Kwa Nini Tunamkubali au Kumkataa Mtu Bila Sababu?

Kwa Nini Tunamkubali au Kumkataa Mtu Bila Sababu?

Ndio. Akili zetu hufanya kazi kama miili yetu ya nyama. Kama mnakumbuka kwenye biolojia, ukipata magonjwa, seli zako huhifadhi kumbukumbu ya magonjwa yako ili iwe rahisi kupambana nayo baadaye.

Akili yako ya ndani(subconscious mind), hukumbuka wale waliokufanyia mabaya kipindi cha nyuma. Sasa unapokutana na mtu mwenye tabia hizo au zinazokaribiana, akili inamgomea ili kujilinda.

Pia akili ikiona ishara nzuri, nayo inajirahisisha.
Mkuu kwa muktadha wa mtu ulikutana naye hapo awali upo sahihi kwa asilimia zote

Hapa chukulia kwamba ndio kwanza unakutana na mtu kwa mara ya kwanza hakujui himjui,utasemaje hapo?
 
Ukisoma na kuijua sayansi ya Quantum physics inaweza kutoa majibu.

Kuna viumbe hai na viumbe visivyo hai katika mazingira yanayotuzunguka.

Chochote kilichokuwepo aidha unakiona au haukioni kwa macho kinakuwa kipo katika mtetemo/vibration.

Hata matter ambayo ipo kwenye solid form Imetengenezwa na particles na molecules ambazo kwa kiasi na kiwango fulani Kuna movements au vibration.

Binadamu, wanyama, wadudu n.k wanaishi katika energetic field Fulani ambayo inawasaidia ku interact.

Hizo energetic field zinakuwa katika frequency au masafa tofauti.

Masafa katika level za energy field yamegawanyika katika high frequency , low frequency & medium frequency.

Hii ina maana kwamba ili uweze kufikia high frequency lazima uwe katika mitetemo au high vibration pia, halikadhalika kwa low frequency unakuwa katika low vibes na hivyo hivyo kwenye masafa ya kati.

Tuje kwenye swali lako, kwanini unakuta unamkataa mtu au unamkubali mtu/kitu/ jambo? Bila sababu yoyote.

Kama ilivyo redio inavyofanya kazi kwenye masafa hivyo hivyo katika maisha ya nishati mambo hapo hivyo

Ukitaka kusikiliza TBC lazima itakulazimu u tune masafa ya TBC, pia ukitaka kusikiliza Radio One, Clouds, Wasafi ni mchakato huo huo.

Kwa binadamu/mnyama ambaye yupo kwenye masafa ya juu lazima automatic atavutia/attraction ya wenzake wenye mtetemo unaofanana au kushabihiana.

Kama upo kwenye masafa ya juu ambayo ni upendo, amani, furaha utavutia aina ya nishati kama yako.

Ukiwa kwenye mtetemo wa kati ni hivyo hivyo pia kwenye masafa ya chini kama wivu, chuki, hasira, aibu n.k utavutia wa design hiyo pia.

Kwa hiyo kinachofanya umkubali mtu au kumkataa ni masafa/frequency mitetemo/vibration na nguvu ya uvutano/ attraction au nguvu ya kupingana/repell.
Safi kabisa!

Kwenye Quantum Mechanics pia kuna kitu kinaitwa entanglement. Kila particle ina pacha wake na hizi particles zimegotana (entangled) na zinawasiliana papo kwa papo bila kujali umbali uliopo kati yao. Mawasiliano haya yanatawaliwa na mitetemo (frequency) inayofanana. Kwa hiyo, katika ujumla wake, unaweza kumkubali mtu aliyeko Marekani huko wakati wewe uko huku Tandahimba ndani ndani bila sababu yo yote. Kumbe mko katika mgotano na mnatetema katika masafa yanayofanana.

