Kwa Nini Tunamkubali au Kumkataa Mtu Bila Sababu?

Kwa Nini Tunamkubali au Kumkataa Mtu Bila Sababu?

Kuna kitu kinaitwa hisia

Kupitia hisia, unaweza kumchukia mtu na wakati mwingine kumpenda

Wanawake wanaweza wanaangalia filamu na kujikuta wanampenda mwigizaji fulani kupitia scene aliyofanya

Wakati mwingine kumchukia mwingine kwakuwa scene yake haijawavutia

Wengine huwa wanamchukia mtu kutokana na maneno ya kuambiwa/kusikia

Mathalani kupitia Siasa, Kuna watu wamejengwa kumchukia Tundu Lissu na wengine kumchukia Edward Lowassa

Hii hata kwenye familia, mtoto anaweza kurithi chuki za Mama yake dhidi ya baba yake

Kwamba nilipokulea wewe, baba yako hakuwajibika hata kidogo yeye alikuwa busy na michepuko

Mtoto unakuwa na kuibeba chuki hii then unaihamishia kwa baba yako

N.k n.k
Wanawake? Kwamba ninyi wanaume huwa hamuwapendi waigizaji?
 
Hapana hili nakataa,haihusiani na changomto za kiakili,ila kuna feelings au machale unayafili kuhusu mtu husika
Nahisi ndio hiyo sababu.... Mfano mkuu, ukipita mahali ambapo panasifika kwa uchangudoa... Kuna posibility kubwa ya kumshuku na kumuhisi vibaya kila mwanamke/mwanaume aliyepo mazingira hayo bila kujali kilichompeleka hapo...

Nasisitiza lazima iwepo sababu tuu
 
Exactly ndio haya ambayo tunajiuliza hapa,kwanini inakuwa hivi

Maana walau angejua mambo yako kwa kuona au kusikia walau tungesema hapa ana file langu

Je,labda huenda roho ndio zinajua kulikoni na sisi tunafeel kile ambacho roho zina experience tu?

Ni nature ya binadamu, ubinadamu ni pamoja na hisia, ziwe hasi au chanya.
Upo sehemu, huna hili wala lile, out of air mtu anakuchukia tuu na kukuletea figisu figisu.
 
Ila
Ukisoma na kuijua sayansi ya Quantum physics inaweza kutoa majibu.

Kuna viumbe hai na viumbe visivyo hai katika mazingira yanayotuzunguka.

Chochote kilichokuwepo aidha unakiona au haukioni kwa macho kinakuwa kipo katika mtetemo/vibration.



Kwa binadamu/mnyama ambaye yupo kwenye masafa ya juu lazima automatic atavutia/attraction ya wenzake wenye mtetemo unaofanana au kushabihiana.

Kama upo kwenye masafa ya juu ambayo ni upendo, amani, furaha utavutia aina ya nishati kama yako.

Ukiwa kwenye mtetemo wa kati ni hivyo hivyo pia kwenye masafa ya chini kama wivu, chuki, hasira, aibu n.k utavutia wa design hiyo pia.


Kwa hiyo kinachofanya umkubali mtu au kumkataa ni masafa/frequency mitetemo/vibration na nguvu ya uvutano/ attraction au nguvu ya kupingana/repell.
Hii point nimejaribu kuapply kwenye like unlike poles attract like poles repel haileti?
Why
 
Lazima uwe mbali na mtu au ata karibu ndo unakuta chemistry na mtu zinaendana kuleta izo feelings?
Sijui kama nitakuwa nimeelewa vizur swali lako?

Hakuna ulazima wa kuwa na mtu karibu kujua chemistry mlinayo nayo,ila the moment mnakutana tu au mnawasiliana unajua hapa tunaendana au laa

Hata mazungumzo machache ambayo mnaweza kuwa nayo you can feel kuna kitu amazing hapa
 
hakuna kitu kama "simkubali tu" au "namkubali tu" hii inatokana na vile tu unashindwa kuelezea sababu hizo either ya wewe kutotaka kuelezea ama unajikuta huwezi kuelezea mtu kwa maneno akakuelewa. lakini inawezekana wewe muhusika kuhisi huna sababu lakini zipo ni wewe hujajua kwamba kuna viashiria flani ndio vimesababisha wewe kumpenda ama kumchukia mtu.

