa za kimataifa na kujikita zaidi kwenye siasa za ndani. Hususan kwenye kipindi hiki anapojiandaa na uchaguzi na kuona anapata upinzani mkubwa nchini...
Zambia alipata dola bilioni ngapi?

Naomba link mkuu nijifunze hili

And from what ki know, Bado ssh Ana kijiti cha cop na mwakani ana jambo kubwa Africa hapa bongo
 
Tangu aapishwe Rais Samia amekuwa akihudhuria kila mualiko anaoupata kutoka nchi za nje na Jumuiya za Kimataifa. Lakini ajabu safari hii amemtuma Kassim Majaliwa kumuwakilisha na badala yake yuko Songea kuhudhuria tamasha la utamaduni!

Je ameogopa maandamano ya yule dada Mange ambaye alikuwa anamsubiri kwa hamu ampe makavu live?

Je ameogopa maswali magumu kutoka kwa waandishi nguli wa kimataifa wa habari kuhusu kuminya demokrasia nchini?

Je ameogopa viongozi wenzake wa kimataifa kuanza kumtilia shaka kuhusu uwezo wake wa kuongoza nchi?
Hata kama alikuwa na udhuru basi Makamu wa Rais Dr Isdory Philip Mpango alipaswa kwenda kumuwakilisha, lakini badala yake ameenda Waziri Mkuu. Naona kuna jambo haliko sawa.
 
Kwa sasa hawezi kuhudhuria vikao vya watu wenye akili zao huko Duniani. Aliwaahidi kwamba yupo tayari hata kupoteza Urais wake ilimradi tu Demokrasia iweze kutamalaki Nchini lakini kwa sasa mambo ni kinyume kabisa na alivyowaahidi zile siku za mwanzo.
Kama anathubutu hata kuwakemea Mabalozi, Viongozi wa Dini, wazee maarufu nk. hapo unategemea nini?

Ameshalikoroga na hawezi tena kwenda huko Duniani, labda awaombe radhi.
 
Akisafir nongwa , asiposafiri nongwa pia...hiki cheo kinahitaji mtu mwenye roho ngumu aisee lelemama lazima isande🤣 huyu mama mpaka namuonea huruma aiseee
 
Siyo kweli, mama Rais Samia mialiko anayohudhuria nchi za nje ni kidogo sana kuliko asiyohudhuria.
. Akisema ahudhurie mialiko yote hatutamwona Tanzania.

Nani alikudanganya?
Sema ukweli tu bibi yangu kwamba mambo si mambo
 
Back
Top Bottom