Kwa sasa ni nadra sana kuwakuta hawa viongozi wapo Dodoma Makao Makuu, wote imekuwa ni njia moja Dar

Hao watu watakaoiheshimu watazaliwa lini?.au utaenda kuwaazima nchi gani?.Watu tayari wako kinachokosekana ni muongozo thabiti ndo maana mambo yanaenda ovyo ovyo.mambo mengine hayahitaji elimu kubwa kuyaelewa
 
Sahihi kabisa
 
Kwahiyo nchi iache kua na viongozi waadilifu tusubir mtu mwenywe abadilike mindset.hakuna kitu cha hivyo duniani ndo maana kuna sheria na vyombo vya dola.mradi umeamua kutumikia wananchi lazima uishi na kutenda kulingana na sheria zilizopo ata kama una tabia zako binafsi.Mambo ya utashi yabaki kwenye mambo binafsi sio shughuli za nchi.
 
Mkuu kwa mtazamo wangu mm huyu mama hawezi kua rais bora kabisa kwa kifupi mm smukubali hata kidogo nimejipa mda ili nijirizishe kwanza na utendaji wake.
 
Hawa watu wanaodai katiba mpya wanataka tume itakayoweza kuwapa ushindi watwae madaraka hakuna kingine cha msingi wanachopigania
 
Bwana yule alikua anaenda Sana chato mbona mawaziri wake hawakuiga kwenda huko kitovuni?
 
Kama umejenga Banda kule imekula kwako,
 
Inakuuma nini labda. Ulitaka wawe Chato mwezi mzima?
 
Hayo yote yanaonyesha nj namna gani viongozi walivyo wanafki
Kipindi cha mwendazake wasingeunga mkono suala la kuhamia Dodoma kama hawakuridhia
Na bado tutajionea mengi na ufujaji wa kodi zetu utakuwa wa hali ya juu mno
 
Hayo yote yanaonyesha nj namna gani viongozi walivyo wanafki
Kipindi cha mwendazake wasingeunga mkono suala la kuhamia Dodoma kama hawakuridhia
Na bado tutajionea mengi na ufujaji wa kodi zetu utakuwa wa hali ya juu mno
Dalili zinaonesha wazi kabisa!
 
Tuliwaambia, maamuzi ya kukurupuka na kutafuta kiki anayoyafanya Mwendazake, yataligharamu Taifa in future, ona Sasa.
Kweli kabisa,Magufuli hakufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuhamisha makao ya serikali.
Yawezekana pia hakuhusisha baraza la mawaziri .Lakini kibaya zaidi kujenga Makao makuu haikuwa kipaumbele cha taifa ni uvujaji wa pesa ya umma.
 
Hivi Dodoma kuna KFC?

Au ShiShi Food tu inatosha![emoji276]
 
Tatizo liko kwa msimamizi
Tatizo liko kwa aliyefikiria kuwa Dodoma kuwa Makao makuu.Tangu mwanzo yeye mwenyewe kamalizia miaka yake zaidi ya 20 akiwa Bongo Daslam sasa anakuja jamaa kurupu twendeni Dom.Thubutu.Kukaa Dodom inahitaji Moyo.Hao wabunge wa Dodoma akina Ndugai wikiend wako Dar. Hata Mwendazake siku alizokaa Dodoma ni chache kuliko alizokaa Dar.Kwa ufupi hakuna Mtazania asiyependa kukaa Dar.
 
Hii ndio Tanzania,my country [emoji17][emoji17][emoji17]
 
Katiba nzuri inajilinda na huwapa wananchi na wasimamizi uwezo wa kuisimamia isivunjwe ovyo ovyo. Ni katiba isiyompa mtu mmoja mamlaka makubwa, hata ya kumwezesha kuivunja katiba yenyewe bila kuhojiwa kwa mamlaka makubwa anayopewa na katiba mbovu.
Nadhani una false expectation kuhusu Katiba; siyo kweli kuwa katiba inajilinda, bali katiba hulindwa na walioapa kuilinda na kuitetea- yaani viongozi. Kila kiongozi huapa kulinda na kuitetea katiba; wananchi hawana kiapo cha kuilinda na kuitetea katiba. False exepectation ni kudhani kuwa katiba ndiyo mwarobaini (lugha ya prof Shivji) wa kila tatizo letu na kusahau nafasi ya wanaopewa dhyamana ya kuilinda na kuitetea katiba hiyo. Angalia kuwa Uingereza hawana katiba kabisa ila wanaishi kwa sheria za bunge tu, na serikali inajiendesha vizuri kwa kufuata hizo sheria za bunge tu (Magna Carta siyo katiba ya uingereza). Halafu Marekani wana katiba na wanaitanguliza sana lakini wakati wa utawala wa Trump imevunjwa sana.
 
Kwa nini viongozi wasifungiwe GPRS tracers kwenye makalio yao
 
Dar imeshakuwa na watu wengi sana kiasi kuwa shughuli za serikali zinakuwa ni kero kwa raia. fikiria unatoka nyumbani kwenda mishe mishe zako, unakuta traffic wamefunga barabara kwa sababu kuna msafara wa rais. Halafu hujafikia mtaa wa pili unakuta barabara zimefungwa kuwa kuna msafara wa makamu wa rais: ni kero sana. Ndiyo maana nchi nyingi sana zilizojengwa miaka ya karibuni hutenga eneo la makao makuu liwe ni tofauati na vitovu vya biashara. Ni nchi za zamani sana ambazo makao makuu ya mfale yalegeuka kuwa vitovu vya biashara na ikabaki hivyo, kwa mfano, Tokyo, London, na nchi kadhaa za ulaya. Na hata hivyo katika miji hiyo bado sehemu za serikali zimetengwa sana na sehemu za biashara.
 
Wananchi ndio wenye madaraka yote, ndio wanaowaweka hao viongozi wanaoapa kuisigina katiba, na kwa hiyo wananchi wanao uwezo wa kuwawajibisha.

Hili nalo ni gumu kwako kulielewa?

Kama uingereza hawana Katiba kabisa, lakini wana sheria zinazotungwa na bunge; hizo sheria zinakiukwa na hao viongozi wanaowekwa na wananchi?
Kwani Katiba ni nini, siyo sheria?

Kama "Trump alivunja katiba" jambo ambalo siyo kweli, eleza sasa yupo wapi?

Unatafuta tu njia za ku'justify' uvunjaji wa sheria wa hao unaosema wanaapa kuilinda katiba, halafu wasiwajibishwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…