Pre GE2025 Kwa Respond hii ya Kariakoo, kuirudisha Serikali ya CCM madarakani itabidi tujitafakari

Pre GE2025 Kwa Respond hii ya Kariakoo, kuirudisha Serikali ya CCM madarakani itabidi tujitafakari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yaah mimi ni mjinga sana mkuu, Ni
Mjinga kiasi kwamba nimeshindwa kutambua siasa inavyochangia kutokea kwa Majanga...

Ikiwemo ilivyochangia mafuriko kule Arusha, maporomoko ya ardhi kule HANANG ..

Pia sijaona Siasa mbovu za nchi kama china mpaka hili jengo likaanguka bila sababu mwaka 2009 .

Wewe ni Genious sana, unaona mbali 👏👏
View attachment 3153851

NB: Siasa China ni hovyo sana, just imagine walishindwa kusimamia ujenzi wa hili jengo 😆😆

Ndiyo ni "mjinga" ingalau katika ufahamu wa eneo hili. Ni vizuri kuwa umekiri mwenyewe kuwa u - mjinga na ndivyo ulivyo kweli...

Nikutie moyo kuwa ujinga unatibika..

Kwa hili la ajali ya kizembe ya Kariakoo - DSM, ngoja nikuwekee kwa lugha hii labda utaelewa...

Ni kwamba, majanga ya asili ni kitu kimoja na nchi/taifa kuwa tayari wakati wowote kujiandaa kukabiliana na majanga hayo kwa utaalamu na vifaa vya uokozi ni kitu kingine kabisa..!

Lakini Kuna maswali mawili kwako yafuatayo:

1. Kwa ufahamu na maoni yako, hili la kuporomoka jengo la Kariakoo - DSM unadhani ni "natural disaster" au "it's just a man made disaster" tokana na uzembe, sera mbovu za makazi na ujenzi na uongozi bomu wa nchi hii...?

2. Umelinganisha kuporomoka kwa jengo huko China na hapa kwetu Bongoland...

Uko sawa na haina shida....

Lakini ungeenda mbele zaidi kwa kulinganisha sababu za kuporomoka kwa jengo huko China na hapa Tanzania...

Halafu upige hatua mbele zaidi ulinganishe mwitikio wa taasisi/vyombo vya uokoaji huko China na hapa Bongo...

Ukimaliza kueleza hayo, njoo nirudie tuendelee kuijadili hoja ya:

Ni kwa vipi mambo haya yako related moja kwa moja na siasa na uongozi wa nchi yetu...

Asante, ubarikiwe...
 
Mimi ni mjinga ambayo ni afadhali kuliko kuwa mpumbavu .

Nianze kujibu swali - Chanzo cha Jengo la Shanghai china kuporomoka [2009] ikujibu AI maana nikijibu mimi utaona kama naleta porojo ;
chrome_screenshot_17 Nov 2024 20_32_52 GMT+03_00.png

Je, hili jengo lilianguka bahati mbaya? Sasa jiulize Kati ya Tanzania na China nchi gani iko polical Stable? China

Iko hivi Gentleman - Mara nyingi hua mainjinia wanashindanishwa bei ya ujenzi, kila mmoja anaweka Masterplan yake na bei zake...

Sasa kwa nchi zetu za kipato cha chini Tajiri anachagua Engineer wa bei ya chini kupunguza gharama za uendeshaji...

Sasa Hapo hapo kwenye bei cheap bado Injinia atataka afaidike tena sababu bajeti aliyopanga ni ndogo hivyo atalazimika kupunguza viwango na kununua material fake ili apate faida kubwa ...

Watu wa serikali watafika kukagua wataambiwa ghorofa inafata viwango na tena wataonyeshwa sample fake za viwango bora, watatoa kibali, Over!!
[Ninaongea kama mtu mwenye Experience - Nimefanya kazi kama fundi kwenye Ghorofa kadhaa za watu Private before sijawa Mjasiriamali]

Unafikiri nini kitafuata? Jengo linakua linabet na Maisha ya watu mda wote .

Labda nikazie tena Chanzo kikuu cha majengo kuporomoka sio siasa ni Uzembe, kukosa ujuzi sahihi wa ujenzi pia Hali mbaya ya mfuko .

Hapa AI inaelezea kwa kina zaidi;
chrome_screenshot_17 Nov 2024 20_45_04 GMT+03_00.png

Sababu ya ujinga walikua confident kabisa wakiamini wanafanya kitu sahihi, labda sababu hiyo mbinu ya kuchimba chini ya jengo imeshawahi kuwapa matokeo mazuri before...

NB : Niwape pole ndugu zetu wote waliopatwa na Majanga lakini sasa ni wakati sasa wa Mamlaka za ujenzi na Maengineer kujifunza ili makosa yasijirudie ...
 
