Kwa Nini Tunamkubali au Kumkataa Mtu Bila Sababu?

Pole sana mkuu kiumbe mbaya zaidi ni binadamu
 
Kumbee mkuu hii mada sikuwaza kama ni pana kiasi hiki
Nimejifunza vingi asante kwa maoni🙏🙏
 
....
 
Nakusalimu mkuu,

Kuhusu maada zako fikirishi Kuna siku nitasema la moyoni.

Niende Moja Kwa moja kujibu swali.

Kutokumkubali mtu binafsi huwa sio chuki ila naamini huwa Kuna msukumo kutoka ndani ambao husababisha hiyo hali.

Mimi binafsi huwa napenda kuwa positive(Positivity), Yaani katika jambo lolote nitaanza kwanza kulichukulia upande wa faida zake na baadae huangalia hasara zake. Hivyo mara nyingi huwa nachukia mtu mwenye negativity. Kwangu mimi hiki ndio Huwa chanzo cha kutokumkubali mtu katika mazingira fulani.

Nikiwa form one kuna jamaa nayeye alikua form one ila alichelewa kufika shule, Hivyo siku ya kwanza tuu amefika shuleni tukacollide nikiwa natoka kula.

Yaani nipo nje ya DH nimeosha poti langu nikanywa maji nikasukutua mdomoni na kuyatema pembeni mbali kabisa nayeye anapokula (alikua ndio amefika kwahiyo walimpea chakula nje). Jamaa yake akaniita nilipoenda pale eti akakwazika vile niliyatema maji akanikasirikia qkanitolea maneno ya shombo, Aisee!😂😡.

Nilimuangalia alikua amevaa Kaunda suti ya kijani (zile wanavaaga makondakta) alafu ametokea kijijini mbali sana huko. Sikumjibu kitu ila sijawahi kumkubali hadi kesho. Darasa zima walikua wanajua mimi huwa naongea na watu wooote ila kitu walikua hawajui ni kwamba nilikua siongeagi kabisa na yule jamaa. Nilikua naongea nae endapo tuu nataka aninyoe kiduku😂😂😂💔( nilikua nanyoa kama baloteli na jamaa alikua mtaalam kweli wa kunyoa)

Tukiwa form four jamaa alikuja kufukuzwa shule na darasa zima walifurahia jamaa alipofukuzwa shule🤔😔👐. Mind you kuna mwenzake alifanya makosa makubwa zaidi yake lakini darasa zima tulimuombea msamaha na akasamehewa ila jamaa hakupata support yoyote.

Mwisho naweza kusema kutokumkubali mtu sio chuki ila Kuna vitu mtu anakua navyo ndani ambavyo mnakua hamuendani tuu. Binafsi sioni kama ni chuki ila huwa nachukulia kama ni utofauti wa mitazamo na kuchukulia mambo pia mawazo mtu anayowaza ndani ya moyo wake ndio hupelekea hiyo hali.
 
Story zako zinakuga kama chai hivi mkuu 🤣🤣🙌🏼

Ila wewe huyo jamaa sio kwamba ulikua humkubali bila sababu no sababu ilikuepo ni kama hivyo ulivyosema kwa sababu alikufokea 😅
 
Story zako zinakuga kama chai hivi mkuu 🤣🤣🙌🏼

Kwahiyo mkuu mimi ni sawa na Manyanza 🤣🤣🤣👐
Sio chai ni ukweli lakini.

Ila wewe huyo jamaa sio kwamba ulikua humkubali bila sababu no sababu ilikuepo ni kama hivyo ulivyosema kwa sababu alikufokea 😅

Mimi sio mtu wa kuchukulia vitu personal na pia sikuona sababu ya jamaa kuongea maneno yale na ndio maana sikumjibu kabisa.

Lakini baada ya kuishi nae ndio nilikuja kujua kwamba hata tungebaki wawili tusingekuja kupatana na yule jamaa. Imagine darasa zima walimchukia. Ni kama alikua na damu ya kunguni😂😂

Siwezi kusema mengi nisije nikaweka utambulisho wangu humu.
 
Sawaa basi story zako sio chai🤣🤣
 
Kwani kuna kubwa hapo?
Mbona hadi mimi muuza genge najua
Mambo si yanasemwa ?
Wamiliki wa magenge mnapita maeneo mengi. Mara bosi fulani akwambie niletee nyanya za elfu 50 na vitunguu vya laki.. ukipeleka mzigo unaweza kujikuta unapata ABCs za yanayoendelea maofisini.
 
Wamiliki wa magenge mnapita maeneo mengi. Mara bosi fulani akwambie niletee nyanya za elfu 50 na vitunguu vya laki.. ukipeleka mzigo unaweza kujikuta unapata ABCs za yanayoendelea maofisini.
Hujawahi kua serious wewe 😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…