ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
- Thread starter
- #101
Jamani bicwa komwe 😅😅🙌🏼Unakuta amekuzidi uzuri basi unanuna kama ibilisi.
Wivu tu unawasumbua wajinga.
Jamani bicwa komwe 😅😅🙌🏼Unakuta amekuzidi uzuri basi unanuna kama ibilisi.
Wivu tu unawasumbua wajinga.
Safiiii ningekua na mdogo wa kike ningekupa kijana mdogo🔥🔥🔥Ndio. Akili zetu hufanya kazi kama miili yetu ya nyama. Kama mnakumbuka kwenye biolojia, ukipata magonjwa, seli zako huhifadhi kumbukumbu ya magonjwa yako ili iwe rahisi kupambana nayo baadaye.
Akili yako ya ndani(subconscious mind), hukumbuka wale waliokufanyia mabaya kipindi cha nyuma. Sasa unapokutana na mtu mwenye tabia hizo au zinazokaribiana, akili inamgomea ili kujilinda.
Pia akili ikiona ishara nzuri, nayo inajirahisisha.
Sababu hua ipo mkuuHii kitu ipo sana tu, mtu anaweza kukuchukia bila sababu akaishi hivyo kwa amani.
Kama ataendelea kuulizwa atoe aababu za kukuchukia basi hapo ataanza kubuni za uongo ilimradi ajifurahishe nafsi yake.
Likewise, mwingine anaweza kumpenda mtu bila sababu, hata kama akiambiwa mabaya ya huyo anayempenda, bado ataendelea kumpenda tu.
Sio ajabu yeye ndie atajipa kazi ya kumtafutia majibu yule ampendae bila sababu, tena ajabu zaidi atatafuta majibu hata pale ambapo huyo anayempenda ameishiwa hana majibu ya tuhuma zake!
Such a great mind,hakuna kitu kama "simkubali tu" au "namkubali tu" hii inatokana na vile tu unashindwa kuelezea sababu hizo either ya wewe kutotaka kuelezea ama unajikuta huwezi kuelezea mtu kwa maneno akakuelewa. lakini inawezekana wewe muhusika kuhisi huna sababu lakini zipo ni wewe hujajua kwamba kuna viashiria flani ndio vimesababisha wewe kumpenda ama kumchukia mtu.
kwamfano, wakati mwingine unamkataa mtu kwa sababu ana life flani hivi ambayo ulitamani kuwa nayo lakini sasa hukufanikiwa kuwa na hiyo life so ule wivu na ego yako ndo inakusumbua so unajikuta unamchukia huyo mtu.
lakin pia unaweza mchukia mtu kwasabab unakuta labda mtu huyo anafanana sauti, sura, au tabia na mtu fulani aliyewahi kukuumiza au kukukwaza huko nyuma. namda mwingine ukute hata humkumbuki huyo mtu aleyekuumiza au hukumbuki tukio lenyewe, lakini akili yako inatambua kama huyo mtu sio salama tokana na memory iliyohifadhi na kukuletea hisia za kutomwamini.
pia unaweza mchukia mtu ambaye ana body Language ama vibes flani ambalo hulielewi unajua nini, binadamu tunasoma lugha ya mwili bila kujitambua, kama mtu ana mtindo fulani wa kuangalia, kusimama, au vibes ambalo haiendani na mfumo wako wa maadili ama jinsi wewe ulivyo utajikuta unamkataa tu. chukulia wewe unaamini ni mstaarabu halafu atokee mtu muhuni muhuni ama haeleweki hivi lazima ujikute unamkataa kiaiana.
lakini unaweza mkataa mtu kwa sababu ya wivu wa chini kwa chini, wakati mwingine mtu ana mafanikio, mvuto, au anapendwa sana na watu, jambo ambalo linagusa mapungufu yako ya ndani (insecurities yako) badala ya kukubali kuwa wewe unamwonea wivu, akili yako inakwambia "humkubali tu" kumbe sababu ni wivu
haya tuje sababu za kumkubali mtu " ile ki moma noma" yan ile 'basi tu namkubali"
kuna ile kitu inaitwa "Halo Effect", hii inatokea ile unakutana na mtu anakua na sifa nzuri, kama labda vile muonekano wake, sauti yake, au tabasamu lake, inakufanya uamini kuwa yeye ni mtu mzuri katika kila kitu. Unajikuta unamkubali kabisa hata kama humjui kwa undani lakini unamkubali, hii hutokea sana watu wanavyowapenda mastaa, ama wengine wanaita ma crush wao kudadeki hahaaaa.
haya tuje sababu nyingine ni ile kujiona ndani ya mtu flani, yani anakua kama kioo unajiona wewe ndani yake. binadamu tunavutiwa na watu wanaofanya vitu tunavyovipenda au wanaofanana na sisi kikabila, kifikra, au kimitindo wa maisha. Ukiona mtu anakua kama anaonyesha kile ulicho nacho au unachotamani kuwa, basi unajikuta unamkubali "ki noma noma" kwa sababu anajenga picha nzuri ya wewe unavyopendezwa navyo.
lakin wengine ni ile mnajikuta mna Chemistry. Binadamu tunatoa kemikali za asili zinazoitwa pheromones ambazo zinaweza kumvutia mtu mwingine bila hata neno moja kuongelewa. Homoni kama oxytocin na dopamine zinaweza kupanda unapomwona mtu fulani, na kukufanya ujisikie furaha na amani ukiwa karibu naye au ukimwangalia.
