Kwa njia za kawaida, uwezo huo hauna. Ila kiheshima, eti unao….

Kwa njia za kawaida, uwezo huo hauna. Ila kiheshima, eti unao….

Wewe mwaka huu utaugua kwa chuki zako kwa mh Rais. Najuwa kinachokutesa sana ni chuki zako binafsi kwa mh Rais,ukabila uliokujaa akilini mwako na ukipofu wako wa akili na mawazo ambao umekufanya ugote na kufika mwisho katika kufikiri.wewe ni wale mliokuwa hamtaki Rais wetu awe Rais.wewe ni wale mliooedelea kukesha usiku na mchana kutaka kuona Rais wetu anashindwa kuongoza Taifa letu.wewe ni wale mliokuwa mkiomba dua mbaya kwa Rais wetu ili asifanikiwe katika mpango wa aina yoyote ile wa kiuchumi na kimaendeleo kwa Taifa letu.

Sasa baada ya kuona mmeshindwa katika Dua zenu zote,baada ya kuona Rais samia anaendelea kukubalika na kupendwa na watanzania,kukubalika nje ya nchi,kutambulika mchango wake kimataifa katika ustawi wa Taifa letu na kuifanya Tanzania kuwa kimbilio la wengi,baada ya kueleweka na kupongezwa na jumuiya za kimataifa kutokana na utawala bora wenye kuheshimu haki za binadamu na kuzingatia haki na usawa katika kuendesha nchi yetu mmebakia mnaumia sana,mnateseka sana na hamuelewi mfanye nini ,maana mnaona Rais samia akiendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania na kuendelea kupata heshima na uungwaji mkono kutoka kila kona ya dunia.

Kaeni tu kwa kutulia maana Rais samia ni mpango wa Mungu na ameimulika na Mungu na siyo na mkono wa mwanadamu na hivyo hawezi kushushwa na mwanadamu aina yako mwemye chuki binafsi na ubaguzi wa kijinga.watanzania Tupo bega kwa bega na Rais wetu na tunaendelea kumuunga mkono usiku na mchana,maana kupitia yeye tumepata matumaini ya kila mtu kutimiza ndoto zake.

Watanzania tunajionea kwa macho yetu namna uchumi wetu unavyokua kwa kasi na namna kila mmoja wetu anavyoguswa na ukuaji huo wa uchumi, tunashuhudia namna huduma za kijamii zinavyoboreshwa na kusogezwa jirani ya watanzania.

Wenye akili wametambua uwezo wa Rais samia na mchango wake katika ustawi wa watu,sasa wewe na umbumbumbu wako ni nani ubishane na wenye akili? Una akili gani hapo ulipo? Kipi ulichokifanya kwa Taifa letu cha kumzidi Rais wetu? Zaidi ya kupiga soko lako la kibaguzi ni nini cha mafanikio chenye kugusa maisha ya watu ulichokifanya na unachoweza kukionyesha kwa watanzania?

Tuondolee mikosi na nuksi zako hapa.Tuachie Rais wetu na uwe na adabu kwa Rais wetu.wewe endelea kuhangaika huko huko nje ya nchi wakati sisi tunaendelea kulijenga Taifa letu kwa mikono yetu kwa kushirikiana na Rais wetu aliye mstari wa mbele katika kulitumikia Taifa letu kwa uzalendo uliotukuka.
 
Wanapewa kwa sababu wanaowapa wanajipendekeza tu, huyo bimdashi ana mchango mkubwa? Upi?
Kwa hiyo India inajipendekeza Kwa Samia 🤣🤣

Ona kubwa jinga hili ,wivu unakufanya ukose akili
download.jpg
 
Naona kama vile kuna watu hapa nchini waonao mtu kupewa ule udaktati wa heshima ni sawa na ule wa kuusomea.

Ukweli ni kwamba, si sawa hata kidogo.

Juzi hapa Rais wenu kapewa tena udaktari wa heshima huko India.

Tayari sasa katika utambulisho wake, watu wameshaanza kumwita eti Dr. Samia Suluhu Hassan.

Naye kwa kupenda ujiko, hata hagomi kuitwa hivyo.

Yupo tu anachekelea na kufurahia.

Now let’s face it. Katika hali ya kawaida, Samia hana uwezo wa kusoma na kufaulu mpaka kiwango cha PhD.

Kuna watu unaona kabisa huyu ana uwezo huo. Mfano Julius Nyerere au Benjamin Mkapa.

Hao ukiwasikiliza tu hata vile waongeavyo kuhusu mada mbali mbali, unauona kabisa uwezo wao.

Ni watu ambao wamewahi kuandika makala zilizochapishwa na magazeti na majarida mbali mbali duniani. Ni watu ambao wameshaahiriki kwenye mijadala mikubwa ya kimataifa na kutoa, kujenga, na kutetea hoja zao kwa umahiri mkubwa sana huku wakiwa na ‘command ya facts’ isiyo na mashaka.

Hao hata wakipewa udaktari wa heshima, mtu unaona kweli wanastahili maana hata wangeamua kupitia mkondo wa elimu, huo udaktari wangeupata tu.

Ila huyu tuliyenaye sasa, hana uwezo wa kupitia mkondo wa elimu na kuipata Phd.