Wabongo huwa hatujali! Tupo buzy na gamond kututoka na pia ushindi wa taifa stars tumempa mama, hili nalo litapita wamekufa maskini kwanza why bother?
 
Mimi ni mjinga ambayo ni afadhali kuliko kuwa mpumbavu .

Nianze kujibu swali - Chanzo cha Jengo la Shanghai china kuporomoka [2009] ikujibu AI maana nikijibu mimi utaona kama naleta porojo ;View attachment 3154850
Je, hili jengo lilianguka bahati mbaya? Sasa jiulize Kati ya Tanzania na China nchi gani iko polical Stable? China

Iko hivi Gentleman - Mara nyingi hua mainjinia wanashindanishwa bei ya ujenzi, kila mmoja anaweka Masterplan yake na bei zake...

Sasa kwa nchi zetu za kipato cha chini Tajiri anachagua Engineer wa bei ya chini kupunguza gharama za uendeshaji...

Sasa Hapo hapo kwenye bei cheap bado Injinia atataka afaidike tena sababu bajeti aliyopanga ni ndogo hivyo atalazimika kupunguza viwango na kununua material fake ili apate faida kubwa ...

Watu wa serikali watafika kukagua wataambiwa ghorofa inafata viwango na tena wataonyeshwa sample fake za viwango bora, watatoa kibali, Over!!
[Ninaongea kama mtu mwenye Experience - Nimefanya kazi kama fundi kwenye Ghorofa kadhaa za watu Private before sijawa Mjasiriamali]

Unafikiri nini kitafuata? Jengo linakua linabet na Maisha ya watu mda wote .

Labda nikazie tena Chanzo kikuu cha majengo kuporomoka sio siasa ni Uzembe, kukosa ujuzi sahihi wa ujenzi pia Hali mbaya ya mfuko .

Hapa AI inaelezea kwa kina zaidi;
View attachment 3154849
Sababu ya ujinga walikua confident kabisa wakiamini wanafanya kitu sahihi, labda sababu hiyo mbinu ya kuchimba chini ya jengo imeshawahi kuwapa matokeo mazuri before...

NB : Niwape pole ndugu zetu wote waliopatwa na Majanga lakini sasa ni wakati sasa wa Mamlaka za ujenzi na Maengineer kujifunza ili makosa yasijirudie ...
Sasa sababu inayokufanya ubishane na mimi kwa hili ni nini hasa maana naona wazi kuwa tunatembea ktk mawazo sawa. Kwanini hukubali kuwa mambo haya shida inaanzia kwenye mifumo ya kisiasa na kisheria..?

Inawezekana shida yako ni pale nilipokuambia kuwa, huwezi kuacha kuhusisha na kuwatupia wanasiasa walio kwenye madaraka ya kiserikali matukio haya mauaji yanayosababishwa na uzembe na makosa ya makusudi ya wasimamizi na watunga sera, sheria na kanuni za masuala ya ujenzi na miundombinu ya ujenzi kwa ujumla kiasi cha uzembe wao kuleta madhara na mauaji kama hivi...

Sasa kwa hiki ulichokileta hapa, simama na ukubaliane nami kuwa serikali zote za China na Tanganyika haziwezi kukwepa lawana za maafa haya...

Na kwa hapa Tanganyika, CCM ndicho chama cha siasa kinachounda na kuongoza serikali na sera na mipango yake ya kisiasa ikiwemo ya ujenzi na makazi ndizo zinazotekelezwa hapa nchini...

Sera zao na mipango yao inapofeli na kusababisha majanga na maafa kama haya, wasione haya au shida kubeba lawama na waye tayari kukiri kuwa, hapa tumeboronga...

Hawa sio kwenye sekta ya ujenzi na makazi tu. CCM mambo yao ni majanga na shida kwenye sekta karibu zote. Mfano barabara nyingi zinajengwa chini ya kiwango, elimu iko hoi, afya ni shida tupu, maji ndo usiseme ni taabu na shida tupu nchi nzima, rushwa na ufisadi ndilo donda ndugu kabisa...

Kila sekta iko hovyo chini ya CCM. We need great political, social & economic reforms now...!!
 
Kwa kweli kuipigia kura CCM tena tunastahili kupimwa akili kama ziko sawa.
Aisee, mkuu 'Chakaza', mbona unashangaza. Haya unamwambia nani? Huko huko kwa walio patwa na janga, hujaona wakitoa "shukrani" nyingi kwa mtu pekee anaye shikilia kila kitu ndani ya nchi hii kwa sasa hivi?
Watu wanadiriki kutoa shukrani kwa Rais Samia kwa kuokoa maisha ya wahanga 45; na kushukuru pia kwa wenzao wengine ambao hawakufanikiwa kunusurika?

