Kwa sasa sipo tayari kuolewa, nahitaji kufanya mambo yangu

Kwa sasa sipo tayari kuolewa, nahitaji kufanya mambo yangu

Shida unahisi au kudhania kuwa hapa tunashindana hoja jambo ambalo si kweli. Kimsingi hapa unabishana na ukweli ambao muda huuleta katika maisha ya kila mtu kulingana na sababu zake.

Mwanamke ndie anayehitaji ndoa kwasababu ya benefits zake na sio kwasababu ya ndoa jina. Wewe kama unabisha bisha kwa sababu umeamua kuleta ligi ila huo ndio ukweli ambao utakuja kuprove hata ubishe vipi.

Ndoa si jambo wala haja ya mwanaume na ndio sababu ambaye huwa anajutia mara nyingi ni mwanaume siku za baadae.

Wanawake huanza kuona sababu au umuhimu wa ndoa age ikienda sababu hawana sababu za kuwavutia wanaume.

Unavyosema kila mtu ana muda wake wa kuingia Ndoani una maanishaje ati?

Unaongelea ndoa jina au ndoa taasisi?

Mwanamke wa miaka 30+ unaolewa na nani katika umri huo ambae atakuwa alikuwa amekaa tu akikungojea uje aishi na wewe?

Na tutakupeleka hospitali kweli kwa utakachoshuhudia. Kwanza hautakuwa hapa kubishana maana utakuwa tayari umeshajionea ukweli na upo huko uraiani unaishi life lako.

Kuna watu tulikuwaga nao hapa JF tukibishana hizi hizi mada miaka ya 2012 na 2013 hapo. Leo wapo kimya huwaoni tena sababu umri umeshakwenda wamejionea sasa uhalisia na wanajua sasa Maisha sio maigizo ya bongo movie.
Hivi kwanini mkishashindwa hoja huwa mnakimbila kusema kwamba tunashindana nani atafute ushindi humu mkuu humu huwa tunajadiliana tu kama ninyi mnatafuta ushindi basi ni ninyi ila mimi najadili uhalisia tu, sasa kama ndoa ni muhimu kwa mwanamke tu na siyo kwa mwanaume kwanini wanaume mnaendelea kuoa pamoja na maovu yote haya ya wanawake ilihali mna uwezo wa kuacha kuwaoa na msipungukiwe na chochote, hayo ya kusema kwamba eti mwanamke akifika umri fulani anapata shida kuolewa je ni nature au ni mitazamo ya kipumbavu ya jamii za kiafrika, na kama ni nature mbona kwenye jamii nyingine mfano za wazungu wapo wanawake wengi tu wanaoolewa katika umri wowote haijalishi wana watoto au la na ndoa zao zinadumu vizuri tu, na hata huku afrika tu wanawake pamoja na maovu yao yote ila bado wanaolewa kila siku
Wewe bila wanaume kupambana na majambazi utakuwa salama wewe?

Nyoka akiingia ndani utamuua wewe?

Gari kuimaintain utaweza hiyo kazi , yule fundi mudi pale gereji ni mama yako mdogo yule au ni mwanaume?

Shida unaleta ligi na ubishi jambo ambalo halina msaada katika mjadala ili tuweze kuelewana.

Ukisema majukumu hayo ni mambo ya ndoa kitu ambacho ninyi wanawake ndio mnakihitaji kwa nguvu na kwa damu na jasho. Ingekuwa hamuhitaji Ndoa then usingesema kuna kuhudumiwa sasa mtu unakiri ndoa haina faida kwa mwanamke ina faida zaidi kwa mwanaume the how the hell mwanaume analipia 290% ya bills za mke, familia na ukoo wako?

