MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
- Thread starter
- #161
Karibu mkuu ulipotea sana.
Mkuu nipo sana. Majukumu yalikuwa mengi.
Shukrani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Karibu mkuu ulipotea sana.
Alisema ,"Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu,si ndio Ndugu zangu?".
Wewe ni chawa tu unataka uendelee kumnyonya damu Mama Samia hutaki kumweleza ukweli. Mimi kazi zangu ni vijijini ni ukweli maeneo mengi ninayopita hawamkubali sanaAcha uongo wako hapa na upotoshaji wako hapa wa kijinga.
Rais samia anakubalika ,kupendwa na kuungwa mkono na watanzania wa makundi yote kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ndani ya muda mfupi wa uongozi wake.
Katika kugusa maisha ya wananchi wa kipato cha chini ambao wengi wao ni wakulima ,Rais samia aliamua kuchukua hatua za makusudi na za kijasiri kwa kuhakikisha kuwa anawapatia mbolea za Ruzuku zinazogharimu Takribani Billion mia moja hamsini ,hali iliyopelekea mbolea kushuka bei sokoni,,mfano mbolea ya DAP iliyokuwa ikiuzwa laki na 40 ikaanza kupatikana kwa Elfu 70 tu,.sasa ni mkulima yupi au mwananchi yupi atakaye shindwa kumshukuru Rais samia hasa kwa kuzingatia asilimia kubwa ni wakulima? Alifanya hivi kwa kutambua ukweli kuwa uchumi mzuri ni ule unaowagusa watu wengi ,na hapa Tanzania ili uwaguse watu wengi nisharti uwekeze katika shughuli za kilimo kama alivyofanya rais samia ,ikiwepo kuongeza bajeti kufikia billion 970.
Ukija kwa vijana nako ni kicheko furaha na Tabasamu ,hasa baada ya kumwaga maelfu ya ajira mitaani katika ndani ya muda mfupi,lakini pia miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikijengwa hapa nchini imechochea ajira nyingi sana kupatikana kwa vijana,lakini pia kwa vijana wanaomaliza kidato cha sita wanapewa mikopo bila shida ,na wawapo vyuoni ni raha tupu na Tabasamu hasa baada ya kuongeza fedha ya kujikimu kufikia elfu kumi kwa siku.
Ukienda kwa wafanyabishara nako ni matumaini kibao ,ambapo kwa sasa kila mfanyabiashara anajisikia fahari kufanyia biashara hapa nchini,kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya biashara hapa nchini,sasa wafanyabishara wanakadiriwa mapato kwa haki na palipo na dosari milango ipo wazi kwa mazungumzo,hali hii ndio imepelekea mapato kwa mwezi kupanda kufikia Trioni 2. Wafanyabishara kwa sasa wanajiona huru kuweka fedha zao benki bila wasiwasi wa kuchotewa fedha zao bila utaratibu wa kisheria au kibenki.
Ukija kwa watumishi wa umma unakuta nako ni shangwe ,nderemo na vifijo hasa baada ya mama wa shoka kuwapandishia mishahara kwa 23% hasa wa kima cha chini,kuwapandisha madaraja,kuwapa nyongeza ya mishahara ya kila mwaka,kuwalipa malimbikizo ya madeni yao na maboresho mengine mengi tu.
Sasa ukitaka kufungua hata biashara katika mwaka wako wa kwanza husumbuliwi na ulipaji wa mapato,kwa kuwa serikali imetoa nafasi ya kukuwa kimtaji na kupata uzoefu wa biashara na kusimama kibiashara.
Ukienda katika huduma za kijamii unakuta Rais samia amegusa kila eneo na kila mahali,iwe ni katika miradi ya maji au umeme au miundombinu una ona namna alivyowekeza vya kutosha ,ndio maana imefika hatua bwawa la nyerere linaanza mapema mwakani kuzalisha umeme.
Ni kundi lipi ambalo halijaguswa na utendaji wa Rais samia? Lipi ambalo halijafikiwa? Lipi ambalo halijatazamwa?