Hawa ni watu ambao walikuwepo kwenye tukio lenyewe, na wana shukuru mtu ambaye hata hana habari ya nini kimetokea hapo!
Nchi hii sasa ipo kwenye hali ya kutisha sana. Watu wanapo tekwa na wengine kuuawa, huku wengine wakishangilia matukio kama hayo!
Humu humu JF, kila siku tunashuhudia watu wakishangilia wakipatwa na mikasa, hasa kama watu hao hawakubaliani na upande waliopo wao! Hii imekuwa ni nchi tena, au pori la wanyama?

Sasa unazungumzia "kupigia kur tenaa CCM", kana kwamba CCM wanahitaji kura ya mtu yeyote kuwepo madarakani!
Bado hujaridhika na unayo yaona kwenye maandalizi ya uchafuzi wa serikali za mitaa? Wewe unataka CCM na serikali yake wafanye nini ndipo uamini kuwa matumaini ya kura yako kumchagua kiongozi unaye mtaka ni njozi ya kutisha.
 
Tukiongea humu tunaonekana wajuaji ila huo ndo ukweli.

CCM imefikiwa mwisho wa uwezo wake kuweza kuwapeleka Watanzania sehemu wanayotakiwa kuwa.

Mbaya zaidi saivi moderators wanafuta hadi nyuzi za maana ambazo watu wanaziandika kama sehemu ya mawazo huru
Nilipo anza kukusoma JF, nilikusoma tofauti na ninavyo kusoma sasa!
Naamini kuna waTanzania wengi wenye mfanano na wewe, ila hawasikiki tu. Sasa sijui kufanyike nini watu hawa waungane na wengine ili kuibadili hali yetu hii inayozidi kuwa duni kila siku!
 
Tukio la maafa limetokea katikati ya jiji eneo lenye watu wengi saa 3 asubuhi, lakini vyombo vyote vya uokozi vimechukua masaa kujitokeza kuokoa watu waliochini hadi Raia wasio na dhana za uokozi wanatumia mikono mitupu kuokoa watu hii ni aibu kwa serikali hii.

Askari hawaonekani kama wale wa maandamano ya Chadema kwa mamia bali mmoja mmoja na kitambi chake, huu ni wendawazimu kabisa yaani kuyafanya maandamano ni ya hatari kuliko maafa kama kudondoka jengo na kufukia watu?

Pengine Mungu anatuonyesha ubovu wa serikali yetu tuliyokubali iwe madarakani huku pamoja na kutupatia "UFAHAMU" bado tunashangilia "mitano tena".

Kwa kweli kuipigia kura CCM tena tunastahili kupimwa akili kama ziko sawa.

View attachment 3153700

Uchaguzi ni uamuzi binafsi, we chagua chama unaona kinafaa. Matukio km hayo yako dunia nzima. Acheni kuokoteza matukio km siasa za majukwaani zimewashinda fanyeni shughuli zingine.
 
Tatizo sio CCM tatizo ni wananchi wenyewe. kuna ujinga na ushamba, imagine jeshi linakuja kwa kuchelewa, wanatembea kama wanaenda kwenye harusi, kisha wajinga waashangilia et "jeshi, jeshi jeshi" huo ni ujinga zaidi
Inawezekana hukuelewa lugha waliyo kuwa wakiitumia hao watu kwa hilo jeshi? Ningependa kuamini kuwa wananchi hao walikuwa na maana yao tofauti na uliyo ielewa wewe.
 
Kwa kweli kuipigia kura CCM tena tunastahili kupimwa akili kama ziko sawa.
Mkuu Chakaza , you might be very right, ila ili mtu asiipigie kura CCM, lazima kuwepo chama mbadala cha kukipigia kura, but very unfortunately, kwa nchi yetu Tanzania, chama cha kuchagulika chenye uwezo wa kuiendesha nchi yetu Tanzania, ni kimoja, the one and only!, hivyo usipoichagua CCM, uchague nani?.

Angalia tarehe za mabandiko haya
Hivyo CCM bado ipo ipo sana, na despite all the odds, CCM itaendelea kuchaguliwa kwasababu CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!
CCM ni Dola!.
P
 
Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, ni muhimu kufikiri kwa makini kuhusu uongozi wetu na jinsi unavyoshughulikia masuala ya msingi yanayoathiri maisha ya wananchi. Ni jambo la kushangaza na kukatisha tamaa kuona Rais wetu akielekea kwenye mikutano ya kimataifa, wakati nyumbani kuna maafa makubwa yanayohitaji uongozi wake wa karibu. Kutojishughulisha na masuala haya ni uthibitisho wa kutokujali hisia na mahitaji ya watu waliomchagua.

