Kwa sasa, mita nyingi za Luku zinaondolewa Tariff Zero

Mita zao zimesetiwa kukupandisha automatic pale tu unapozidisha Units na kukupeleka kundi la watumiaji wakubwa, lakini kukushusha pale unapokuwa na matumizi madogo haipo automatic.

Wao wanakwambia ni lazima uende ofisini ujaze form then utawaachia wao watashugulikia. Subiri sasa washugulikie[emoji1787][emoji1787]
 
Wengi tu mnatuweka siko, mtaani hapa tunatumia unit 85 kwa miezi miwili au mmoja na wiki 2(minimum)..
 
Awamu ya 5 ndio imesababisha yote haya, ilikopa sana pesa
Ni kweli Mkuu, haya ndio matokeo ya serikali ya hovyo ya awamu ya 5, sasa kuna madeni mengi ambayo lazima yalipwe maana mengi yao yana riba kubwa ukichelewa kulipa, unaona wanavyotukamua kwenye huduma za simu,
 
Nilikwenda tanesco kurasini kuulizia wakasema wamepokea waraka toka ewura kuwa Dar es Salaam watu wote wana uwezo hivyo tariff 4 iondolewe lakini tulipowasiliana na ewura wakasema hilo no pendekezo bado halijapitishwa lakini tanesco kurasini wameshikilia huo msimamo wa kuondoa tariff 4
 
Tafadhali pitia maelezo yote mwanzo wa thread hii tumefafanua hili
 
Tanesco tatizo lao ni kuchelewa kuunganishia wateja umeme....kuna site hapa inahitaji nguzo..naanza kuwaza kama nitafikiwa kweli?
 
Tafadhali pitia maelezo yote mwanzo wa thread hii tumefafanua hili
Tariff ziliwekwa kutokana na kiwango cha matumizi ya mhusika ila mnachofanya tanesco ni kuforce kupata mapato makubwa halafu mabadiliko kama hayo yana taratibu zake na sio kukaa na kujiamria
 
Nyie ni wezi, mngekuwa mna nia njema ya kutoa huduma kwa wateja mngekuwa wazi na mambo yenu, mimi natumia unit 60-65 kwa mwezi bado niko tarrif 4, namba yangu ya mita ni 01313926840, wekeni utaratibu mzuri smart wa mtu kuwasiliana na makao makuu kwa ajili ya kupata huduma hii, maana tukienda kwenye ofisi zenu za kanda na mikoani huduma ni mbaya sana
 
Serikali imeamua kukwapua pesa za watu kwa njia nyingine baada ya ile ya DPP na uhujumu uchumi kusitishwa kwa muda mpaka 2026 pale mama na Kikwete watakapoitwa wote wastaafu
 
Tafadhali pitia maelezo yote mwanzo wa thread hii tumefafanua hili
Nyumba yangu, tumelipia umeme, gharama zote na kila kitu ni tangu mwezi wa nne mwishoni lakini mpaka leo hamjaja kuweka umeme na tuliambiwa ni ndani ya mwezi mmoja tu.

Mnazungusha zungusha tu
 
Nyumba yangu, tumelipia umeme, gharama zote na kila kitu ni tangu mwezi wa nne mwishoni lakini mpaka leo hamjaja kuweka umeme na tuliambiwa ni ndani ya mwezi mmoja tu.

Mnazungusha zungusha tu
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Mh Tanesco samahani sana, mita namba 24216933469 ina sifa zote za kuwekwa kwenye hiyo inayoitwa tarrif zero.Mbona hamuiweki?
 
Hii nchi haiwezi kujengwa kwa kutegemea pesa za misaada ya wazungu, ni lazima watanzania tujitoe kwa jasho na damu kuijenga nchi yetu.
 
Na hakuna meter separation. Maana meter separation inaongeza wateja lakini haiongezi mapato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…