Masuala ya Tozo, je nchi gani ya ulaya au Marekani au zilizoendelea zilizopata maendeleo yake kwa kushushwa kutoka angani? Ni wapi ambako watu wake hawakujibana bana kulipa Tozo ili wajenge nchi zao? Ni wapi huko ambako mataifa yao na wananchi wao walikaa na kubweteka kusubiri wenzao kutoka mataifa mengine walipe Tozo na kodi ili wao wapewe maendeleo.
Watanzania hawajawahi kupinga Tozo na wakati wote wameunga mpango huo wa serikali,ndio maana walikuwa Tayari kuijenga nchi yetu kwa mikono yao ,maana waliona ni aibu kusubiri misaada kwa ajili ya kujengea matundu ya vyoo vya wanafunzi wetu mashuleni. Matokeo chanya ya Tozo hizo ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya Elfu ishirini nchini kwote yaliyopelekea wanafunzi wote wanaofaulu kuanza masomo kwa wakati mmoja, utolewaji wa Elimu bure hadi kidato cha sita,Ujenzi wa vituo vya Afya kila kona ya nchi ikiwepo 234 miezi michache iliyopita ,utolewaji wa Ruzuku ya billion mia moja kila mwezi katika mafuta wakati wa mfumuko wa bei ya mafuta Duniani uliokuwa umesababishwa na vita vya ukrein, n.k.
Mambo aliyoyafanya Rais samia huwezi kumaliza kuandika hapa maana ni mengi sana ,hapo sijazungumzia namna alivyokuza uchumi wetu na kupelekea mzunguko mzuri wa fedha mitaani,kukuza na kuimarisha Demokrasia n.k
Naunga mkono hoja . Hakubaliki kabisa. Wananchi wanasema havutii hata kwenye hotuba zake. Ukimuangalia vizuri hata yeye amejua sikubaliki ila anachofanya ni watajua wenyewe Wacha Nile maisha tu.
This time itakuwa tofauti mkuu, watu wako radhi walale nje ya vyumba vya masanduku😄😄Kwani CCM kuiba kura wameacha?
Nimefurahishwa na andiko lako yote uliyogusia ni ukweli mtupu, je unadhani anayo nafasi ya kubadili mihemko ya Wananchi kabla hatujafika kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025?
Dah...mwana Magufuli mwenzangu tuliepigwa na kitu kizito kichwani,nimefarijika kuona bandiko lako tena hapa jukwaani.
Ila alieleta siasa duniani hususani huku kwetu afrika alaaniwe.
Mimi nashangaa CCM wanamng'ang'ania, wanabeba udhaifu wake,Kwa mara ya kwanza Tangu nikufahamu umeandika jambo la kweli , Hongera sana .
Zile kauli zake za ‘na hili mkaliangalie’ ‘na hili mkalitazame’, zinamuonyeshaga kuwa nchi kawaachia watu fulani, yeye ni incompetent. Na huwa hazina ufatiliaji. Akiongea hapo kamaliza. Sad. Sikutegemea awe hivi.
Bora umesema ukweli bila kupindisha.Kamwe siwezi kuchagua mwanamke kama rais wa kuongoza TzMh.SAMIA hata atangazwe kila sekunde hawezi kukubalika,hata afanye mazuri 1000 hawezi kukubalika na sabubu ni 2 tu
1.Wenye Tanzania ni Watanganyika na sio Wazanzibari-na Watanganyika hawapendi kutawaliwa na Wazanzibar wachache.
2.pia sababu ni Mwanamke,hamna Mwanaume wa Kiafrika anaweza kumchagua Mwanamke amuongoze na hamna Mwanamke wa Kiafrika anataka aongozwe na Mwanamke mwezake.
Binafsi yangu Mwaamke hata awe na uwezo kama wa Margaret Thatcher siwezi kimchagua aniongoze.
Natusua tuShoga anaweza mshughulikia nani?
