Kwa sasa, mita nyingi za Luku zinaondolewa Tariff Zero

Kwa sasa, mita nyingi za Luku zinaondolewa Tariff Zero

Ndugu wapendwa wateja wetu!

Wateja wetu wote wanawekwa kwenye makundi ya matumizi yanayoendana na matumizi yao kwa kuzingatia wastani wa matumizi na eneo alilopo.

Ifahamike kuwa hakuna mteja wa matumizi ya nyumbani anayeweza kuwekwa kwenye kundi la matumizi ya viwanda.
Kundi la matumizi ya viwanda elfu 10 wanapata gb ngapi?
 
Mimi sijawahi zidisha units 50 kwa mwezi tangia niunge umeme 2018 lakini hawajaniweka kwenye hiyo tarrif D1
Mkuu rudi nyuma kwenye maelezo yake amesena kigezo cha kwanza ni uwe kijijini, wewe Upo Goba una disqualify
 
Nyie ni wezi, mngekuwa mna nia njema ya kutoa huduma kwa wateja mngekuwa wazi na mambo yenu, mimi natumia unit 60-65 kwa mwezi bado niko tarrif 4, namba yangu ya mita ni 01313926840, wekeni utaratibu mzuri smart wa mtu kuwasiliana na makao makuu kwa ajili ya kupata huduma hii, maana tukienda kwenye ofisi zenu za kanda na mikoani huduma ni mbaya sana
Unaanza na kutukana halafu unaomba msaada
 
Meter ya mama yangu ilipiga short baada ya kuanguka mti huko barabarani wakaja TANESCO wakaiangalia wakasema haifai tena ilikuwa na unit 190 wakasema hatuwezi kuzipata maana tumefungiwa meter Mpya hazihamishiki
 
Nyumba yangu, tumelipia umeme, gharama zote na kila kitu ni tangu mwezi wa nne mwishoni lakini mpaka leo hamjaja kuweka umeme na tuliambiwa ni ndani ya mwezi mmoja tu.

Mnazungusha zungusha tu
Yaan wewe yale maneno ya kalemani uliyaamini ?, zile zilikuwa ni porojo tu, endelea kusuubiri labda mwezi kwao haujaisha
 
Unaanza na kutukana halafu unaomba msaada
Wewe uaona sio wezi ?, haya wanayoyafanya kwa wateja ni nini ?, siombi msaada, ndio maana nimesema waweke utaratibu mzuri ili mtu akae mahala anapostahili, sio mtu haki yako mpaka ujiombeleze, umesikia mdau mmoja amesema pale juu kwamba, kukuweka tarifu 1 ni auto lakini ukitaka kurudishwa tarrif 4 ni mpaka uandike maombe na yakajadiliwe, kwangu mimi huo ni wizi
 
Meter ya mama yangu ilipiga short baada ya kuanguka mti huko barabarani wakaja TANESCO wakaiangalia wakasema haifai tena ilikuwa na unit 190 wakasema hatuwezi kuzipata maana tumefungiwa meter Mpya hazihamishiki
Mkuu, ukifuatilia wanakurudishia.
 
Tanesco mkitoka kula eid msisahau kunijibu hili leo nilinunua umeme wa tsh. 500 kama nilivyozoea nkakuta mmeikata na unit ikasoma zero zero. Nkanunua tena wa 500 nkipata unit mbona mwanzo haikuwa Hivyo maana matumizi yangu sio makubwa Hivyo inakuaje tsh 500 ya mwanzo mliikata sikupata unit
 
Ndugu wapendwa wateja wetu!

Wateja wetu wote wanawekwa kwenye makundi ya matumizi yanayoendana na matumizi yao kwa kuzingatia wastani wa matumizi na eneo alilopo.

Ifahamike kuwa hakuna mteja wa matumizi ya nyumbani anayeweza kuwekwa kwenye kundi la matumizi ya viwanda.
Sasa kama nilikuwa nanunua unit 5.7 kwa 2000/= na hiyo sio tarrif Zero, kwanini sasa mbadilishe mtunyonye hivyo?

Mimi nawasha bulb 4 tu na kuchaji simu.
 
Hii wiki imekua Ni vilio kwa watu kila mahali,

Wengi wameondolewa tarrif zero, na Hakuna maelezo ya kueleweka.

Tumezoea ukizidisha matumizi ya unit 70 kwa mwezi, automatically system inakuondoa tariff zero (umeme wa 1,000= unit 8.4)
Kwa sasa unaondolewa tu kwa lazima hata Kama ujazidisha.

Mtu Hana tv Wala redio, anatumia balbu 2 tu na simu kaondolewa tarrif zero. Akitaka kununua umeme UNAGOMA afu anaambiwa "unatakiwa upate key change".

Sijajua ndo ukusanyaji mpya wa mapato ya serikali kwa kulazimisha watu wengi watumie tarrif 4 (umeme wa 1000= unit 2.9) au Kuna kitu kingine pembeni kinaendelea TUFAHAMISHWE.

Kwa maana tangu huu mwezi uanze, vijana wa Tanesco wamekua wakipita nyumba Hadi nyumba mara kwa mara, wakidai wanakusanya takwimu za mita za luku.
WEEE NDUGU HUTAKI KUSHIKAMANA
KAMA HUJUI.NDIO MSHIKAA......HUO
 
Mbuge babu tale
Kusoma bajeti yawizara na uijadili nikazi inahtaj maarifa mana imeandikwa na mtaalam
 
Hongera kumbe unajenga, tungejuaje sasa, kaza umalize jengo sasa
Na bado kwanza serikali angalieni na mafundi mbalimbali yaani juzi tuu hapa fundi kanikamua 1,000,000 eti kujenga msingi na nyumba usawa wa Renta huku hajalipa kodi yoyote

Hamuoni mnapoteza mapato ,wapenzi leseni za kazi hao,kwa sasa hawalipi kodi ila utasikia nao wanalilia eti bei ya miamala iko juu,pumbavu sana
 
Ndugu wapendwa wateja wetu!

Wateja wetu wote wanawekwa kwenye makundi ya matumizi yanayoendana na matumizi yao kwa kuzingatia wastani wa matumizi na eneo alilopo.

Ifahamike kuwa hakuna mteja wa matumizi ya nyumbani anayeweza kuwekwa kwenye kundi la matumizi ya viwanda.
Tanesco, naona hamjibu maoni na maswali ya wadau
 
Tanesco wanakwepa tu kuwaambia ukweli hapa ili kifupi ni kuwa hiyo huduma kwa Sasa ipo vijijini tu kwa Yale maeneo ambayo wana ruzuku.
Mimi nimejaza form tangu mwanzoni mwa mwezi wa nane mwaka Jana na kipindi chote hicho wamekuwa wakinizungusha tu hadi juzi walipoamua kuniambia ukweli
Screenshot_20210722-121315.jpg
 
Back
Top Bottom