Kwa sasa, mita nyingi za Luku zinaondolewa Tariff Zero

Nafikiri hiyo 30k unazungumzia ile ya uchoraji ramani
 
Mimu tangu 2016 nauziwa unit kwa bei zaid ya 200 wakat matumiz yangu ni chin ya unit 30 kwa mwezi mf nikinunua umeme wa shiling 1000 napata unit 2.8 wakat huo jiran kwa hiyohiyo 1000 anapata zaid ya unit 7 inakuaje hapo???
Nanda kabadili uende Tarif4
 
Nia ya bei ya matumizi ya unit 75 ilikuwa kuwasaidia wenye kipato kidogo, japo sasa imeingiliwa. Wenye uwezo mradi matumizi yake si makubwa, eg nyumba za mapumziko za michepuko, maduka ya nguo etc nao wamo.
 
Pls tutofautishie lwanza hiyo D1 na T1, Unamaanisha nini? Na hapo kwa wateja waliopo mjini kutumia mpaka unit 7500 kwa mwezi sijaelewa au umemaanisha 75?
 
Pls tutofautishie lwanza hiyo D1 na T1, Unamaanisha nini? Na hapo kwa wateja waliopo mjini kutumia mpaka unit 7500 kwa mwezi sijaelewa au umemaanisha 75?
D1 ni wateja wanaonunua umeme chini ya unit 75 kwa mwezi, wanaozidi hapo hadi 7500 ni T1 ambao ni matumizi ya nyumbani
 
Mimi sijawahi zidisha units 50 kwa mwezi tangia niunge umeme 2018 lakini hawajaniweka kwenye hiyo tarrif D1
Nenda TANESCO, ofisi iliyopo jirani nawewe waambie wakurekebishie Mkuu, kuna form utajaza.
 
Nahitaji kuunganishiwa umeme, nilifata taratibu zote anzia kujaza form tangia mwaka Jana mwez wa Saba mwaka Jana, juzi nikaenda kumuona mkurugenzi wa Tanesco mkoa wa Kilimanjaro, akaniambia Hadi waombe budget ya eneo husika, nataka tu kufahamu umeme unaenda kwa maeneo ama kila anayehitaji umeme anaweza unganishiwa kama hakuna shida yoyote mf. Nguzo? Maana km kulipia nguzo tuko tayari Ila nashangaa kwanini inakuwa ngumu sana kupata umeme? Eneo ni Pumuani, Mkoa wa Kilimanjaro. Naomba sana km mkurugenzi atasoma hapa ama mtampa taarifa, tunahitaji umeme kwasababu anzia mwaka Jana kabla taratibu za kulipia nguzo hazijaja tulikuwa tumejaza form na walikuja wakakagua wakaondoka hadi Leo sijawaona. Pumuani barabara inayoenda Mkonga, tuko zaidi ya watu 15 pamoja na shule inayojengwa, tunaomba umeme jamani.
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Je Waliopo mijini lakini wana matumizi chini ya unit 75 kwa miezi mitatu?
TANESCO

Pia kuna mdau ameuliza kuwa kwanini kupelekwa Tarif T1 ipo automatically lakini kurudishwa Tarif D1 ihusishe kuandika barua?
 
Mteja anapaswa kuandika barua kwa kuwa matumizi hayo yamekusudiwa kwa watu wa kipato cha chini hivyo unapoanesha nia ya kuyahitaji lazima uombe tufanye uhakiki na kujiridhisha kama unakidhi vigezo
 
Mteja anapaswa kuandika barua kwa kuwa matumizi hayo yamekusudiwa kwa watu wa kipato cha chini hivyo unapoanesha nia ya kuyahitaji lazima uombe tufanye uhakiki na kujiridhisha kama unakidhi vigezo
Sasa kama nipo kijijini kweli na matumizi ya umeme ni madogo hayafiki hata 60 units kwa mwezi kwanini hamumuweki mteja kwenye D1 automatically? Ilihali majirani wote wapo D1?
 
I have done the same mistake today
 
Nenda TANESCO, ofisi iliyopo jirani nawewe waambie wakurekebishie Mkuu, kuna form utajaza.
Hawawezi kukupa hizo fomu,
Nilienda nikaambiwa kwa sasa hatutoi,mpaka tutakaporuhusiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…