Kwa nini Wanajeshi, polisi, magereza na Usalama wa Taifa bado wanamlilia Rais Magufuli?

Kwa nini Wanajeshi, polisi, magereza na Usalama wa Taifa bado wanamlilia Rais Magufuli?

Amani iwe nanyi.

Mimi ni mmoja wa watumiaji wa mitandao ya kijamii, specifically Whatsapp. Katika matumizi hayo, napitia sana Status za marafiki pamoja na jamaa zangu.

Ninao jamaa ambao nawafahamu wanafanya kazi katika idara na majeshi husika. Japo hawapost mara nyingi, ila wanapopost huwa wanamweka Magufuli katika kurasa zao hizo, ikiambatana na caption mbakimbali kama Mwamba, emoji za machozi, nk

Ukifatilia trend, hata hapo majuzi wakati wa Sikukuu ya Noeli, video ya Magufuli ndiyo iliyotrend zaidi ya video ya Mh Rais Samia. Video ile ilisambazwa kwa wingi na sehemu kubwa ya Watumishi majeshi tajwa.

Watu hao katika post zao tisa kwa wastani, basi Mh Samia atapostiwa mara moja pekee au asipostiwe kabisa.

Sina shaka na kuwaamulia watu hao nini cha kupost, ila nina hamu kufahamu nini haswa kinawafanya wamkumbuke Rais Magufuli zaidi ya Mh Samia?

Katika kuwadodosa, wanasema wazi Magufuli aliboresha maisha yao na kuwapa meno kwa kiasi kikubwa..

Rais Samia kwa upande mwingine anaonekana kuwabana na kuwarudisha katika mstari wa kusimamia haki na kuwalinda Raia.

Je,nini haswa kinawafanya Wamkumbuke Rais Magufuli kuliko Amri Jeshi Mkuu wa sasa?

Kuna siri nyuma ya pazia ambayo hatuifahamu?
Mwaka 2016 mchambuzi mmoja aliandika kwenye moja ya yale magezeti yaliyofungwa kuwa ingawa tulipiga kura 2015 kuchagua viongozi tulikuwa tunatawaliwa na vyombo! Nchi ilikabidhiwa kwenye vyombo ambavyo baadhi kama Polisi vilipewa madaraka yasiyokuwa na mipaka kama ilivyokuwa Afrika ya Kusini ya Makaburu!
 
Kila binaadamu ana dhambi zake na atazitumikia na ndio maana nikasema hata hao viongozi waliyopita huko nao walikuwa na madhambi yao waliuwa na kutesa watu pia ila tofauti hapa hamuwachukii pamoja na kufanya hayo maovu yao, labda mseme watu aliyowauwa Magufuli wana hadi ya mitume ndio maana mmeguswa sana na mawauwaji aliyofanya Magufuli.
Wewe ndiyo wajua nani waliuliwa na Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete? Waandike hapa basi utujuze ila sisi tunaandika waliouliwa na dikteta Magufuli ambaye Mungu alimkataa tarehe 17/03/21 kutokana na maovu yake kwa watanzania
 
Kuna professor wa nchi jiran alisema "tunataka Magufuli wa Afrika" ili alinyooshe bara la Afrika. Hivyo aliinyoosha mambo mengi nao wakapumua kwa raha ndio maana anakumbukwa. Kabla sijalala usiku ni lazima nisikilize hotuba zake alizotoa nyakati za mwisho kabla ya kifo chake.
 
Amani iwe nanyi.

Mimi ni mmoja wa watumiaji wa mitandao ya kijamii, specifically Whatsapp. Katika matumizi hayo, napitia sana Status za marafiki pamoja na jamaa zangu.

Ninao jamaa ambao nawafahamu wanafanya kazi katika idara na majeshi husika. Japo hawapost mara nyingi, ila wanapopost huwa wanamweka Magufuli katika kurasa zao hizo, ikiambatana na caption mbakimbali kama Mwamba, emoji za machozi, nk

Ukifatilia trend, hata hapo majuzi wakati wa Sikukuu ya Noeli, video ya Magufuli ndiyo iliyotrend zaidi ya video ya Mh Rais Samia. Video ile ilisambazwa kwa wingi na sehemu kubwa ya Watumishi majeshi tajwa.

Watu hao katika post zao tisa kwa wastani, basi Mh Samia atapostiwa mara moja pekee au asipostiwe kabisa.

Sina shaka na kuwaamulia watu hao nini cha kupost, ila nina hamu kufahamu nini haswa kinawafanya wamkumbuke Rais Magufuli zaidi ya Mh Samia?

Katika kuwadodosa, wanasema wazi Magufuli aliboresha maisha yao na kuwapa meno kwa kiasi kikubwa..

Rais Samia kwa upande mwingine anaonekana kuwabana na kuwarudisha katika mstari wa kusimamia haki na kuwalinda Raia.

Je,nini haswa kinawafanya Wamkumbuke Rais Magufuli kuliko Amri Jeshi Mkuu wa sasa?

