Kwa sasa, mita nyingi za Luku zinaondolewa Tariff Zero

Tafadhali tambua sio kwa sasa bali muda wote wateja waliopo mijini wenye matumizi ya kuanzia unit 76 hadi 7500 kwa mwezi wanakuwa Tarif 1 na waliopo vijijini wenye matumizi chini ya unit 75 kwa miezi mitatu mfululizo wanakuwa Tarif four na waliozidi hapo hadi 7500 wanakuwa tarif 1. Hii ipo wazi kwenye miongozo yetu
 
Naomba kuelimishwa juu ya tariffs
1. Why anayetumia sana ndo analipa sana!?
2. Kwanini kuwe na hizo tariffs!? why not flat rate!?
 
Yaani huwezi jibu bila kuweka hayo makitu..!? Au unataka ujuwe nani kayaandika hayo!?
Tutumie taarifa hata PM tukujibu kwa data kamili kwani lengi ni wewe uelewe na sisi tujitidhishe muwa tumekuelewesha
 
Tutumie taarifa hata PM tukujibu kwa data kamili kwani lengi ni wewe uelewe na sisi tujitidhishe muwa tumekuelewesha
Ziwekeni hapa hizo data... itaondoa kuulizwa swali hili hilo na kila mtu
 
Na waliopo mijini wenye matumizi chini ya 75 units wapo tarrif gani?
 
Naomba kuelimishwa juu ya tariffs
1. Why anayetumia sana ndo analipa sana!?
2. Kwanini kuwe na hizo tariffs!? why not flat rate!?
Sio kweli kuwa anayetumia sana ndio anayelipa sana watumiaji wa umeme haswa viwanda bei yao ipo chini zaidi na wana matumizi makubwa zaidi lengo ni kuhamasisha uzalishaji, kuboresha hali ya maisha na kuhakikisha mfumuko wa bei unakuwa rafiki.Kuhusu kucharge wote kiasi kimoja ushauri umechukuliwa
 
Sasa nina miaka 3 kasoro tangu nimeweka umeme na kwa muda wote huo sijawahi kuvuka unit 75 kwa mwezi na nimejaza form Sasa Ni mwaka mmoja sijapata hiyo huduma. Tatizo liko wapi?
 
Sasa nina miaka 3 kasoro tangu nimeweka umeme na kwa muda wote huo sijawahi kuvuka unit 75 kwa mwezi na nimejaza form Sasa Ni mwaka mmoja sijapata hiyo huduma. Tatizo liko wapi?
Tunaomba namba yako ya mita tuangalie
 
Mkuu mimi shida yangu ni tofauti kidogo.Nyumba yangu inatumia mita moja na ya mpangaji.Takriban miaka mitatu iliyopita niliomba nyumba ya mpangaji iwekewe mita.Nikaambiwa nifuate taratibu zote za kuwekewa umeme nikafanya hivyo.Nikalipa Sh.30,000 za contractor ingawa nyumba tayari ilikuwa na umeme.Mpaka leo mita sijaiona,na nikifuatilia naambiwa nianze process upya,huku hela yangu ikiwa imezama.Hii ni sawa kweli na nifanyeje?
 
Je ulilipa kwa control numbee kupitia bank? Ulilipa kwa jina lipi namba ya simu uliyoandika na wilaya tafadhali
 
Je ulilipa kwa control numbee kupitia bank? Ulilipa kwa jina lipi namba ya simu uliyoandika na wilaya tafadhali
Ndio mkuu.Nakumbuka pia nilipewa slip ya kupeleka Sub-Office ya TANESCO ambayo ingefanya hiyo kazi.Niliambiwa nisubiri nipate message ili nikamalizie malipo ya Sh.27,000.Mpaka leo sijapata hiyo message.

Hata hivyo bado nashangaa kwa nini niliambiwa nilipe hela ya contractor wakati nyumba ilikuwa kuweka mita tu umeme ulikuwepo tayari.
 
Kimsingi haukulipa hela TANESCO kwa kuwa malipo kwa mkandarasi ni makubaliano yenu hivyo fika ofisi unaa za taratibu na ulipe kwa kupitia control number utakayopewa.
 
Kaka nunua solar uwakomeshe

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…