Na ikawe hivyo mkuu.This time itakuwa tofauti mkuu, watu wako radhi walale nje ya vyumba vya masanduku
Mama baada ya kumsliza kuiuza nchi, atakimbilia uarabuni na tayari ana geto lake kule.
Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
UnatusuliwaNatusua tu
Nakumenya tuUnatusuliwa
Tena hata hizo ziara wana ccm wenyewe wanasonya tu, eti wanawaita kwa kuwa beba kwa magari Kisha wanawashindisha njaa uwanja I.. Hoja za kutetea mkataba hazina mashiko, kwetu huku wamerudi wajumbe wamashina wanasema wamelikoroga wanywe wenyewe, sie hatuthubutu kutetea ujinga... Tulale njaa tutete matumbo yao😂😂😂Ilinichukua miezi mitano kufahamu kuwa Rais Samia hana maisha marefu ya kisiasa kwa sababu hana karama, kipaji na ujuzi wa uongozi.
Unaweza kuukataa ukweli lakini hata kama ukiukataa hakuwezi kuubadilisha kuwa uongo.
Mwl. Nyerere aliwahi kusema, “Ukweli una tabia moja nzuri sana, haujali mkubwa wala mdogo, hujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kupiga teke jiwe kwa kuwa unafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi kupuuzwapuuzwa”.
Rais Samia kwa sasa hakubaliki nchini lakini kibaya zaidi hakubaliki ndani ya kundi kubwa la watu wenye maisha ya chini ambao ni wengi nchini na hutumiwa kama “kete” ya CCM katika chaguzi.
Rais Samia amebandika mabango ya kujitangaza nchi nzima lakini kinyume chake watu wakiyaona wanaanza kuyatukana!
Sakata la kuwapa DP-World bandari zetu limekuwa ndio msumari wa mwisho katika kaburi lake la kisiasa baada ya kuwabambikia wananchi tozo mbalimbali.
Ndani ya CCM wameanza kukubali kuwa hali ni mbaya sana mpaka wameamua kuanza ziara za “kuwatongoza” wananchi hasa wa kupato cha chini huku wakisema eti Rais hawezi “kuiuza” nchi.
Katika hali ya kutapatapa wameanza kutumia mbinu ya udini ili kugusa hisia za imani ya dini angalau kundi la watu lenye mlengo wa dini yake lianze kumuunga mkono hasa kundi la watu wa kipato cha chini ambalo halitaki hata kumsikia.
Kinachowashitua zaidi ndani ya CCM ni kuona kuwa juhudi zote za kuwaleta ndani ya utawala wake wapinzani hasa CHADEMA katika “dhana ya kujenga umoja” haijazaa matunda endelevu na badala yake wananchi wa kipato cha chini hawataki hata kumsikiliza achilia mbali kumuona.
Ukiwauliza wananchi wengi kama wanakumbukumbu ya jambo lolote ambalo Rais Samia amelifanya na hawawezi kumsahau watakuambia ni tozo na kugawa bure raslimali zetu za Taifa.
Hotuba zake husahaulika pindi anapomaliza kutoa hotuba. Nadhani hata mawaziri wake ukiwauliza baada ya hotuba yake hawawezi kukumbuka alichokisema! Garbage in, garbage out.
Mikutano yake ya barabarani kwa sasa inakuwa na magari mengi zaidi ya wananchi ukiondoa wale wanaovalishwa nguo za CCM!
Historia nchini huonyesha kuwa Rais huanza kuchokwa na kuchukiwa katika kipindi cha pili cha utawala wake lakini Rais Samia imemchukua miaka miwili tu kuchukiwa na wananchi wengi.
Kwa jinsi hali ilivyo mbaya kuna uwezekano mkubwa Rais Samia akawa ni Rais wa kipindi kimoja katika historia ya Tanzania kwa sababu katika nchi yoyote wanaoleta mabadiliko ni watu wa kipato cha chini ambao kwa sasa hawataki hata kumsikia.
Watz ni vifaa nyie[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mama baada ya kumsliza kuiuza nchi, atakimbilia uarabuni na tayari ana geto lake kule.
Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app