Huo udaktari wake wa kupewa, unatokana na yeye kubahatika tu kuwa Rais.

Hana uwezo wa kuwa PhD wa ukweli…..
Mr. Ngabu,

hii ni dalili ya inferiority or seniority complex, ni conflict! Hivi Lula alikuwa mbeba mabox kama wewe, ulimsikia lini anaenda kutafuta degree ili aongoze nchi; typical Africa; kila kitu kudanganya danganya hamna viongozi wenye kujiamini. These are Banana republics; mie nashangaa sana kwa nini umejisumbua kuandika hayo yote!
 
Wanasiasa wengi wa bongolala uwezo wao kitaaluma ni tia maji tia maji, hivyo wanashoboka kuitwa madaktari wakati madaktari original hatuna hata wenge la kuitwa hivyo.
 
Kwa hali ya Kisiasa tuliyonayo pamoja na machawa tuliowazalisha usishangae wewe mwenyewe ukibahatika kuwa Raisi wa Tanzania ukapewa huo u-Dr, na ukafurahia mwenyewe kuitwa Dr Nyani Ngabu

Kama Mbunge Msukuma amepata udaktari wa heshima kwa kuwaongoza Wananchi wa jimbo moja tu, iwe ajabu kwa Samia anayeongoza Watanzania milioni 60?
PhD naijua vizuri sana kabla hata sijazaliwa.

Sidhani kama kuna mtu anayeweza kunieleza jambo nisilolijua kuhusu PhD.

PhD za ukweli lakini. Siyo hizo feki.
 
Naomba unipe exceptional achievement ya Dr. Musukuma na bimdashi...manake naona mmeamua kuzigawa kama njugu tu!!
Musukuma alipewa na nani? Na Chuo gani chenye heshima kubwa Duniani?

Hapa tuko Kwa case ya Samia ukitaka hizo exceptiona achievements za Samia ziko kibao na nyingine nimesema hapo Juu.
 
Naona kama vile kuna watu hapa nchini waonao mtu kupewa ule udaktati wa heshima ni sawa na ule wa kuusomea.

Ukweli ni kwamba, si sawa hata kidogo.

Juzi hapa Rais wenu kapewa tena udaktari wa heshima huko India.

Tayari sasa katika utambulisho wake, watu wameshaanza kumwita eti Dr. Samia Suluhu Hassan.

Naye kwa kupenda ujiko, hata hagomi kuitwa hivyo.

Yupo tu anachekelea na kufurahia.

Now let’s face it. Katika hali ya kawaida, Samia hana uwezo wa kusoma na kufaulu mpaka kiwango cha PhD.

Kuna watu unaona kabisa huyu ana uwezo huo. Mfano Julius Nyerere au Benjamin Mkapa.

Hao ukiwasikiliza tu hata vile waongeavyo kuhusu mada mbali mbali, unauona kabisa uwezo wao.

Ni watu ambao wamewahi kuandika makala zilizochapishwa na magazeti na majarida mbali mbali duniani. Ni watu ambao wameshaahiriki kwenye mijadala mikubwa ya kimataifa na kutoa, kujenga, na kutetea hoja zao kwa umahiri mkubwa sana huku wakiwa na ‘command ya facts’ isiyo na mashaka.

Hao hata wakipewa udaktari wa heshima, mtu unaona kweli wanastahili maana hata wangeamua kupitia mkondo wa elimu, huo udaktari wangeupata tu.

Ila huyu tuliyenaye sasa, hana uwezo wa kupitia mkondo wa elimu na kuipata Phd.

Huo udaktari wake wa kupewa, unatokana na yeye kubahatika tu kuwa Rais.

Hana uwezo wa kuwa PhD wa ukweli…..
We unaumia sana inakuuma, Acha ujinga, hayo ni mawazo ya kiwaki
 
Kuna yule Mama sijui ni Mbunge wa Iringa nadhani.
Ni PhD holder kwa kusoma ila huwa hajiiti Dr..alipoulizwa kwanini hapendi kuitwa hivyo alisema kitu ukiwa nacho na kikiwa chako unakuwa hata huna mbwembwe nacho maana tayari ni chako.
ila kitu kama siyo chako sasa 😁
mbwembwe,ngekewa, yaani tafranj tupu.

anyway.

lakini Rais hajawaomba wamwite Dr.
 
Samia yeye hataki imra (maneno matamu yasiokua na uhalisia) yeye kaamua kutoongeaongea na kutekeleza.

Malanyingi mtu anaependa kuongea saana na maneno matamu mbele za watu mtu huyo ni mtu wa sifa na mafanikio kidogo kwasababu mtu anaeongea sana sio mtu mwenye bidii kwenye kazi yake.
Mtu asiependa kuongea saana ni mtu wa kazi na malanyingi huyo ni mtu wa kufanikiwa sana kwenye kazi zake.

Hivyo wanaomtunuku udakitali sio wajinga wanaangalia kazi zake.
Unataka kusema Samia ni mtu wa bidii na mafanikio katika kazi kuliko Julius Nyerere na Benjamin Mkapa?
Tukiwalinganisha kwa muktadha ya nafasi ya uraisi wa nchi?

Acheni mizaha tumieni akili kidogo mnapotoa michango mitandaoni.
 
Back
Top Bottom