Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!

Hata kikwete na magufuli mliwasema hivyo hivyo kwa hiyo hata akija mwingine mtamsema hivyohivyo
 
CCM wana wakati mno walisahahu kwamba vizazi cha leo ni tofauti na wale wa 1977. Chadema nao mmmh.
Swala si kizazi ni mtu kuingia mkataba mbovu. Nashangaa watu kila mara wanadai kizazi. Lakini kiukweli kizazi kilichopita ndo kulikuwa na misimamo haswa. Kumbuka Bunge lilivyokuwa moto enzi hata za chama kimoja.
Wabunge bila kuogopa walisimama na kudai Tanganyika. Leo watathubutu?

Wakati Loliondo inauzwa Waandishi wa habari kama akina Katabaro, Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema, alisimamia swala na kuandika ukweli hadi akauwawa kwa mazingira ya ajabu pale ofisini kwake mitaa ya mnazi mmoja.
Leo waandishi waandishi wanaotumia digital ndo kwanza wanausifia mkataba. Waandishi wa habari wamekuwa wa kujikomba hasa wa kizazi hiki.

Kuna watu walikuwa hawamuogopi Rais, ndani ya CCM akina Munasa Sabbi Munasa, huyu alikuwa akisema nami nachukua fomu ya kugombea Urais. Hakumwogopa Nyerere.

Zamani hakukuwa na uchawa. Vijana sikuhizi wamekuwa machawa. Hata kama jambo ni la kipumbavu wanashadadia. Hiyo miaka unayoisema upumbavu huu haukuwepo.

Zamani hakukuwa na muheshimiwa, watu walitumia neno ndugu, ati siku hizi uheshimiwa ndo umewekwa mbele watu wanalambwa miguu. Upuuzi huu haukuwepo.

Hivyo acheni kupondea kizazi cha zamani ukadhani watu walikuwa wajinga. Zamani watu tulifundishwa uzalendo. Tunakimbia mchakamchaka, nyimbo za uzalendo. Kwanza zamani tuliifaidi serikali sana.
Matibabu yalikuwa bure, kusoma bure hadi vitabu na madaftari wapewa skuli. Watu wa sekondari na chuo walisafirishwa na serikali wakati wa likizo kwenda na kurudi.

Ebu acheni kuwa mnataka kudharirisha miaka ya zamani mkadhani tulikuwa wajinga. Miaka hiyo kulikuwa na park, au garden karibu kila mkoa. Siku hizi mmejenga kila sehemu, mnauza tu maeneo Dar haina hata sehemu ya kupumlia.

Ebu acheni kuona watu wa zamani kama ndo walikuwa wajinga. Nambia hiyo zamani unayoiponda ulisikia kuna mikataba ya kipumbavu kama hii inayoingiwa leo? Ha ha ha, acheni kusema miaka ya zamani ukadhani watu walikuwa wajinga. Wanaopinga hiyo mikataba leo wote ndio hao wa zamani wanao waelimisha ninyi vijana wa miaka ya 90 na 2000.
 
Amka!!!

Nchi inazo Fursa nyingi sana za KIBIASHARA kaleta huyu Rais!

Hata Wafugaji wanauza Ng'ombe Nje ya Nchi siku hizi we unaleta masikhara wewe!

NFRA wananunua Mahindi kwa 850/= kwa kilo-Unataka Rais wa kukuogesha?

Kura zikipigwa kesho asubuhi Rais Samia ana 80%

Hapo bado Uchumi haujafunguka...mpk ifike 2025 hakutakuwa na haja ya Kampeni.

Tatizo moja watu ni Wavivu sana!!!

Pale KIA ndege zinapishana kutoka Ulaya...Royal Tour-Acha kabisa!!

Halafu siku hizi watalii ni Celebrities...

Andika kitu kama hiki mwakani mwezi kama huu!!

Utabadili mtizamo wako!


Tufanye kazi!!!
 
