Kwa Nini Ukristo Hauna Mfumo wa Social Guidance Kama Uislamu na Uyahudi?”

Kwa Nini Ukristo Hauna Mfumo wa Social Guidance Kama Uislamu na Uyahudi?”

Hata Uislamu pia tuna concept ya kutii mamlaka. Qur'an 4:59 inaamuru waumini kumtii Allah, Mtume na ulil-amr (wenye mamlaka), huku utii uwe ndani ya mipaka ya haki.

Lakin haiondoi haki ya dini kuwa na guidance zake za namna ya watu kuishi na kufafanua Mambo , Ikiwa dini ipo kwenye hali ya minority lazima itii mamlaka na sheria kwa haki.

Lakin ikiwa ndio Supiority lazima iwe na mfumo wake kamili wa kuongoza jamii, kwa Ukristo sio kwamba haitaki kulazimisha jamii, tatizo ni kwamba haina huo mfumo wa kuongoza jamii.

Ndio maana hata inchi zenye majority ya wakristo bado kila Mtu anaishi kwa utaratibu wake, hamna single comprehensive religious civil code. watu wanatafuta majibu na ufafanuz nje Ukristo,

Muislamu anaweza kuishi UK, marekani na akutii sheria ya nchi, lakini bado akawa na Sharia kama religious framework inayomwongoza kwenye ibada, ndoa, talaka, mirathi, biashara, madeni, mali, familia na mambo mengine ya maish
Umesoma comment iliyofuata niliyokuwekea vifungu?
 
Kila kitu kimeandikwa ni kutenga muda wako kusoma. Pia Yesu hakuja kutengua torati mkuu jielimishe.

1. Mirathi
Kumbukumbu la Torati 21:15–17
“Akina mtu wawili wakimwoa wake, mmoja apendwaye na mmoja achukiwaye, nao wakamzalia wana, na mzaliwa wa kwanza ni wa yule mke achukiwaye; ndipo itakapokuwa siku ya kumpa wanawe urithi wake, hatamfanya mwana wa mke apendwaye kuwa mzaliwa wa kwanza mbele ya mwana wa mke achukiwaye, aliye mzaliwa wa kwanza; bali atamkubali mwana wa mke achukiwaye kuwa mzaliwa wa kwanza, kwa kumpa sehemu mbili za mali yake yote...
2.Hukumu
Mambo ya Walawi 19:15
“Hamtatenda uovu katika hukumu; hutamfavouri maskini, wala hutamheshimu mwenye cheo; kwa haki utamhukumu jirani yako.”

Kutoka 18:21–22
“Zaidi ya hayo utachagua katika watu wote watu wenye uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wanaochukia tamaa; nawe uwaweke juu yao kuwa wakuu wa maelfu, wakuu wa mamia, wakuu wa hamsini, na wakuu wa makumi; nao wahukumu watu kila wakati...”

3. Migogoro
Mathayo 18:15–17
“Na ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonye faraghani; akikusikia umempata ndugu yako. Lakini asiposikia, chukua pamoja nawe mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikia hao, liambie kanisa; na asipolisikia kanisa, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.”
4. Maadili ya Jumla
Mika 6:8
“Ameonyesha kwako, ee mwanadamu, lililo jema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.”
Huzo ni Mosaic law na unavysema hakuja kutengua Torah, kwahy unamaanisha mkristo bado anaweza kuhukumiwa kwa sheria za Torah?

Kutenda haki, upendo, kuwa mnyenyekevu kusamehe, kutoa Msada hizi ni moral principle zinakuambia nini chema na kibaya

Tofauti na legal code zinakuwa ni set za sheria zinazotolew kwenye jamii kufafanua Mambo na kuhukumia vitu

Kwa mfano, Mtu akifanya kosa fulani, sheria inaeleza kosa hilo ni lipi, litathibitishwaje, nani atasikiliza kesi, na adhabu au suluhisho litakuwa nini
 
