Amani iwe nanyi.
Mimi ni mmoja wa watumiaji wa mitandao ya kijamii, specifically Whatsapp. Katika matumizi hayo, napitia sana Status za marafiki pamoja na jamaa zangu.
Sawa.
Ninao jamaa ambao nawafahamu wanafanya kazi katika idara na majeshi husika. Japo hawapost mara nyingi, ila wanapopost huwa wanamweka Magufuli katika kurasa zao hizo, ikiambatana na caption mbakimbali kama Mwamba, emoji za machozi, nk
Binafsi sioni tatizo hapa.(Unawafahamu) marafiki, au umejiingiza vipi kwenye hayo makundi? Hususan Wassapu?
Ukifatilia trend, hata hapo majuzi wakati wa Sikukuu ya Noeli, video ya Magufuli ndiyo iliyotrend zaidi ya video ya Mh Rais Samia. Video ile ilisambazwa kwa wingi na sehemu kubwa ya Watumishi majeshi tajwa.
Bado sijaona tatizo, na naamini kama hata wameposti hizo Video wamefanya kama Raia wa Kawaida...au Ukiwa Mjeshi wewe sio Binadamu? au Raia? wa Nchi?
Sheria zinasemaje kuhusu Jeshi au Wanajeshi kutumia TEHAMA?
Watu hao katika post zao tisa kwa wastani, basi Mh Samia atapostiwa mara moja pekee au asipostiwe kabisa.
Bado sijaona Tatizo... Naona kama kawivu hapa? Unawachongea kiaina hapa...au?
Sina shaka na kuwaamulia watu hao nini cha kupost, ila nina hamu kufahamu nini haswa kinawafanya wamkumbuke Rais Magufuli zaidi ya Mh Samia?
Haha, ...si "Unawafahamu" kwa nini Usiwaulize? au haukuwa na Ujasiri huo? Kama kweli unawafahamu na upo kwenye kundi lao kwanini usiwa dodose zaidi? Ahhh ...Ebo Raisi Samia yupo hapa Duniani...Jazba tofauti. na Walio hai na Waliotangulia au? Kwanini? Umkumbuke...?
Katika kuwadodosa, wanasema wazi Magufuli aliboresha maisha yao na kuwapa meno kwa kiasi kikubwa..
Uliwauliza? ( ) Ni nini Kibaya katika Kuboresha maisha ya Raia wako? Wowote? Haya meno...Ndio yapi?
Rais Samia kwa upande mwingine anaonekana kuwabana na kuwarudisha katika mstari wa kusimamia haki na kuwalinda Raia.
Mhhh , Unataka kusema nini hapa...kweli hao ni marafiki zako? Wanabanwa na nini haswa? Ni sawa kuwabana Jeshi lako? Hakuna Jenerali au Amiri Jeshi Mkuu sehemu yeyoye ile katika Dunia anataka kufanya Hivyo....ni Kutafuta taharuki....
Je,nini haswa kinawafanya Wamkumbuke Rais Magufuli kuliko Amri Jeshi Mkuu wa sasa?
Kwa maana nyingine unataka kudai hawafutailii Amri, hawamtii Amri Jeshi Mkuu....Ukumbuke huko juu nimesoma Mama.... hapa Imekaaje mara bin vuuu ni Amri Jeshi Mkuu? Unataka kusema nini? Kumkumbuka? Kuto tii Amri? Walimtii Amri Hayati kuliko Mama kwa Sababu yeye ndio anyetoa Amri Kuu....sielewi hapa...
Kuna siri nyuma ya pazia ambayo hatuifahamu?
Mtu ambaye ame "dodosa" na Kuambiwa kuwa maisha yao yaliboreshwa na kupewa meno(nguvu za kisheria au? Bado tu kuna kitu? Hujaridhika na dodosa zako? au Siri nyuma ya pazia? la nani Amri Jeshi au Mama au 'Unaowafahamu' Unazusha? Unakisia
Hayo juu ni maswali nilikuwa najiuliza(hauna ulazimu wa kujibu) nilitumia kujaribu kukudadavua, sina hoja yeyote ile....Walakin
Ninavyo dadavua naona unataka kuchonganisha, Kuzusha a hatma yake,Ungependa kuwaona wanalala katika hali duni? Ungependa kuona wanachukuliwa hatua, kwa meno tena kwa sababu video zao zimetrendi, au kwasababu walimpenda Hayati Raisi.
Jamani! kazi ipo.
Amani iwafikie