Kama ilivyo kawaida katika nchi nyingi, viongozi wanapokumbana na matatizo makubwa, kama vifo vya raia zaidi ya 13, inatarajiwa kuwa watachukua hatua za haraka na kuonyesha mshikamano na jamii. Lakini badala yake, tunaona Rais akifanya mipango ya safari ambazo hazina umuhimu wa dharura. Ni kweli kwamba wakati mwingine wanaweza kukabiliwa na majukumu mengine, lakini je, kweli kuna jambo lolote muhimu zaidi kuliko maisha ya watu? Hii ni dhahiri ya kutojua na kukosa uelewa wa hali halisi ya wananchi.

Kila kifo ni hadithi ya maisha, na kila mmoja wa waliokufa alikuwa na familia, marafiki, na jamii ambayo inakabiliwa na maumivu na huzuni. Hivyo, ni jukumu la Rais kuonyesha uongozi wa kweli, kutojificha nyuma ya kisingizio cha majukumu mengine. Kuwa muungwana hakumaanishi tu kusema maneno ya faraja; inahitaji vitendo vinavyothibitisha kwamba unajali na unaguswa na hali halisi ya raia.

Wakati tunaposema "huyu ni mtu wa watu," tunatarajia kuona mabadiliko katika matendo yake, na sio maneno matupu. Ni rahisi kwa viongozi kusema wanaweza kuja kwa wananchi wakati wa kampeni, lakini je, wanajali kweli? Tunaona kwamba wengi wao wanatumia lugha nzuri ili kupata kura, lakini wanaposhika madaraka, wanajitenga na matatizo ya wananchi. Tunashuhudia viongozi wakifanya ahadi ambazo hazitekelezwi, na hatimaye wanarudi kwa raia wakati wa kampeni nyingine, wakitumia maneno kama "mama atosha" kama kivuli cha ukweli wa hali halisi.

Ni muhimu pia kutambua kwamba Rais anapaswa kuwa na washauri wazuri, lakini ni wazi kwamba katika baadhi ya matukio, amekosa ushauri mzuri. Kuwa na washauri wazuri ni muhimu, lakini pia ni jukumu lake mwenyewe kutafakari na kuona ni nini kinachotokea katika jamii. Kufanyika kwa maafa, kama vile vifo vya watu 13, ni dalili tosha ya kwamba kuna haja ya maamuzi ya haraka na ya busara. Kutangaza maombolezo ya kitaifa si tu ni ishara ya kuheshimu waliokufa, bali pia ni njia ya kuonyesha kwamba serikali inajali na inatambua maumivu ya raia wake.

Kwa hivyo, tunahitaji kujiuliza: Je, Rais huyu anatoshea kuendelea kuwa kiongozi wetu? Je, tunahitaji mtu ambaye anaweza kujiweka mbali na matatizo ya raia? Tunahitaji kiongozi ambaye anaweza kuungana na wananchi, ambaye anajali na kuonyesha uongozi wa kweli katika nyakati za shida. Wakati wa uchaguzi wa 2025, ni muhimu kwa wapiga kura kufikiri kwa makini na kufanya maamuzi ambayo yataweza kubadilisha hali hii ya uongozi.

Kwa kumalizia, ni wazi kwamba ni wakati wa kutafakari maisha na vipaumbele vyetu kama taifa. Tunahitaji kiongozi ambaye atajali hisia za wananchi, ambaye atajitolea kwa watu na ambaye ataonyesha uongozi kwa vitendo, si maneno tu. Hii ni nafasi yetu ya kuamua mustakabali wa taifa letu, na ni muhimu kuhakikisha kwamba tunachagua viongozi wanaoleta mabadiliko ya kweli na endelevu.
 
Tukio la maafa limetokea katikati ya jiji eneo lenye watu wengi saa 3 asubuhi, lakini vyombo vyote vya uokozi vimechukua masaa kujitokeza kuokoa watu waliochini hadi Raia wasio na dhana za uokozi wanatumia mikono mitupu kuokoa watu hii ni aibu kwa serikali hii.

Askari hawaonekani kama wale wa maandamano ya Chadema kwa mamia bali mmoja mmoja na kitambi chake, huu ni wendawazimu kabisa yaani kuyafanya maandamano ni ya hatari kuliko maafa kama kudondoka jengo na kufukia watu?

Pengine Mungu anatuonyesha ubovu wa serikali yetu tuliyokubali iwe madarakani huku pamoja na kutupatia "UFAHAMU" bado tunashangilia "mitano tena".

Kwa kweli kuipigia kura CCM tena tunastahili kupimwa akili kama ziko sawa.

View attachment 3153700
Tangu lini Tanzania ikawa na utayati mkubwa na Uokoaji?

Kuna wakati Serikali ya Mwendazake ilitenga pesa za kununua vifaa vya ukokoaji lakini akakataa na kutimua viongozi wa Wizara ,haya Sasa aje kuwaokoa 😁😁
 
Back
Top Bottom