Kwa hiyo kwa kumalizia niseme tu hakuna hisia inayokuja bila sababu. Usemi wa "namkataa tu" au "namkubali tu" ni tafsiri ambayo akili yetu inatupa pale inaposhindwa kupata maneno sahihi ya kuelezea mchakato mrefu na mgumu wa kisaikolojia unaoendelea ndani yetu.
adios! chao! 😉 👍👍
Hakikabila sababu == sababu nisizotaka kuzitaja
Mkuu maelezo yako nimeyaelewa vizuri yanaleta majibu kwanini huwa tunaenda sawa na watu fulani na kwanini wengine hatuendi nao sawaSafi kabisa!
Kwenye Quantum Mechanics pia kuna kitu kinaitwa entanglement. Kila particle ina pacha wake na hizi particles zimegotana (entangled) na zinawasiliana papo kwa papo bila kujali umbali uliopo kati yao. Mawasiliano haya yanatawaliwa na mitetemo (frequency) inayofanana. Kwa hiyo, katika ujumla wake, unaweza kumkubali mtu aliyeko Marekani huko wakati wewe uko huku Tandahimba ndani ndani bila sababu yo yote. Kumbe mko katika mgotano na mnatetema katika masafa yanayofanana.
Kuna watu ukimuona tu yaani inakuwa rahisi sana kumkubali na kumzoea. Yaani utafikiri mmeshafamiana kwa muda mrefu. Hata hapa JF. Unaona ID tu ya mtu na nguvu fulani inakuambia kwamba huyu ni mtu poa sana na unamkubali tu otomatikale. Na mwingine ukiona tu ID yake unaboreka hata bila sababu. Kumbe hampatani katika ulimwengu wa roho ambao Quantum Mechanics inatwambia ni mpishano tu wa masafa ya mitetemo ya nishati zenu. Mitetemo hiyo ikigotana, mambo yote safiiii!
➡️➡️➡️ Kama wewe ShesRise_1. Mimi nakukubali sana tu japo sikufahamu. Inavyoonekana nishati zetu zinatetema katika masafa yanayofanana. Pengine mimi na wewe tumo katika mgotano yaani sisi ni soulmates ❤ 😂😂😂🏃🏿♂️🏃🏿♂️🏃🏿♂️
Hakika na kuna watu humu JF wanafanya hivyo, nongwa binafsi na kusambaza watu uongo kumhusu mtu.Wengine hufuata mkumbo tu. Na inaenda mbali zaidi kuwalazimisha na wenzao wamchukie huyo mtu. Yaweza kuwa mi nipo upande fulani koiyo ugomvi wenu usiathiri mahusiano ya wengine
Mbona soul mates 😅😅😅Safi kabisa!
Kwenye Quantum Mechanics pia kuna kitu kinaitwa entanglement. Kila particle ina pacha wake na hizi particles zimegotana (entangled) na zinawasiliana papo kwa papo bila kujali umbali uliopo kati yao. Mawasiliano haya yanatawaliwa na mitetemo (frequency) inayofanana. Kwa hiyo, katika ujumla wake, unaweza kumkubali mtu aliyeko Marekani huko wakati wewe uko huku Tandahimba ndani ndani bila sababu yo yote. Kumbe mko katika mgotano na mnatetema katika masafa yanayofanana.
Kuna watu ukimuona tu yaani inakuwa rahisi sana kumkubali na kumzoea. Yaani utafikiri mmeshafamiana kwa muda mrefu. Hata hapa JF. Unaona ID tu ya mtu na nguvu fulani inakuambia kwamba huyu ni mtu poa sana na unamkubali tu otomatikale. Na mwingine ukiona tu ID yake unaboreka hata bila sababu. Kumbe hampatani katika ulimwengu wa roho ambao Quantum Mechanics inatwambia ni mpishano tu wa masafa ya mitetemo ya nishati zenu. Mitetemo hiyo ikigotana, mambo yote safiiii!
➡️➡️➡️ Kama wewe ShesRise_1. Mimi nakukubali sana tu japo sikufahamu. Inavyoonekana nishati zetu zinatetema katika masafa yanayofanana. Pengine mimi na wewe tumo katika mgotano yaani sisi ni soulmates ❤ 😂😂😂🏃🏿♂️🏃🏿♂️🏃🏿♂️
Jambo la kuzingatia ni nishati tu.Hii una experience nayo mkuu?
Yaani unakutana na mtu unajikuta upo active kama mnafahamiana kwa muda mrefu na unahisi amani na huyo mtu
Hivi ni kweli hakuna sababu?
