Uchaguzi 2020 Kwa press hii, Polepole anakivuruga chama, atafutwe mtu mwingine wa kufanya press

Ila na wewe hapo umechemsa lema msingwa wasinge weza kununulika kirahisi hivyo upinzani ni imani na ndio maana aliondoka slaa lakini cdm bado IPO hai Joshua nasari alijifanya mwamba wako wapi na ninazani huko waliko wanajuta sana kwa uamuzi wao na lisu akichukua nchi ndio itakuwa shida kwao
 
Pole pole sio mwanasiasa kama Nape ndio maana tunamuona kapwaya.
Polepole amejikita kwenye facts.
Halafu ukiangalia ana Masters ya Development studies basi burudaaaaaniiii
Toka lini siasa ikahitaji Facts, maana Mimi sionagi hzo Facts maana Nape alihudumu kipindi chenye Uhuru mwingi Sasa huyu polepole kaachiwa uwanja lakini bado kapoa flani hivi
 
Huyo Polepole, Bashiru ndiyo wanaoleta matatizo kama hayo ya kuiba forms za wapinzani, kuengua wapinzani kwa uonevu na mengine mengi. Itafika siku yao soon.


Hayo ndio mambo yamefanya wananchi kuwachukia sana ...ikiwamo na jambo la kununua wapinzani na kuwapa nafasi imekuwa kama kuwatukana wananchi.

Lakini ufisadi ..na wizi anaofanya magufuli kupita kampuni zake ni wizi mkubwa haujawahi kutokea tangu uhuuru, kupora wanmanchi pesa cash kupitia DPP. Watu wameporwa pesa DPP Maganga hakupeleka bank.

Ardhi imeporwa huko Kagera heka 30,0000 amejenga nyumba yake na ranchi
 
Mwaka huu CCM original Wanaunga Mkono CHADEMA huku bara ...na Kule Zanzibar wanaunga mkono ACT ..Kuna clip zinatembea mikutano hadi ya chadema na act wana ccm wanaonekana tena wengine wamefunika nyuso
 
Sasa Kama Polepole anaiharibia CCM si ndio vizuri kwa upinzani, Kimsingi Sasa hivi kila Lissu akiongopa, CCM hawasubiri aendelee kupotosha sasa inamfanya Lissu aonekane Mwongo....
usiri = ufisadi
 
Kaniacha hoi kutetea 20,000 ya vitambulisho vya machinga wakati Raisi mwenyewe kaomba poo kasema si lazima πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Nawe hiki ulichoandika ndo nini? Usijali hizo likes unazopewa maana, kila mtu ana wafuasi wa aina yake. Umetumia neno propaganda bila kujua maana yake. Naomba unifahamishe, uwazi wa kununua ndege huwa ukoje? Ulitaka ifanyike namna gani ili iwe wazi?

Au unafuata maneno ya akina Zitto kwamba walitakiwa kutangaza tenda? Nijibu kwanza ili nikusaidie jinsi ya kuwaza. Rais mwingine unayeamini ataliua shirika la ndege, hiyo ni miujiza ya Lissu kuwa rais.

Mradi wa reli una kasoro ipi, wakatyi ulianza tangu awamu ya 4? Kama hadi leo hujui unavyojengwa, nani akueleweshe kwa miaka yote hiyo?
 
Polepole ni mpango wa Mungu kabisa amesaidia kwa kiasi kikubwa kukivuruga hicho chama hivyo kama ni kazi basi amefanya kwa ufanisi mkubwa kama bwana Habibu kwenye riwaya ya Mimi na Raisi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mana
Hata hoja ya Lissu kuhusu manunuzi ya ndege hawajaielewa. Lissu hoja yake sio kama bunge lilitenga bajeti ya kununua ndege au la!!! Hoja ya Lissu ni kuwa kila ndege walinunua shilingi ngapi na walilipaje?

Ni vizuri angejibu kwa kuleta bank transactions kuonesha kila ndege ilikuwa shilingi ngapi. Sasa nazidi kuamini kuwa Kuna uwezekano kukawa na kupiga hela kwenye manunuzi ya zile ndege πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Tuleteeni bank transactions kutuonesha kila ndege mlinunua shilingi ngapi???? Sio kutuambia bunge lilitenga kiasi fulani. Bunge linaweza tenga bilioni 400 kununua ndege 6 ila nyie mkanunua ndege sita kwa bilioni 180

Tuonesheni Pia mmelipa shilingi ngapi kwa kampuni ya kujenga bwawa la rufiji. Bank transactions za hayo malipo zipo wapi????

Alichofanya polepole leo ni comedy sio kujibu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kasema aliyoagizwa aseme, ccm wamrudishe Nape.
Polepole kajiabisha sana!!! Eti kila Mkoa ndo utakuwa jimbo kama kipindi cha mkoloni????πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Huyu jamaa CCM walimtoa wapi???? Yaaani ameshindwa tu kujua chadema wataunganisha mikoa kuform jimbo moja!! Sasa huo ukabila utatoka wapi????πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Huyu sio Humphrey Polepole,nadhani anafananishwa.Kiukweli jina lake halisi ni Hamfurahi Mtopolo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…