Kuna siri nyuma ya pazia ambayo hatuifahamu?
Magufuli aliwapa rushwa ili wamlinde aliokuwa anavunja katiba. Operesheni vyeti feki haikugusa majeshi. Rushwa kwa trafiki ilhalalishwa kwa jina la hela ya kubrashi viatu. Mishahara, vyeo na marupurupu manono kwa mejeshi. Baadhi ya polisi ni kama majambazi waliohalalishiwa kazi yao. Hivi wasiojulikana walikuwa raia wa kawaida (civilian)?
 
Ha ha ha ha, mkuu Magufuli alikuwa mtu makini saana, itatuchukua miaka mingi sana kumpata mtu kama huyo tena... miaka mingi sana nasema
Mungu ni mwema. Hawezi kuruhusu nchi hii itawaliwe na shetani. Atahakikisha inaongozwa na watu wenye hekima.
 
Kuna professor wa nchi jiran alisema "tunataka Magufuli wa Afrika" ili alinyooshe bara la Afrika. Hivyo aliinyoosha mambo mengi nao wakapumua kwa raha ndio maana anakumbukwa. Kabla sijalala usiku ni lazima nisikilize hotuba zake alizotoa nyakati za mwisho kabla ya kifo chake.
Ni ipi inakufurahisha zaidi? Ukichagua mpinzani sahau maendeleo? Mlale na mavi yenu ndani ya nyumba zenu? Ukimwi kwenu, tetemeko kwenu, katerero kwenu?
 
Itakuwa wana miss police state.
 
Wewe ndiyo wajua nani waliuliwa na Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete? Waandike hapa basi utujuze ila sisi tunaandika waliouliwa na dikteta Magufuli ambaye Mungu alimkataa tarehe 17/03/21 kutokana na maovu yake kwa watanzania
Tatizo langu hata sio nyie kuandika hao waliyouliwa au kuteswa na Magufuli ila nawashangaa kwamba kwanini mnachukia Magufuli? Maana tukio la Ulimboka hatukuona kumchukia Kikwete na tena hao Chadema walirushiwa hadi bomu na baadhi ya wakafa ila bado Hamkumchukia Kikwete, enzi hizo Cuf walichezea sana vipondo vya polisi na hadi kuuliwa ila hakukuwa na kumchukia Rais aliyefanya hivyo madarakani na hapo ndio napowashangaa.
 
Nani kakudanganya hivo wewe dada?
Ukizungumzia ushetani unazungumzia madhambi na uzinifu ni dhambi, sasa kama wewe zinifu la kutupa malaya halafu unategemea usiwe shetani wakati vitendo vyako ni vya kishetani? Hata huyo shetani mwenyewe aliitwa hivyo baada ya kufanya dhambi.
 
Tatizo langu hata sio nyie kuandika hao waliyouliwa au kuteswa na Magufuli ila nawashangaa kwamba kwanini mnachukia Magufuli? Maana tukio la Ulimboka hatukuona kumchukia Kikwete na tena hao Chadema walirushiwa hadi bomu na baadhi ya wakafa ila bado Hamkumchukia Kikwete, enzi hizo Cuf walichezea sana vipondo vya polisi na hadi kuuliwa ila hakukuwa na kumchukia Rais aliyefanya hivyo madarakani na hapo ndio napowashangaa.
Ulimboka yupo hai, je yuko wapi Ben Saanane, Azory Gwanda, Lwajabe na wale wa kwenye viroba?

Chuki siyo kitu unachofundishwa au kuiga, bali ni response to natural stmuli. Huwezi kuwashawishi watu wamchukie Kikwette kwa sababu ya kuvamiwa Ulimboka.

Na hata wanaomchukia Magufuli siyo kwamba kuna mahali wamefanya mkutano na kuamua kuwa sasa tumchukie Magufuli. Bali ni matokeo ya vitendo vyake viovu dhidi ya Watanzania, kila mmoja anaandika kwa namna alivyoathiriwa.
 
Hata Lissu yupo hai pia ila hiyo haibadili kuwa kitendo alichofanyiwa ni kiovu kama Kikwete alivyomfanyia Ulimboka ni unyama sio ubinaadamu ila hamkujenga chuki kwa unyama huo ikiwa kweli mnachukia Magufuli kwa unyama aliyoufanya kwa Lissu na wengineo, vinginevyo itakuwa chuki yenu imejengwa kwa kitu kingine kabisa na si hayo matukio ya Lissu na Bensaa8.
 
Haya ni baadhi ya matukio niliyoyakumbuka kwa haraka,

1. Alizika uhuru wa vyombo vya habari na kutia saini sheria kandamizi kwa vyombo vya habari. Vyomno vyote vililazimishwa kumuandika kwa kumsifu na kumpamba, kilichothubutu kumkosoa kilifungiwa.