Kuna watu ukimuona tu yaani inakuwa rahisi sana kumkubali na kumzoea. Yaani utafikiri mmeshafamiana kwa muda mrefu. Hata hapa JF. Unaona ID tu ya mtu na nguvu fulani inakuambia kwamba huyu ni mtu poa sana na unamkubali tu otomatikale. Na mwingine ukiona tu ID yake unaboreka hata bila sababu. Kumbe hampatani katika ulimwengu wa roho ambao Quantum Mechanics inatwambia ni mpishano tu wa masafa ya mitetemo ya nishati zenu. Mitetemo hiyo ikigotana, mambo yote safiiii!

➡️➡️➡️ Kama wewe ShesRise_1. Mimi nakukubali sana tu japo sikufahamu. Inavyoonekana nishati zetu zinatetema katika masafa yanayofanana. Pengine mimi na wewe tumo katika mgotano yaani sisi ni SOULMATES! ❤ 😂😂😂🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️
 
Kuna kitu kinaitwa hisia

Kupitia hisia, unaweza kumchukia mtu na wakati mwingine kumpenda

Wanawake wanaweza wanaangalia filamu na kujikuta wanampenda mwigizaji fulani kupitia scene aliyofanya

Wakati mwingine kumchukia mwingine kwakuwa scene yake haijawavutia

Wengine huwa wanamchukia mtu kutokana na maneno ya kuambiwa/kusikia

Mathalani kupitia Siasa, Kuna watu wamejengwa kumchukia Tundu Lissu na wengine kumchukia Edward Lowassa

Hii hata kwenye familia, mtoto anaweza kurithi chuki za Mama yake dhidi ya baba yake

Kwamba nilipokulea wewe, baba yako hakuwajibika hata kidogo yeye alikuwa busy na michepuko

Mtoto unakuwa na kuibeba chuki hii then unaihamishia kwa baba yako

N.k n.k
Shukran babu
Hapa tumeona kua yote uliyoeleza yana sababu hakuna ile kusema "basi tu" si ndio?
 
Simpendi Shivji kwakuwa simpendi Tu na haikuhusu

Muhindi kwangu ni Muhindi tu kariba ya Kihindi utaijua site

Huna wa kukutetea huna wa kumuomba akuokoe wakati kila kitu kanunua

Ukiambatanisha na historia ya kubinafsisha makazi ya wakajikuta wageni sehemu waliyowekeza hutoshindwa kuona chuki yao kwa hila ya uzalendo

Siwapendi wahindi ila kiatu chao cha kibaniani nakilamba
 
Nina experience na hii kitu tena sio mara moja au mbili ni mara nyingi tu

Kwakweli binafsi naona huwa hamna sababu ya msingi,mnajikuta tu kama kipande flan cha puzzle ambacho kimekuja kukava nafasi ambayo imeachwa wazi na kukava kikamilifu, nadhani kuna kitu cha siri ambacho huenda bado hakija kuwa wazi kwenye utambuzi wetu

Na upande wa kutomkubali mtu nayo nina uzoefu nayo pia,yeah unajikuta tu unaona huyu mtu kama sio hivi, yani ni kama umbali wa mashariki na magharibi,hata ukiulizwa mbona humkubali hiyu mtu,unabakia huna majibu
Chunguza lazima kuna sababu
 
Sipingi mawazo yako,lakini hapa kumbuka hamfahamiani na mtu,maana mkianza kufahamiana ndio Kuna mambo utayajua labda kupitia vitendo vyake au maneno yake

Ila hapa ni kama ile tu unakutana na mtu kwa mara ya kwanza lakini hisia zako chap tu zinakwambia huyu mtu mbona kama sie vile
Kuna sababu trust me
 
Mimi ni Dao (asiyeonekana) nilimuumba Dei mwenye kuonekana kwa uzuri

Nikafurusha umakini wangu kwenye usingizi ili kujitafuta kwenye Mhimili wa Dei ili kujipata

Niko hivyo kufanya maisha yasichoshe infinity

Sio mimi ni QUOTE
 
Ila

Hii point nimejaribu kuapply kwenye like unlike poles attract like poles repel haileti?
Why
Kanuni ya nishati law of conservation of energy inaeleza nishati haiwezi kuharibiwa wala kutengenezwa kamwe ila inaweza ikabadilishwa kutoka aina moja au nyingine.

