Kwa sasa ni nadra sana kuwakuta hawa viongozi wapo Dodoma Makao Makuu, wote imekuwa ni njia moja Dar


..Nakubaliana na wewe kwa 50%.

..Ni kweli Wamarekani walitingishwa na kiongozi mhuni Donald Trump.

..Lakini ni kweli pia katiba yao ndio iliyowaokoa wasisambaratishwe moja kwa moja.

..kama katiba ya Marekani isingekuwa imesukwa kwa namna ambayo Raisi wao hawezi kuingilia uchaguzi na kupanga matokeo leo hii Trump angekuwa bado ni Raisi.

..kwa hiyo bado tunahitaji katiba bora pamoja na kwamba upo uwezekano wa wananchi kuchagua viongozi wa hovyo.

..katiba bora ndiyo itakayowapa nguvu na ulinzi WAADILIFU kumfunga breki kiongozi wa hovyo-hovyo.
 
Uonaji wa mambo wako una hitilafu.
Unatoa mfano huo wa Katiba ya marekani, unasahau ilivyo imara na jinsi inavyofanya kazi?

Huo mfano wa 'Trump' unaoutumia, wewe huoni kama ingekuwa ni katiba kama hii hapa ya kwetu Trump hadi sasa angekuwa anawaendesha wananchi wake?
Unajuwa ni mambo mamngapi, pamoja na ukichaa wake, Trump hakuweza kuyafanya kwa kushindwa kuitingisha katiba imara?
Hukumbuki lolote kuhusu 'impeachment' aliyofanyiwa?

Kwa katiba yetu hapa ni nani angethubutu kum'peach' Magufuli?
 
Hapo sasa ndipo tunaingia kwenye mjadala wa kati ya kuku na yai kipi kinamtangulia mwenzake
Ni hivi nikisema mindset naamina utambuzi wa mtu binafsi kuelewa nini mana ya kuwa na katiba na jinsi ya kuiheshimh na kuilinda hiyo katiba.kama watu hawafika kwenye hiyo level ya kutambua umuhimu wa kuiheshimu na kuilinda katiba baas ujue hata hiyo mpyaa itasiginwaa mchana na usiku..
Jambo la pili nani wakuibadilisha hiyo kindset.? Jibu ni moja tu mindset haibadilishwi na mtu mwingine yyte yule isipokuwa na muhusika mwenyewe..leo ww ukiwa na mindset inayoheshimu uhuru wa mtu basi huyo mtu uliemuheshimu leo kesho na yeye ataheshimu wengine and it keeps on evolving..
Mfano hivi unazani leo hii chadema wakikamata nchi wataheshimu uhuru wa wapinzani wao? Hakuna kwa sabab wao hawakuheshimiwaaa...hivyo to change a mindset, begins with an individual him/herself.
 
Mwisho kabisaaa..kipi kianze kati ya mindset au katiba..
Jibu ni rahisi..ili uwe na katiba bora, lazima wanaoiandaa hiyo katiba wawe na mindset nzuri ambazo hazitakuwa na bias zozote au kufanya muhiml mmoja kuwa na nguvu zid ya mwingine..hivyo katiba bora huundwa na watu wenye mindset bora na sio katiba bora ilete watu wenye mindset bora..
 
Utasemwa unaanza chokochoko ,wakati wasema ukweli, jamani viongozi Dodoma haiepukiki, hatuwezi kua twafanya Jambo twarudi nyuma, mh rais stop that
 
Katiba ,katiba, katiba
 
Endelea kushangaa
 

..mifano uliyoitoa ni ya kweli.

..mimi hoja yangu ni kwamba uamuzi wetu haukuwa na tija, wala ulazima.

..kwanini tujengee mawaziri maofisi mapya wakati tayari walikuwa na ofisi hizo Dsm?

..Ni uamuzi umeshafanyika. Kama ni fedha zimeshakwenda hivyo nakubaliana na wewe kuwa viongozi waishi na uamuzi wao.
 
Watakwambia wapo kwenye safari za kikazi Dar, kwa nini tusiwaone na mikoa mingine.......jambo la muhimu kama hao maafisa wana mishe zao binafsi Dar watumie magari yao binafsi siyo ya umma......
 
Kwahiyo unataka tuondoe kwanza viongozi waliopo tulete wapya watakaoiheshimu katiba ?
 
Trump aliwatingisha wamarekani au alijitingisha mwenyewe na kudondoka ??
 
Hapana brother,hiyo katiba tunayoiongelea hapa sio hii,raisi akiikanyaga anajua kabisa atafunguliwa mashtaka so watawala hawa wame-relax kwa sababu wanajua katiba hii haina meno na mihimili mingine wameitia mfukoni.tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa utawala wa bwana yule,na mtu yeyote mwenye akili timamu hatopenda mtawala kama yule atokee tena kwenye nchi yetu.
 
Ni wazi walikuwa wanamheshimu mwenda zake kinafiki,hawakupenda kuhamia Dodoma,hii sasa ni sawa na kumpeleka punda mtoni kunywa maji wakati hana kiu hatokunywa,na sidhani kama Bi mkubwa anaweza kuwadhibiti.
 
Hivi hata PM naye hayaoni haya. Yeye ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za serikali kule bungeni na kiranja wa hao mawaziri.

Kwa nini hamsaidii mama?

Mpango naye naona sasa ameelewa nafasi yake ya umakamu,maana mwanzoni alijiona kama rais wa nchi.

Tuwahimize wajue ofisi ni dodoma, sijui zile taasisi zilizokuwa na mipango ya Dom kama bado wanamawazo hayo pia.

Mwendazake ameenda na mengi sana.
 
Yote kwa yote katiba mpya iwepo kwanza wasiotaka kuishemu katiba wembe ni ule ule uliotumika kumnyolea Jacob Zuma ndio huohuo utakaotumika kuwanyolea wasiotaka kuiheshimu katiba
 
Hayo ni matunda ya utawala wa kiimla ya dikteta Magufuli. Watendaji walijaa unafiki mtupu. Watu waliacha kufanya kazi kufuata miongozo na wakawa busy kumridhisha Magufuli huku wakitesa watanzania.
Si mlikuwa mnamtukana Magufuli?

Si mlisema mama anaupiga mwingi na sasa ufipa mnapumua?

Season ya nyumbu migration imeanza rasmi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…