Pre GE2025 Kwa Respond hii ya Kariakoo, kuirudisha Serikali ya CCM madarakani itabidi tujitafakari

Pre GE2025 Kwa Respond hii ya Kariakoo, kuirudisha Serikali ya CCM madarakani itabidi tujitafakari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Msiba wa Mafuru ulikuwa muhimu kuliko msiba wa Kariakoo.

Saa100 agekuwa anatumia usarifi wa helicopter,ningetuma sadaka.
 
Wewe kama kiongozi awamu ya 6, hujisikii vibaya, bibi kupaa na pipa hapa Dar,anawacha mamia ya watanganyika chini ya vifusi wakiomba msaada wa kupatia oxygen?
Ulitaka aende akasaidie kutoa vifusi?. Hujamuona Waziri Lukuvi pale kwenye eneo la tukio?.

Majanga hayana muda maalum ni sawa na siku ya kifo huwa haijulikani.
 
Ina maana Jeshi la Uokoji halina vifaa vya kisasa vya uokoaji? Mbona Jeshi la Polisi lina vifaa vya kisasa vya kuthibiti ghasia?
 
Jengo limeanguka Samia akiwa angani anakaribia huko alipoenda, kabla ya kulaumu tujaribu kuangalia ulivyokuwa mtiririko wa matukio.
Angerudi kuomboleza na kuhimiza uokoaji. Yaani mwenye nyumba itokee tatizo hata ukiwa safarini si unarudi kuonyesha kujali maisha ya watu wako?
 
Angerudi kuomboleza na kuhimiza uokoaji. Yaani mwenye nyumba itokee tatizo hata ukiwa safarini si unarudi kuonyesha kujali maisha ya watu wako?
Mawaziri wake walikuwepo katika eneo la tukio, mkuu wa mkoa na Lukuvi walikuwepo. Nina uhakika angekuwepo hapa nchini ni lazima angekwenda mahali pale.
 
Mawaziri wake walikuwepo katika eneo la tukio, mkuu wa mkoa na Lukuvi walikuwepo. Nina uhakika angekuwepo hapa nchini ni lazima angekwenda mahali pale.
Uwepo wake kama Mfariji Mkuu wa Nchi ungesaidia sana hata kwa maamuzi magumu yangefanyika maana yeye ndio mwamuzi hakuna wa kumuomba ruhusa.
 
Kwani ujinga na ubovu wa serikali huonekana wapi na wakati gani?

JIBU NI: Ni response yake wakati wa kushughulikia majanga kama haya

Wether unapenda au hutaki, ukweli ni kuwa CCM na serikali yake kwenye kushughulikia uhai na ustawi wa watu sio kipaumbele chao. Kipaumbele chao ni kutetea uwepo wao madarakani na matumbo yao...

Kwa fyongo na udhaifu huu wa serikali yenu utazuiaje wapinzani wenu kisiasa kuwapiga mawe na kuwaona hamfai...???

Tukio hili la Kariokoo leo ni ushahidi wa ubovu wa CCM na hivyo serikali yao na tayari wiki ijayo zinaanza kampeni za uchaguzi wa viongozi wa vijiji, mitaa/vitongoji....

Huwezi kuzuia wapinzani wenu kuifanya hii kuwa ni ajenda na nyundo mojawapo ya kuwapondea nayo CCM wakati wa kampeni kuwa hamfai kuaminiwa tena...
Kwahiyo Chadema ikiingia madarakani ndio inaweza kuresponse haraka kwenye haya majanga?
 
Mngekuwa mnajali uhai wa binadamu mngeleta
Madawa hospitalini
Maji safi
Umeme wa uhakika
Nk
Mbona hivyo vitu havifanywi pia na Chadema lakini kwenye haranbee zakusaidia chama chao wanafanya sana kijana hakuna chama kitachokukusaidia badala yake wewe ndio utatumika kuwa ngazi yao ya kuingia madarakani
 
Kwa kweli CCM ni janga kubwa kwa Taifa. Yaani serikali ya CCM hakuna jema inayoliweza, zaidi ya uovu. MV Bukoba watu walipotea kwa uzembe. Ajali ya ndege Bukoba, uzembe mtupu. Ajali mbalimbali zinazohitaji uokozi, hakuna wakati ambapo Serikali imewahi kufanya kama inavyotakiwa. Wanachokiweza ni uovu wa kupora uchaguzi, kufanya ufisadi, kuteka na kuua watu!!
So unataka kutuambia Chadema ikiingia madarakani ndio watakuwa solution ya matatizo yetu yote?
 
Uwepo wake kama Mfariji Mkuu wa Nchi ungesaidia sana hata kwa maamuzi magumu yangefanyika maana yeye ndio mwamuzi hakuna wa kumuomba ruhusa.
Alipokwenda ni kikazi zaidi tukumbuke. Faraja aliituma jana usiku kwa njia ya video na kuahidi maziko ya wote 13 waliofariki.

Alituma mawaziri waandamizi kina Lukuvi.
 