Na hapa pia una experience mkuu ilikuaje yaani?
Labda ana sukuma ndinga kali halafu wewe unapeta kwa mguu😀Hapa tukubaliane kutokukubaliana, hapa nakutana na mtu hanijui na simjui hay sababu zinatoka wapi?
Aiseeeee noma sanaSimpendi Shivji kwakuwa simpendi Tu na haikuhusu
Muhindi kwangu ni Muhindi tu kariba ya Kihindi utaijua site
Huna wa kukutetea huna wa kumuomba akuokoe wakati kila kitu kanunua
Ukiambatanisha na historia ya kubinafsisha makazi ya wakajikuta wageni sehemu waliyowekeza hutoshindwa kuona chuki yao kwa hila ya uzalendo
Siwapendi wahindi ila kiatu chao cha kibaniani nakilamba
Karibu sanaNipo mdada mkubwa
Usiongeze chupa nyingine😁Mimi ni Dao (asiyeonekana) nilimuumba Dei mwenye kuonekana kwa uzuri
Nikafurusha umakini wangu kwenye usingizi ili kujitafuta kwenye Mhimili wa Dei ili kujipata
Niko hivyo kufanya maisha yasichoshe infinity
Sio mimi ni QUOTE
Hapa naitaji kiti nikae mkuu nina mkanganyiko aiseeeSpiritual energy frequency differences. Kiroho level ya energy frequency zinatofautiana ndiyo maana mtu ambaye nguvu zenu za kiroho haziendani huwa kunakuwa na utofauti huo automatically.
Tunatafsiri ni chuki ila deep down utofauti wenu katika ulimwengu wa kiroho haupatani.
Huwa naamini katika masuala ya kiroho (siyo dini) na chochote katika ulimwengu wa nyama huanzia ulimwengu wa roho.
Ah sasa huo n uwendawazimu 😂Haiwezekani unaweza kua umemuona hata ni handsome kukuzidi au ana six-pack wewe una miliki kitambi jokes😅
Tena 😆 tulia mzee🤣Mkuu maelezo yako nimeyaelewa vizuri yanaleta majibu kwanini huwa tunaenda sawa na watu fulani na kwanini wengine hatuendi nao sawa
Hiyo paragraph ya mwisho mwewnyewe mhusika inamhusu🤣🤣
Nitaanzia mbali kidogoNini huwa sababu, au ni kipi kinapelekea mtu kusema:
Ujue mimi mtu fulani simkubali wala nini!
Ukimuuliza why? hana sababu
Kwa kifupi, yeye anadai tu hamkubali tu
Hivi hili linawezekana vipi? 🤔
Yaani mtu usimpende au usimkubali bila sababu?
Au sababu ipo ila imejificha kiasi kwamba hata mhusika mwenyewe haijui?
Au mwingine atasema:
Mi mtu fulani namkubali ki noma noma
Ukimuuliza why? anasema
Basi namkubali tu
Hivi huwa kweli ni basi tu au kuna sababu fulani nyuma yake ambayo hata wewe mwenyewe huijui?
Au tuseme labda mtu humkubali mtu fulani bila kujua sababu, kumbe behind the scenes huyo mtu si mtu mzuri?
Yaani huwa kuna nguvu fulani inayotokea ndani yetu ambayo hatuielewi, ikitusukuma kumkubali au kutomkubali mtu fulani kwa sababu labda inajaribu kutuepusha na madhara ambayo yanaweza kutokea?
Au yote haya ni namna tu akili yetu inavyofanya observation, bila sisi kujitambua?
Na mwisho kabisa…
Je kutokumkubali mtu tafsiri yake ni chuki ?
Au kuna tafsiri nyingine ?
Chemsha bongo 🧠 na ShesRise_1 ✋️
Shukran sana mkuuJambo la kuzingatia ni nishati tu.
Usimfikirie mtu kama mtu au mnyama kama mnyama au mdudu kama mdudu.
Jifunze na tambua jinsi ya ku sense na ku detect energy na kuitumia hiyo nishati positively.
Mfano ukikaa au ukikutana na mtu usim judge au kumtafsiri kwa jinsi alivyo kwa muonekano wa nje jitahidi usikilizie na kuhisi mtetemo, masafa na nishati yake.
Ulishasikia ule msemo damu zetu zinaendana? Bila shaka unaujua.
Issue ni kwamba mmekutana watu wenye energy level zinazofanana au kushabihiana ndio unajikuta unajisikia vizuri zaidi na nguvu.
Ulishapanda daladala yenye mlango wa mbele tu ukakuta siti za mbele zote zipo wazi hazina abiria ila Kuna nafasi Moja ipo nyuma Kuna mtu unajikuta umeacha nafasi zote umekaa naye siti moja for no reason?
Kila kitu Kina energy na jifunze kufikiria, kutenda hata kufanya maamuzi kwa ku consider energy field.
Nimeipenda hiiJambo la kuzingatia ni nishati tu.