You have to be serious.
Yani unavyoongelea hayo majukumu ya kupambana na majambazi ni kama vile ni majukumu ya kila siku na ni kama vile wanaume wote ni lazima wapitie hayo wakati kuna wanaume wengi tu toka wanazaliwa hadi wanakufa uzeeni hawajawahi kukumbana na madhila hayo, hebu acheni kujificha kwenye majukumu ambayo yako based on uncertainties na they are not likely to happen in daily life msiyafananishe na majukumu ya kila siku ambayo yanaconsume time na energy ya mhusika na kumfanya achoke kila siku, hayo majukumu ambayo mnatimiza wanaume si kwamba mnayafurahia ila ni kwa sababu tu kuna vitu mnategemea kuvipata in return toka kwa hao wanawake mnaowahudumia mfano kufanyiwa kazi za ndani, kulelewa watoto, kupewa heshima na utii pamoja na kuliwazwa hakuna mwanaume mwenye moyo wa kuhudumia mwanamke ambaye hatimizi hayo majukumu
Unafanya swala la Ndoa lionekane personal au la mtu binafsi wakati ni swala la ustawi wa kijamii na swala la kitaifa.

Usidhani wanaume tunawabembeleza kwamba nje ya ndoa hatupati tunachotaka. Ni kazi ya wanaume kulinda ustawi wa jamii.

Wewe unaongea hapa ila unaishi chini ya mbawa za baba yako anakulinda na unafaidika na benefits za taasisi ndoa,mama yako angekuwa analeta habari kama zako sidhani kama ungekuwa hapo kuongea haya unayosema hapa. Unaponda kitu ambacho benefits zake kinakufaidisha wewe tena ukiwa mtoto au uzao wa taasisi ndoa.
Unaona sasa jinsi mlivyo wanafiki yani mnadai kwamba ni kazi yenu kulinda ustawi wa jamii wakati huo huo mkiambiwa muache kuchezea wanawake ili wajitunze mnaleta visingizio vya kipumbavu eti oo ni wao wanaoumia zaidi hivyo wao ndio wanatakiwa wajitunze, haya sasa kwa kuangalia uhalisia uliopo kwenye jamii ni jinsia gani inayoumia zaidi kwa kukosa wenza wenye maadili mema kama siyo ninyi wenyewe hadi mnafikia hatua ya kujifanya mnakataa ndoa kumbe ni sizitaki mbichi hizi tu, kama kweli mmeamua kulinda the so called ustawi wa jamii basi anzeni ninyi kubadilika acheni kuwachezea na kuwaharibu mabinti hovyo kwa kisingizio kwamba ni nature yenu, then wanawake wakishaona mko serious kwenye hilo nao wataanza kutambaa na beat taratibu na hatimaye mambo yatakaa sawa na kuenda vile mnavyotaka, ninyi si ndio viongozi bana sasa mbona kwenye hili suala la ustawi wa jamii hamtaki kuongoza njia mnabaki kuwatukana na kuwadhalilisha wanawake kwa upumbavu wenu
 
Niwe na Tsh ngapi nisiambiwe haya maneno ? (Kiasi gani cha pesa).

Huyo anaeiniambia hivyo anakuwa katika hali gani ya kiuchumi ?.


Ninashauku ya kuambiwa hivyo, ila nikuhakikishie tu huku uswahilini kwetu hio kauli hutamkwa na binti asiejitambua tu.

Tumezoea vizinga vyetu elfu mbili mbili mwisho elfu tano. Labda huko kwenu ulipo UKWASI.
Uwe na fixed assets, nyumba za biashara, mashamba na nyumba yako ya kuishi, uwe na gari na uwezo wa kumfadhili mwanamke kwa mahitaji yake yote, jumlisha outings na vacations za ndani na nje ya nchi
 
Uwe na fixed assets, nyumba za biashara, mashamba na nyumba yako ya kuishi, uwe na gari na uwezo wa kumfadhili mwanamke kwa mahitaji yake yote, jumlisha outings na vacations za ndani na nje ya nchi
Wakati huo uyo mwanamke anamiliki nini na anaongeza thamani gani kwenye mahusiano?
 
Back
Top Bottom