2. Alitumia nguvu nyingi kupambana na upinzani na kutesa wanasiasa wa upinzani kwa kuwafungulia kesi za uongo

3. Aligawanya nchi kwa misingi ya ukabila, ukanda, uchama na udini na ubaguzi wa kijinsia.

4. Alibomoa nyumba za wakazi wa Kimara- Kibamba bila kuwafidia huku akiwaacha wa Mwanza kwa kuwa ndiyo walimpigia kura

5. Alihakikisha wakuu wa vyombo vya ulinzi wanatoka kanda ya ziwa ili kumlinda likitokea lolote, CDF - Mara, IGP - Mara na CGP - Geita na CGF - Mwanza. Madikteta wote hufanya hivi maana wanajua watu wa kwao hawawezi kuwageuka.

6. Hakupandisha mishahara kwa wafanyakazi wa umma kwa miaka yote 6 ya utawala wake.

7. Hakutangaza ajira mpya katika kipindi chote cha utawala wake. Waalimu waliomaliza vyuo mwaka 2015 hadi leo wapo mtaaji jobless.

8. Aliua sekta binafsi kwa kutoza kodi kubwa, na kuharibu mazingira ya biashara. Hoteli nyingi za kitalii zimekufa kama vile Ngurdoto, Impala, Naura Spring na nyingine zimegeuka hostel za wanafunzi kama Landmark ya Ubungo.

9. Alipunguza mzunguko wa pesa mtaani na kuhakikisha matajiri wanaishi kama mashetani.

10. Katika utawala wake waliibuka watu wasiojulikana ambao waliteka, kujeruhi na kuua watu wasio na hatia. Watu hao walimpiga risasi Tundu Lissu mchana kweupe na mpaka leo hawajakamatwa.

11. Aliwapa nguvu baadhi ya viongozi kama vile Makonda na Sabaya kutesa na kuumiza wananchi kadri walivyojisikia. Makonda alishambulia kituo cha CMG kwa mitutu ya bunduki lakini hakuchukuliwa hatua yoyote.

12. Alifuta fao la kujitoa na kusababisha watumishi wengi wenye mikataba ya muda mfupi kuishi maisha magumu baada ya ajira zao kukoma.

13. Katika serikali yake Wapinzani walionekana maadui na sio watu wenye mawazo mbadala. Waliteswa na kufunguliwa kesi za uchochezi. Alitamani upinzani ufe.

15. Katika utawala wake maiti 17 ziliokotwa ufukwe wa Coco na nyingine 6 ziliokotwa mto Ruvu kwa pamoja zikiwa zimefungwa kwenye sandarusi, na baadhi zikivuja damu.

16. Aliharibu mahusiano ya kidiplomasia na mataifa mengi ukimwenguni. Serikali yake ilichoma vifaranga vya kuku kutoka Kenya na kutaifisha ng'ombe waliovuka mpaka kuja Tanzania.

17. Alisababisha wanasiasa wa Tanzania wakimbie nchi na kuishi uhamisho kama wakimbizi wa kisiasa wakiwemo Ansbert Ngurumo, Tundu Lissu na Godbless Lema.

18. Alitumia mabavu kulazimisha ushindi kwenye uchaguzi wa 2020 na kuhakikisha CCM inashinda majimbo yote. Alipora ushindi wa upinzani kwenye majimbo mengi kwa mtutu wa bunduki.

19. Alitumia sheria ya uhujumu uchumi kutesa wapinzani wake kisiasa na wafanyabiashara aliokua na kisasi kwa mfano Rugemala na Lema wa Elerai Construction.

20. Alipenda kuabudiwa, kutukuzwa na kuogopwa. Wote waliomnyenyekea aliwapa vyeo.

21. Aliamini mawazo yake ndio sahihi na hakutaka kushauriwa kwenye jambo lolote. Aliwahi kusema yeye hapangiwi cha kufanya.

22. Alipenda kuonekana mcha Mungu japo kiuhalisia ni dikteta katili aliyetisha. Alimpoteza Ben Saanane baada ya kuhoji kuhusu PHD yake.

23. Alitangaza kuwa Tanzania haina corona na akataka watu wasivae barakoa wala wasikubali chanjo kutoka nje ya nchi.

24. Alipeleka miradi mingi ya maendeleo kijijini kwake Chato kama uwanja wa ndege, hospitali ya rufaa, benkiz barabara za lami na mbuga ya wanyama ambayo haikua na wanyama ikabidi kuhamisha kutoka mbuza zingine.

25. Aliingilia mihimili yote ya dola ikiwemo mahakama na bunge. Aliwazawadia vyeo vya ujaji mahakimu waliowafunga wapinzani jela.

26. Aliigeuza Tanzania kama mali yake binafsi na katika kila mradi alipenda atajwe yeye. Aliamini akiondoka hakuna atakayeweza kuendeleza yale aliyofanya.

Bunge liliwahi kupendekeza kumuongezea muda wa kutawala atakapomaliza mihula yake miwili, kumbe Mungu ana mipango yake hata hiyo miezi 4 hakumaliza ya kura alizoiba
 
Back
Top Bottom