kwamfano, wakati mwingine unamkataa mtu kwa sababu ana life flani hivi ambayo ulitamani kuwa nayo lakini sasa hukufanikiwa kuwa na hiyo life so ule wivu na ego yako ndo inakusumbua so unajikuta unamchukia huyo mtu.

lakin pia unaweza mchukia mtu kwasabab unakuta labda mtu huyo anafanana sauti, sura, au tabia na mtu fulani aliyewahi kukuumiza au kukukwaza huko nyuma. namda mwingine ukute hata humkumbuki huyo mtu aleyekuumiza au hukumbuki tukio lenyewe, lakini akili yako inatambua kama huyo mtu sio salama tokana na memory iliyohifadhi na kukuletea hisia za kutomwamini.

pia unaweza mchukia mtu ambaye ana body Language ama vibes flani ambalo hulielewi unajua nini, binadamu tunasoma lugha ya mwili bila kujitambua, kama mtu ana mtindo fulani wa kuangalia, kusimama, au vibes ambalo haiendani na mfumo wako wa maadili ama jinsi wewe ulivyo utajikuta unamkataa tu. chukulia wewe unaamini ni mstaarabu halafu atokee mtu muhuni muhuni ama haeleweki hivi lazima ujikute unamkataa kiaiana.

lakini unaweza mkataa mtu kwa sababu ya wivu wa chini kwa chini, wakati mwingine mtu ana mafanikio, mvuto, au anapendwa sana na watu, jambo ambalo linagusa mapungufu yako ya ndani (insecurities yako) badala ya kukubali kuwa wewe unamwonea wivu, akili yako inakwambia "humkubali tu" kumbe sababu ni wivu

haya tuje sababu za kumkubali mtu " ile ki moma noma" yan ile 'basi tu namkubali"
kuna ile kitu inaitwa "Halo Effect", hii inatokea ile unakutana na mtu anakua na sifa nzuri, kama labda vile muonekano wake, sauti yake, au tabasamu lake, inakufanya uamini kuwa yeye ni mtu mzuri katika kila kitu. Unajikuta unamkubali kabisa hata kama humjui kwa undani lakini unamkubali, hii hutokea sana watu wanavyowapenda mastaa, ama wengine wanaita ma crush wao kudadeki hahaaaa.

haya tuje sababu nyingine ni ile kujiona ndani ya mtu flani, yani anakua kama kioo unajiona wewe ndani yake. binadamu tunavutiwa na watu wanaofanya vitu tunavyovipenda au wanaofanana na sisi kikabila, kifikra, au kimitindo wa maisha. Ukiona mtu anakua kama anaonyesha kile ulicho nacho au unachotamani kuwa, basi unajikuta unamkubali "ki noma noma" kwa sababu anajenga picha nzuri ya wewe unavyopendezwa navyo.

lakin wengine ni ile mnajikuta mna Chemistry. Binadamu tunatoa kemikali za asili zinazoitwa pheromones ambazo zinaweza kumvutia mtu mwingine bila hata neno moja kuongelewa. Homoni kama oxytocin na dopamine zinaweza kupanda unapomwona mtu fulani, na kukufanya ujisikie furaha na amani ukiwa karibu naye au ukimwangalia.

Kwa hiyo kwa kumalizia niseme tu hakuna hisia inayokuja bila sababu. Usemi wa "namkataa tu" au "namkubali tu" ni tafsiri ambayo akili yetu inatupa pale inaposhindwa kupata maneno sahihi ya kuelezea mchakato mrefu na mgumu wa kisaikolojia unaoendelea ndani yetu.

adios! chao! 😉 👍 :ANYGIFTERS:👍
 
Katika ulimwengu wa nishati/energy kunakuwa na muingiliano wa hizo nguvu.

Muingiliano au interference huwa inatokea hata kwenye mawimbi ya sauti mathalani radio au television.

Kuna watu ambao wanauwezo wa kucheza, ku deal na kufanya manipulation ya hizo nguvu au nishati.

