Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!

HATOGOMBEA!!!
Sasa mapicha mitaani ni ya nini?
Na hawa "waandishi maalum", na "MACHAWA" ni wa kazi gani?

Ujue wote hawa ni makupe na chawa hasa hasa, ni lazima yanyonye damu kwa gharama kubwa.

Mama anahaha, anahangaika kutafuta pesa ya kumrudisha madarakani kwa kila njia iwezekanayo.

Njia pekee ya kumzuia, ni huko huko CCM, paibuke kundi la vichaa wasiopenda ujuha wa chama chao kinaoufanya kila mwaka wa uchaguzi.
Hilo pekee ndilo linaloweza kuwa kikwazo kwa Samia kutogombea., au hata akilazimisha kugombea anasindwa uchaguzi na hawezi kuiba kura kama ilivyozoeleka.
 
Samia hafai kabisa, hayupo yeyote anayejielewa anamuamini tena, ameshapoteza uaminifu kwa wale anaowaongoza, sasa anajiendea tu ilimradi..

Naamini ni JK na kundi lao ndio wanaonuona anafaa kuendelea kukalia kile kiti, lakini nje ya pale, hakuna mwingine yeyote mwenye imani nae.
 
Mi sikutaka hata kujibu hizo takataka zao. Wamekusanyana wenyewe na kujibizana wenyewe kimada chao hiki eti wanawavisha watanzania! Miongo na minafiki hii dadadeki!!! ahsante kwa kuwasaidia.

Ukweli ni kuwa majuha haya a.k.a nyumbu hizi a.k.a haters hawa wamekwama na wanamuogopa Mama Samia, The Mother of Modern Tanzania, kuliko maelezo......si kwa sababu ni mkali bali kwa mipango ya kimapinduzi ya kimaendeleo mikubwa kabisa inayoenda kutokea nchi hii tangu ipate uhuru. Wanahofu na hawapendi kwelikweli kwa sababu zao za kiubaguzi, kikanda, wivu tu, kijinsi na pengine kidini. Kadiri mambo yanavyosonga mbele kwa kasi ndivyo wanavyozidi kuchanganyikiwa. Katika kujidariji na kuchanganyikiwa huko ndo 'wamebuni' huu mtindo wa kuja na vithread vyao vya kijingajinga kila dakika.

Ukwdli ni kuwa WATANZANIA HALISI HUKU MITAANI TUPO PAMOJA MNO NA MAMA YETU....TENA SAANA. Hivi vijitu 15-20 vya humu jf vinavyojivika kofia ya watanzania wote ni vya kuvipuuza tu.
 
Rais Samia kwa sasa hakubaliki nchini lakini kibaya zaidi hakubaliki ndani ya kundi kubwa la watu wenye maisha ya chini ambao ni wengi nchini na hutumiwa kama β€œkete” ya CCM katika chaguzi.
Huku kitaa watu wakijani wenye matumbo makubwa tena wengine ni wateule wake wanamnanga vibaya
 
Wewe endelea na β€œuchawa” wa kijinga!

Uliza wakongwe wa Jamiiforums watakuambia mimi ni nani!

Mimi nimekuwa ndani ya CCM na serikali kabla hujazaliwa achilia mbali kuijua Jamiiforums mwaka 2022.
Kama ni hivyo basi ni bora walivyokutema, kwa hoja hii uliyoleta hapa ni dhahiri kuwa si kwamba hutoshi tu lakini pia hujielewi.....samahani lkn maana umesema we ni mkongwe.
Halafu, wakongwe wenyewe wa kuwauliza humu si ndo hao hao walio'like' na kussuport mada yako; yaani kina erythrocyte & co? Ndo tuwaulize hao na unataka utuambie kuwa uko serious?!!!!🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Wewe ni zwazwa!
 
Siku Ya Kufa Nyani, Miti Yote Huteleza
Kwasasa Wameanza Kujitafakari Mmoja Mmoja Wameshapata Yupi Atolewe Bangusiro (Kondoo Wa Kafara)
 
Umesema ukweli kabisa.Mimi nimetembea sehemu nyingi Tanzania nzima,vijiji na vijiji kote huko kila mmoja hawamkubali kabisa huyu mother.
 
Samia hafai kuwa Rais. Katiba iboreshwe isije kutokea tena upuuzi wa namna hii
Hata uje Katiba kutoka wapi au Tume huru kutoka sayari ipo bado mamilioni ya watanzania tutamchagua Rais Samia.Ndio maana tumeamua kuwa naye mpaka 2030,hutaki hama nchi na familia yako maana sisi watanzania chaguo letu ni Rais samia
 
Atakuwa anazuga ili mumchague muhula wa pili auze kila kitu. Hata apige magoti aombe msamaha hachaguliwi kabisa. Labda aibe na afanikiwe kuwashawishi majeshi wamweke kwa lazima.
Sauti za mamilioni ya watanzania zimeshapaza sauti kuhitaji utumishi wa mama samia kutuongoza muhula wa pili,kwa hiyo utake usitake,upende usipende watanzania tumeshaamua kwenda na kumchagua Tena Rais samia,jua liwake au mvua inyeshe tutakwenda na Rais samia na ndiye Rais ajaye kwa mara nyingine Tena.kama hutaki tafuta nchi yako uende na watoto wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…