Swali zuri sana mtu mmoja wapo ni mimi,huwa siwezi kukaa na chuki kwa muda mrefu,yani tunaweza kuzinguana sasa na muda sio mrefu napotezea.
Ila kwanza ifahamike hakuna mtu ambaye hachukii au hakasirki,hizi ni hisia ambazo tumeumbwa nazo na ndio ubinadamu wenyewe
Ila tofauti inakuja kwenye kuzihifadhi hizi hisa,kuna wengine wanahifadhi kwa muda mrefu,wengine muda wa kati na wengine akina sie,chap tu tunaendelea na maisha yetu kana kwamba hakuna kilichotokea aibu unaona wewe
Kwanza ni kujua chuki inakudhuru wewe mwenyewe,yes usifikiri eti nikiimchukia flani namkomoa au ntamfanya ajisikie vibaya,hapana huenda yeye ashasahau tayar,ila wewe kila ukimuona ndio unachefukwa zaidi,kwahiyo inakutafuna wewe mwenyewe
Kwahiyo ukishalijua hili basi you let it go,kwakuwa unajipa nafasi ya kujiponya mwenyewe
Lingine fikiria katika namna ambayo ni positive zaidi
Mfano:
Binti Kiziwi amenitukana,sasa hapa fikiri au jaribu kujua kwanini amenitukana. Huenda swala ambalo limetokea baina yetu lilikuwa kubwa sana kwake kulihandle ndio maana akajikuta kanitukana,huenda hayupo strong emotionally
Kwahiyo ukifikir kwa mtazamo huu unapata justification kwani yametokea haya yaliyotokea
Lingine ni Ile hali ya kuwa na stress free, huwezi kutokuwa na stress kama kila jambo unaliweka kichwani au moyoni,jifunze kuachilia mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako
Mtu kukutukana au kutokukutukana ni swali ambalo lipo nje ya uwezo wako,ila ambalo lipo ndani ya uwezo ni jinsi gani utaamua kulipokea hilo jambo,sasa amua kulipokea positively na the rest itakuwa amani tu