Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!

Wewe ni chawa tu unataka uendelee kumnyonya damu Mama Samia hutaki kumweleza ukweli. Mimi kazi zangu ni vijijini ni ukweli maeneo mengi ninayopita hawamkubali sana
 
Kitu ambacho hua nasikitika kwa Mh Rais wetu ni kama hana anachosimamia tofauti na Marais waliopita...
Mfano JK - Hari mpya, Nguvu Mpya, wimbo ukawa kilimo kwanza
Magufuli - Hapa kazi tuu, wimbo ukawa viwanda...
Lakini kwa Rais wetu saiv kila kitu anagusagusa tuu, Leo tutaamka na kilimo, kesho viwanda kesho kutwa mambo mengine...
 
Naunga mkono hoja . Hakubaliki kabisa. Wananchi wanasema havutii hata kwenye hotuba zake. Ukimuangalia vizuri hata yeye amejua sikubaliki ila anachofanya ni watajua wenyewe Wacha Nile maisha tu.

CCM wana hali mbaya sana!
 
Mama anakipeleka chama kubaya Kama JK 2010, namwangalia Kinana anavyoongea kama amekata tamaa Ila hana jinsi ndio ameachiwa jukumu hilo huku mwenyekiti wake akienda kubarizi Dubai na Saudia
 
Nimefurahishwa na andiko lako yote uliyogusia ni ukweli mtupu, je unadhani anayo nafasi ya kubadili mihemko ya Wananchi kabla hatujafika kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025?

Anatakiwa awe mtumishi wa watanzania wote na sio kikundi fulani cha watu.

Tatizo lililopo ni kuwa hana karama, kipaji na ujuzi wa uongozi!
 
Dah...mwana Magufuli mwenzangu tuliepigwa na kitu kizito kichwani,nimefarijika kuona bandiko lako tena hapa jukwaani.

Ila alieleta siasa duniani hususani huku kwetu afrika alaaniwe.

Mkuu, nipo ila majukumu mengine hayakunipa nafasi ya kuingia mara kwa mara hapa jukwaani.

Tuendelee kulijenga taifa letu.
 
Kwa mara ya kwanza Tangu nikufahamu umeandika jambo la kweli , Hongera sana .
Mimi nashangaa CCM wanamng'ang'ania, wanabeba udhaifu wake,
Miiko ya CCM ni
1: Nitasema Kweli Daima
2: Rushwa ni Adui
3: sisi sote ni Ndugu.....
4........

Wanapo anza kuongea uongo mmmmmm, nashangaa sana
 
Zile kauli zake za ‘na hili mkaliangalie’ ‘na hili mkalitazame’, zinamuonyeshaga kuwa nchi kawaachia watu fulani, yeye ni incompetent. Na huwa hazina ufatiliaji. Akiongea hapo kamaliza. Sad. Sikutegemea awe hivi.

Mimi imenichukua miezi mitano kujua kama “tumepigwa”.

She’s incompetence to the core!
 
Bora umesema ukweli bila kupindisha.Kamwe siwezi kuchagua mwanamke kama rais wa kuongoza Tz
 
Natamani jamii forum wangeruhusu kudownload uzi ili huu niupitie kila muda kuikumbusha akili yangu kuwa taifa limepata kiongozi wa hovyo kuwahi kutokea
 
Tena hata hizo ziara wana ccm wenyewe wanasonya tu, eti wanawaita kwa kuwa beba kwa magari Kisha wanawashindisha njaa uwanja I.. Hoja za kutetea mkataba hazina mashiko, kwetu huku wamerudi wajumbe wamashina wanasema wamelikoroga wanywe wenyewe, sie hatuthubutu kutetea ujinga... Tulale njaa tutete matumbo yao😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…