Kabla ya kuja kwenye sumaku na kuongelea hizo like poles na unlike poles inabidi ujikumbushe jinsi gani na namna gani mvutano na kukingana kunavyotokea. halafu itakuwa rahisi kufanya transformation.
 
Bado nina swali kwanini wanasema kila mtu tunayekutana naye ana sababu maalum kwa maisha yetu either kuwa funzo etc.. unakuta izo frequency ndo zinamvuta au nini au imeandikwa ukutane naye bila ata izo frequency kuendana
Ni sahihi kabisa ukiwa positive kwa kila kitu ambacho unakutana nacho kwenye maisha yako,utaona funzo kwa kila kitu,kila kitu kina sababu ya uwepo wake, ni Mimi na wewe kuona hekima ya kitu hicho

Hata kuachwa na mtu unayempenda sana kuna faida ndani yake ingawa inakuja maumivu yake,why if angekuja kuwa mwenza mbaya zaidi huko mbeleni? Ni bora kakuacha now kabla hamjafika mballi

Sasa kuhusu je,ni frequency zinakuvutia huko hapo sijui kwakweli
 
Kanuni ya nishati law of conservation of energy inaeleza nishati haiwezi kuharibiwa wala kutengenezwa kamwe ila inaweza ikabadilishwa kutoka aina moja au nyingine.

Kabla ya kuja kwenye sumaku na kuongelea hizo like poles na unlike poles inabidi ujikumbushe jinsi gani na namna gani mvutano na kukingana kunavyotokea. halafu itakuwa rahisi kufanya transformation.
Mwaga vitu mkuu
 
Safi kabisa!

Kwenye Quantum Mechanics pia kuna kitu kinaitwa entanglement. Kila particle ina pacha wake na hizi particles zimegotana (entangled) na zinawasiliana papo kwa papo bila kujali umbali uliopo kati yao. Mawasiliano haya yanatawaliwa na mitetemo (frequency) inayofanana. Kwa hiyo, katika ujumla wake, unaweza kumkubali mtu aliyeko Marekani huko wakati wewe uko huku Tandahimba ndani ndani bila sababu yo yote. Kumbe mko katika mgotano na mnatetema katika masafa yanayofanana.

Kuna watu ukimuona tu yaani inakuwa rahisi sana kumkubali na kumzoea. Yaani utafikiri mmeshafamiana kwa muda mrefu. Hata hapa JF. Unaona ID tu ya mtu na nguvu fulani inakuambia kwamba huyu ni mtu poa sana na unamkubali tu otomatikale. Na mwingine ukiona tu ID yake unaboreka hata bila sababu. Kumbe hampatani katika ulimwengu wa roho ambao Quantum Mechanics inatwambia ni mpishano tu wa masafa ya mitetemo ya nishati zenu. Mitetemo hiyo ikigotana, mambo yote safiiii!

➡️➡️➡️ Kama wewe ShesRise_1. Mimi nakukubali sana tu japo sikufahamu. Inavyoonekana nishati zetu zinatetema katika masafa yanayofanana. Pengine mimi na wewe tumo katika mgotano yaani sisi ni soulmates 😂😂😂🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️

Nakushukuru sana mkuu, umekwiva kwenye quantum mechanics.

Siongezi wala kupunguza neno.
 
Spiritual energy frequency differences. Kiroho level ya energy frequency zinatofautiana ndiyo maana mtu ambaye nguvu zenu za kiroho haziendani huwa kunakuwa na utofauti huo automatically.

Tunatafsiri ni chuki ila deep down utofauti wenu katika ulimwengu wa kiroho haupatani.

Huwa naamini katika masuala ya kiroho (siyo dini) na chochote katika ulimwengu wa nyama huanzia ulimwengu wa roho.
 
Back
Top Bottom