Nimeshakujibu kwa maelezo na mifano kuhusiana na swali lako sasa sijui katika maelezo yangu hujapata la kukusaidia, ama umekaza kichwa hutaki kufungua kichwa na kukubali ukweli mchungu, kama umekaza kichwa hapa hatuwezi kuelewana hata nielezee vipi hauwezi kunielewa.
Mwanaume ana uwezo mkubwa kufanya majukumu ya mwanamke kuliko ambavyo mwanamke angefanya majukumu ya mwanaume hata wakibadilishana, hili halina ubishi hata wanawake wenzako watakiri juu ya hili, ndio maana nimetoa mifano mingi tu ya kueleweka.
Kama unataka kuelewa utaelewa kama upo hapa kwa ajili ya kubisha basi nitakua natwanga maji kwenye kinu, hata niandike kitabu hutonielewa na hauna huo utayari.
Kingine tunatokea background tofauti katika malezi, utofauti katika jamii n.k.
Inawezekana unapotoka hujashuhudia mwanaume akipika, kuosha vyombo, kufua na kazi nyingi za nyumbani.
Familia ninayotokea mzee wangu alikuwa anafanya kazi zote nyumbani kipindi nipo mdogo, kuanzia kupika hadi kufua, usafi nyumbani na kila kitu kwa miaka hadi naanza kujitambua.
Mimi hakuna kazi ya nyumbani itanishinda, hata kupika biryani napika na sioni huo ugumu wowote ambao unasemwa kufanya kazi za nyumbani.
Wanaume wengi hizo kazi za nyumbani wanafanya sana tu, kuna zile familia unakuta kuna watoto wa kiume tupu utakuta wanafanya kazi zote za nyumbani.