Wengine hawana uelewa wa Kutambua na ku detect hizo nishati kama positive au negative
.
Kwa mkuu Ertugrul Bey unaweza ukawa katika masafa ya juu positive na ukakutana nguvu au nishati hasi ambayo inajaribu kukuvuta chini.

Jambo la msingi ni kujifunza na Kutambua jinsi ya kufanya manipulation ya hizo mambo
 
Au yote haya ni namna tu akili yetu inavyofanya observation, bila sisi kujitambua?
Ndio. Akili zetu hufanya kazi kama miili yetu ya nyama. Kama mnakumbuka kwenye biolojia, ukipata magonjwa, seli zako huhifadhi kumbukumbu ya magonjwa yako ili iwe rahisi kupambana nayo baadaye.

Akili yako ya ndani(subconscious mind), hukumbuka wale waliokufanyia mabaya kipindi cha nyuma. Sasa unapokutana na mtu mwenye tabia hizo au zinazokaribiana, akili inamgomea ili kujilinda.

Pia akili ikiona ishara nzuri, nayo inajirahisisha.
 
Hii kitu ipo sana tu, mtu anaweza kukuchukia bila sababu akaishi hivyo kwa amani.

Kama ataendelea kuulizwa atoe aababu za kukuchukia basi hapo ataanza kubuni za uongo ilimradi ajifurahishe nafsi yake.

Likewise, mwingine anaweza kumpenda mtu bila sababu, hata kama akiambiwa mabaya ya huyo anayempenda, bado ataendelea kumpenda tu.

Sio ajabu yeye ndie atajipa kazi ya kumtafutia majibu yule ampendae bila sababu, tena ajabu zaidi atatafuta majibu hata pale ambapo huyo anayempenda ameishiwa hana majibu ya tuhuma zake!
 
Katika ulimwengu wa nishati/energy kunakuwa na muingiliano wa hizo nguvu.

Muingiliano au interference huwa inatokea hata kwenye mawimbi ya sauti mathalani radio au television.

Kuna watu ambao wanauwezo wa kucheza, ku deal na kufanya manipulation ya hizo nguvu au nishati.

Wengine hawana uelewa wa Kutambua na ku detect hizo nishati kama positive au negative
.
Kwa mkuu Ertugrul Bey unaweza ukawa katika masafa ya juu positive na ukakutana nguvu au nishati hasi ambayo inajaribu kukuvuta chini.

Jambo la msingi ni kujifunza na Kutambua jinsi ya kufanya manipulation ya hizo mambo
Nimekupata vizur hapo mkuu,hapo ni swala utambuzi ndio muhimu sana

Inasemwa ukikutana na nguvu hasi huwa inakawaida ya kunyonya nguvu zako chanya

Ndo ile kuna watu unafanya nao mazungumzo ukiachana nae anakuacha na uchovu tu,mathalani mtu ambaye kila mkikutana ni kuwalaumu watu na mazingira,kusenyengenya tu,kulaumu kila kitu,watu Kama Hawa wanadrain positive energy yako
 
Sijui kama nitakuwa nimeelewa vizur swali lako?

Hakuna ulazima wa kuwa na mtu karibu kujua chemistry mlinayo nayo,ila the moment mnakutana tu au mnawasiliana unajua hapa tunaendana au laa

Hata mazungumzo machache ambayo mnaweza kuwa nayo you can feel kuna kitu amazing hapa
Bado nina swali kwanini wanasema kila mtu tunayekutana naye ana sababu maalum kwa maisha yetu either kuwa funzo etc.. unakuta izo frequency ndo zinamvuta au nini au imeandikwa ukutane naye bila ata izo frequency kuendana
 
Na vile vile kujibu swali lako,kwamba kutomkubali mtu je chuki?

Kwa mtazamo wangu ni kwamba huwa tunakuwa na chuki pale tunafanyiwa matendo mabaya na wahusika,au Wakafanya jambo lolote ambalo huwa na madhara kwetu,na hapo ndio chuki inafuata kama reaction kwa kile ambacho wametufanyia

Ila hapa siwezi sema ni chuki kwasababu yani hakuna sababu tu
Kusema humkubali mtu bila sababu hiyo mimi sikubali lazima sababu ipo tu
 
Back
Top Bottom