KIasi umesema sawa. Hii tofauti ni kubwa mno na ni ngumu sana kuielewa kwa njia rahisi.
Dini ya Kiyahudi na Uisilamu unafundisha dini ya nje ya mwili yaani mtu anafundishwa matendo yanayoongozwa na taratibu za nje ambazo zinamuongoza kuishi na zinamuongoza amfurahishe au kumpendeza Mungu.
mfano taratibu za ibada, kutawadha au kuosha mwili ni sehemu ya mambo ambayo dini ya Kiyahudi na Kiislamu huongoza muumini katika usafi mbele za Mungu wake, huu ni usafi wa nje au usafi wa mwili sio wa nia
Mirathi ni moja ya mfano ulioutoa nami nitautumia, huu ni utaratibu wa kisheria wa kugawana mali unaongozwa na sheria za nje si za nia, mtu atapewa kulingana na taratibu si kulingana na upendo uliopo mioyoni, UKristo una deal na roho au moyo wa muumini(akili) amabayo kama itamuelekea Mungu usafi wa mwili si kitu bali usafi wa moyo hivyo kutawadha au kutotawadha si kitu kama moyo wako haujatawaliwa na nia ya Mungu. Mayahudi wajisafisha sana kila siku wakati wa ibada zao lakini wakimaliza wanamuua mtoto wa jirani ya mplalestina , sasa hapa utaratibu wa kidini umesaidia nini?
Uchoyo wa mtu hautibi kwa sheria za mirathi, mtu mchoyo mbele za sheria atatekeleza takwa la sheria ya mirathi lakini moyoni mwake ataendelea kuwa na nia ya kudhulumu ndugu yake, hivyo kwa nje ametekeleza takwa la kidini lakini moyoni hana nia njema ya Kimunngu.
Kwa kufupisha Uyahudi na Usilamu unatatua tatizo kwa nje yaani matokeo kwa kuweka taratibu na sheria kadhaa , lakini Ukristo unashughulika na chanzo cha tatizo ambalo ni moyo wa mtu. Moja ni dini ya nje ya roho na nyingine ni dini ya rohoni
Umeongea vyema sana...
 
Huzo ni Mosaic law na unavysema hakuja kutengua Torah, kwahy unamaanisha mkristo bado anaweza kuhukumiwa kwa sheria za Torah?

Kutenda haki, upendo, kuwa mnyenyekevu kusamehe, kutoa Msada hizi ni moral principle zinakuambia nini chema na kibaya

Tofauti na legal code zinakuwa ni set za sheria zinazotolew kwenye jamii kufafanua Mambo na kuhukumia vitu

Kwa mfano, Mtu akifanya kosa fulani, sheria inaeleza kosa hilo ni lipi, litathibitishwaje, nani atasikiliza kesi, na adhabu au suluhisho litakuwa nini
Mkuu nikuulize swali.

Sheria za dini zinapogongana na za serikali/mamlaka ipi inapewa kipaumbele?
 
Kwahiyo nyinyi mnaenda na wakati kwa kuambiwa muwe mashoga kwenye ukristo ni sawa
Leta hapa hizo sheria unazosema ni against humanity devolopment wakati wewe bado unaishi kwenye shimo la uchafu wa afrika huku wanaofata hizo sheria nchi zao zimeendelea
Jina lako tu ni matako na unaongelea ushoga maana makebo yako wameyatumia sana ...hivi ww ushoga unauona kwa wakristo tu hebu chukua mfano bora hapa tz mashoga mengi ni waislam
 
Yani swali langu wakristo wanaish kwa utaratibu gani kuanzia ibada na Hadi maisha ya kila siku au kila mtu na maamuzi yake

Maana Muislamu anaweza kufungua Qur'an na Sunnah/fiqh na kupata hukumu au sheria kuhusu ibada,au mfano mirathi humo atakuta mfumo wa kujua nani ni mrithi, nani anazuiwa kurithi na share yake ni kiasi gani.

Au Myahudi anafuata Halakha anaweza kwenda kwenye sheria za Jewish inheritance na kupata kanuni zake.

Mkristo mnanda wapi kuhumiana Mambo yenu ?
hapa ndipo tofauti ya Wakristo na iman nyingine. kwetu sheria kuu ni upendo. ni badiliko la ndani sio nje. ukiwa na upendo huhitaji sheria. wana wa israel walipewa sheria za mwilin ili wakazitumie wakifika nchi ya ahadi. kumbuka walikuwa nchi ya kigen kizaz kizima so wakaanza safar ya kurud nchi yao waliyoahidiwa wazee wao so hiyo nchi ilikuwa ndio wataenda kuish na kumuabud Mungu mtakatifu so lazima sheria wapewe ili wajue namna ya kuishi maeneo matakatifu. hata wakristo wako safarin kwenda nchi ya ahad ya mbinguni na badala ya kuweka sheria mwilin huku sheria zipo rohon maana ni ndan ya moyo ndimo yalipo mawazo machafu na mipango mibovu. so ukiufundisho moyo upendo utapata jamii yenye hitimisho la pamoja na kwasabu Mungu ni upendo anakuwa pamoja nanyi muda wote. so tuko kwenye.safar ya kiroho kuelekea nchi tuliyoahidiwa na Bwana. na kanuni kuu ya huku njian ni upendo. ndio sheria.
 
Back
Top Bottom