Tukio la maafa limetokea katikati ya jiji eneo lenye watu wengi saa 3 asubuhi, lakini vyombo vyote vya uokozi vimechukua masaa kujitokeza kuokoa watu waliochini hadi Raia wasio na dhana za uokozi wanatumia mikono mitupu kuokoa watu hii ni aibu kwa serikali hii. Askari hawaonekani kama wale wa maandamano ya Chadema kwa mamia bali mmoja mmoja na kitambi chake, huu ni wendawazimu kabisa yaani kuyafanya maandamano ni ya hatari kuliko maafa kama kudondoka jengo na kufukia watu? Pengine Mungu anatuonyesha ubovu wa serikali yetu tuliyokubali iwe madarakani huku pamoja na kutupatia "UFAHAMU" bado tunashangilia "mitano tena". Kwa kweli kuipigia kura CCM tena tunastahili kupimwa akili kama ziko sawa. View attachment 3153700
Kama huna elimu ya uokoaji ni vyema ukakaa kimya maana ulichoandika ni upuuzi mtupu, vikosi vya uokoaji si kwamba vinakuwa mahali pa tukio bali vinakuwa katika maeneo tofauti na tukio pia kuna majukumu mengine pia. Lakini pia Vikosi hivyo vikishapata taarifa kuna maandalizi ikiwa ni pamoja na kupata taarifa sahihi, kuangalia ni vifaa gani stahiki wanapaswa kwenda navyo, vikosi vitakuwa na timu ngapi na ni timu ipi inatakiwa kutangulia na timu ipi itakuwa back up. Baada ya kufika eneo la tukio kabla ya kuanza kazi ya uokoaji lazima kwanza ifanyike Field Level Risk Assessment ili kuwalinda waokoaji, watu wanaozunguka eneo husika, waathirika wa tukio, pia mali zilizopo katika eneo hilo. Unapoleta mambo ya maandamano, hilo ni jambo tofauti kabisa na uokoaji.
 
Mimi akiri zangu hazipo sawa nitaipigia kura CCM Maana ndo nimeikuta na nitaicha...wewe ambaye kila kukuicha unaota kuisambaratisha CCM Endelea kuwanga mchana.
 
Kipi kisichoeleweka au we ndo wajitoa akili? “ jeshi jeshi.. “ ni kama vile watu wa kazi wameingia mambo yataenda, watu wakazi wenyewe wako mikoni mitupu wanatbea kama vile hawajui kinachoendela,

Au hilo nalo hadi taarifa rasmu ya polisi? Faq idiot
HEEEEE HEEEEEE!
Ukiwa JF hukosi kukutana na vituko!

Mkuu 'miviga', hujambo lakini?
Tukiacha hayo mengine yote ya ufafanuzi ulio toa kuonyesha umahiri wako katika uelewa wa mambo!
Naomba unifafanulie hiyo "Faq idiot" uliyo tumia hapo kunikoga ambayo mimi sina uwezo nayo, hata bila "kujitoa akili!"
 
Kama huna elimu ya uokoaji ni vyema ukakaa kimya maana ulichoandika ni upuuzi mtupu, vikosi vya uokoaji si kwamba vinakuwa mahali pa tukio bali vinakuwa katika maeneo tofauti na tukio pia kuna majukumu mengine pia. Lakini pia Vikosi hivyo vikishapata taarifa kuna maandalizi ikiwa ni pamoja na kupata taarifa sahihi, kuangalia ni vifaa gani stahiki wanapaswa kwenda navyo, vikosi vitakuwa na timu ngapi na ni timu ipi inatakiwa kutangulia na timu ipi itakuwa back up. Baada ya kufika eneo la tukio kabla ya kuanza kazi ya uokoaji lazima kwanza ifanyike Field Level Risk Assessment ili kuwalinda waokoaji, watu wanaozunguka eneo husika, waathirika wa tukio, pia mali zilizopo katika eneo hilo. Unapoleta mambo ya maandamano, hilo ni jambo tofauti kabisa na uokoaji.
Umekariri wapi hii mkuu 'mkaruka'?
Halafu nawe kwa kazi hii ya kukariri utajiita na kutaka watu wakutambue kuwa unajuwa kazi ya uokoaji wa dharura!
Hapo mezani kwako ofisini bila shaka pamejaa makabrasha yanayo eleza mengi kuhusu maswala haya, lakini hata siku moja hujawahi kwenda 'field' kuhakikisha kuwa hayo uliyo kariri ndiyo hasa uhalisia wa mambo yalivyo.

Najuwa hata ukisoma jinsi ya upasuaji wa ngiri unavyo paswa kufanyika, utakuja hapa na kutueleza vizuri sana kwamba wewe ni mbobezi katika eneo hilo! CCM inawa penda sana wataalam wa aina yenu!
 
Tukio la maafa limetokea katikati ya jiji eneo lenye watu wengi saa 3 asubuhi, lakini vyombo vyote vya uokozi vimechukua masaa kujitokeza kuokoa watu waliochini hadi Raia wasio na dhana za uokozi wanatumia mikono mitupu kuokoa watu hii ni aibu kwa serikali hii.

Askari hawaonekani kama wale wa maandamano ya Chadema kwa mamia bali mmoja mmoja na kitambi chake, huu ni wendawazimu kabisa yaani kuyafanya maandamano ni ya hatari kuliko maafa kama kudondoka jengo na kufukia watu?

Pengine Mungu anatuonyesha ubovu wa serikali yetu tuliyokubali iwe madarakani huku pamoja na kutupatia "UFAHAMU" bado tunashangilia "mitano tena".

Kwa kweli kuipigia kura CCM tena tunastahili kupimwa akili kama ziko sawa.

View attachment 3153700
Uchaguzi wa HAKI hakujawahi kutokea CCM ikashinda.

Wizi wa kura na mauaji ya raia ndivyo fuel ya CCM kuendelea kutawala
 
Back
Top Bottom