Kwa sasa, mita nyingi za Luku zinaondolewa Tariff Zero

Kwa sasa, mita nyingi za Luku zinaondolewa Tariff Zero

Tunakujulisha kuwa upo kundi sahihi la matumizi na manunuzi yako ya umeme yanafika mpaka unit 97 kwa mwezi
Sio kweli wengi sana matumizi sio ya viwanda ila tunalipia tarrifs izoo kubwa
Mita namba 37207033004 angalia utajua na nshatuma maombi skunyingi sana kurudi tarrifs 0
 
Tunakujulisha kuwa upo kundi sahihi la matumizi na manunuzi yako ya umeme yanafika mpaka unit 97 kwa mwezi
Ndio maana nimesema nyinyi wezi, mimi ndie mwenye hiyo meter number na ninatumia kiasi cha units 70 mpaka 73 kwa mwezi, hizo Units zako 97 umezipata wapi, Nyie ni wezi, Tungekuwa na serikali sikivu ingeruhusu makampuni binafsi kama ilivyo kwenye ving'amuzi na simu za mikononi.

Na hata kama ni 97 kwanini na kwa makubaliano nanani mliamua kuifanya hiyo numba iwe kama ni Anasa ??, kwanini isiwe 100 ??
 
Akili za Kiafrika eti kwasababu nyumba ina vitu vingi vinavyohitaji umeme ili kurahisisha maisha, wao wanakuambia unatakiwa uingie kundi la viwandani! You TANESCO a incompetent and dumb. Kwahiyo kigezo cha kiwanda kwaakili zenu ni mtu kutumia zaidi ya unit 97 kwa mwezi?? Be smart guys!
 
Isiwe rahisi kutumia lugha ya kudhani wanaokuhudumia hawajui wanachofanya bali zipo taratibu na miongozo ya makundi mbalimbali ya watumiaji wa umeme hivyo wateja wetu wanawekwa kwenye makundi yanayoendana na matumizi yao
 
Akili za Kiafrika eti kwasababu nyumba ina vitu vingi vinavyohitaji umeme ili kurahisisha maisha, wao wanakuambia unatakiwa uingie kundi la viwandani! You TANESCO a incompetent and dumb. Kwahiyo kigezo cha kiwanda kwaakili zenu ni mtu kutumia zaidi ya unit 97 kwa mwezi?? Be smart guys!
Mimi nilishasema dawa ya hawa Tanesco ni kupata kampuni nyingine binafsi ili iweze kuwa challenge, wakianza kugombania wateja wao wenyewe watashikishana adabu na hapo ndipo tutapona na huu utapeli wa kila siku, Patakuwa na heshima na kuthaminiana pale tutakapokuwa na kampuni zaidi ya moja ya kutoa huduma hii ya umeme, nadhani wote mmeona jinsi Voda na Tigo wanavyopigana vikumbo kwa ajili yetu, yaani mpaka wanakuitia songesha, unafurahia kuwa na umiliki wa laini ya simu, unakuwa nazo mbili au tatu, moja ikisumbua unahamia nyingine huku unatembea, sasa kuwa na tanesco pekee yake lazima watihiriki
 
Meter ambayo haitambuliki maana yake haijadajiliwa ili ionekana kwenye mfumi ndio maana tunaomba taarifa hizo kwa wepesi wa kumudumia
Nakubaliana na wewe, nisemacho ni kuwa kwa vile anatumia ID fake, apige tu hiyo emegency namba yetu ili kuendelea kujificha kwenye ID fake...
 
Mimi mwezi huu nilinunua umeme mara mbili kwa bahati mbaya. Maana niliponunua ule wa units 75 kwa TZS. 9150 system ya bank ilionesha ime-fail hivyo ikabidi nihamie m-pesa.

Kulipa ile ya m-pesa ikaniletea units kidogo, kumbe system ya bank ilikuwa imekata kimya kimya!

Hivyo nasubiri mwezi ujao nione kama watakuwa wameniondoa kwenye hiyo ya TZS. 9150 kwa units 75.
Vipi wameshakutoa au bado
 
Ndugu wapendwa wateja wetu!

Wateja wetu wote wanawekwa kwenye makundi ya matumizi yanayoendana na matumizi yao kwa kuzingatia wastani wa matumizi na eneo alilopo.

Ifahamike kuwa hakuna mteja wa matumizi ya nyumbani anayeweza kuwekwa kwenye kundi la matumizi ya viwanda.
Kwahiyo mtu akiwa Masaki lazima awekwe kundi moja na WAMASAKI wenzie hata kama matumizi yake ni sawa na mtu wa Kigogo ambaye anatumia taa 3, redio na kuchaji simu?
 
Ndugu wapendwa wateja wetu!

Wateja wetu wote wanawekwa kwenye makundi ya matumizi yanayoendana na matumizi yao kwa kuzingatia wastani wa matumizi na eneo alilopo.

Ifahamike kuwa hakuna mteja wa matumizi ya nyumbani anayeweza kuwekwa kwenye kundi la matumizi ya viwanda
Sasa nyinyi mlikubaliana na nani kuweka hayo magrupu ?, nyie ni wezi, hamjui matumizi halisi ya wateja wenu mnakurupuka na kupamga mabei bila kuzingatia uhalisia, hivi mnadhani watu wote tunapata hela za bure kama mnavyopata nyie ?, acheni tabia hiyo, heshimuni wateja basi
 
Ndugu Mteja!

Zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022

[emoji3578]Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,

[emoji3578] Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,

[emoji3578]Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=

[emoji3578]Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,

[emoji3578] Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,

[emoji3578]umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.

Zingatia

Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= kama ilivyoelekezwa na EWURA.

NB: Gharama zote zimejumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
 
Ndugu wapendwa wateja wetu!

Wateja wetu wote wanawekwa kwenye makundi ya matumizi yanayoendana na matumizi yao kwa kuzingatia wastani wa matumizi na eneo alilopo.

Ifahamike kuwa hakuna mteja wa matumizi ya nyumbani anayeweza kuwekwa kwenye kundi la matumizi ya viwanda.

Tenesco tanzania nimelipia ili niunganishiwe umeme nimelipia Tsh 515 617.52 niko mwezi wa nne xx cjapatiwa huduma na hakuna chochote kinachoendlea sipewi taarifa yeyote
 
Tenesco tanzania nimelipia ili niunganishiwe umeme nimelipia Tsh 515 617.52 niko mwezi wa nne xx cjapatiwa huduma na hakuna chochote kinachoendlea sipewi taarifa yeyote
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Mimi mwezi huu nilinunua umeme mara mbili kwa bahati mbaya. Maana niliponunua ule wa units 75 kwa TZS. 9150 system ya bank ilionesha ime-fail hivyo ikabidi nihamie m-pesa.

Kulipa ile ya m-pesa ikaniletea units kidogo, kumbe system ya bank ilikuwa imekata kimya kimya!

Hivyo nasubiri mwezi ujao nione kama watakuwa wameniondoa kwenye hiyo ya TZS. 9150 kwa units 75.
Upo mkoa gani kiongozi?
 
Back
Top Bottom