Hayo mabango ni akina nape na akina mwigulu waliyaweka ili kuweza kumfunika mtangulizi wake. .lakin ndo kwwnza amekuwa kituko
 
Hiyo asilimia 80 tutaziona kwenye uchaguz wa serikali za mitaa
 
...You have solemnly swore to tell the truth, the whole truth, and nothing but the truth, and you will keep secret all of the proceedings of the grand jury conducted in your presence? So help you God.
 
Shukrani kwa kutoa hoja yenye kina kirefu.

Nadhami uzalendo nchini umeanza kupungua baada ya kuingia kwenye siasa za mfumo wa vyama vingi na uchumi wa soko huria. Kwa sasa pesa zinatangulia katika uongozi
 
Tuna jamii mfu ambayo haiwezi kuhoji kwa sauti inayosikia yaani bora liende ama fuata mkumbo
 
Mkuu, maelezo marefu halafu unahitimisha kwa kuwashutumu wananchi kuwa ni wavivu kama vile huwa unawalisha!

Hoja zako zimebeba fikra za tabaka aali katika jamii (elitist mentality). Ninyi ndio mnaowaona machinga ni wavivu na wachafu na kwa mantiki hiyo hawapaswi kuonekana katika miji na majiji.

Fursa ulidhorodhesha unadhani ni mpya wakati hata kabla ya uhuru zilikuwepo. kwani NFRA imeanzishwa na Rais Samia? Kwani lini mifugo ilikuwa haiuzwi nchi za nje?

Acha kuandika vichekesho!
 
Mkuu msemaji ukweli upo? Habari ya siku nyingi?

Samia sifa ya kua kiongozi hata wa nyumba 10 hana, lakini ajabu ndie rais wa Tanzania. Inawezekana kabisa huko sayari nyingine za Aliens wakitaka vituko ama vichekesho hua wanaangalia Tanzania.

Samia hana authoritative speech, hana commanding speach, hana convincing speech, hana chochote, hana.

Juzi akiwa kwao Zanzibar anasema mungu kampa mtihani mgumu sana hata hajui afanyeje, halafu anataka tena agombee 2025, unajiuliza kwani kalazimishwa, si aache ama ajiuzuru.

Rais Samia speech zake zimejaa maneno kama mkalitizame na hili, mkaliangalie na hili, hili pia litizamwe, hili liangaliwe, hili likafanyiwe kazi, hili lifikirieni. Unajiuliza anawaambia kina nani?

Nchi ina safari ndefu sana.
 
Kwa mara ya kwanza Tangu nikufahamu umeandika jambo la kweli , Hongera sana .
Nilisha msahau huyu kuwa aliwahi kuwepo hapa na zile makala zake za ajabu ajabu!

Sijui alipotelea wapi, na leo kaibuka na sura mpya kabisa!
 

Hata kama rais huyu achokwe vipi, bado hakuna namna ya kumtoa madarakani kwa njia ya kura, labda machafuko au mapinduzi. Tuna katiba inayokibeba chama tawala, na inampa nguvu rais aliyeko madarakani kuamua kiwango cha ushindi akitakacho. Hili lilidhibita wazi wazi chini ya utawala wa Magufuli.

Kwa hiyo rais huyu yupo madarakani hadi amalize vipindi vyake bila kujali matokeo ya kura. Magufuli ameotesha mbegu mbaya sana ya kutoheshimu chaguzi zetu, na hakuna kiongozi yoyote wa CCM atakayeacha kutumia mbinu zile chafu. Sana sana wapiga kura hawatajitokeza kwa wingi kupiga kura, na kuna uwezekano wa chama tawala kuamua idadi ya kura za kupika.
 
Karibu mtetezi wa mafisadi na uporaji wa bandari zote za Tanganyika
 
Mimi ni CCM lakini siwezi kumpa Mama kura yangu! HATOSHI!
Hahitaji kura yako, wala hategemei kura ya mtu yoyote kukaa madarakani. Vyombo vya dola na tume isiyo huru ya uchaguzi zinatosha kufanya kazi hiyo ya kumpatia kura. Huu ni ukweli mchungu boss wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…