Sasa mwanaume kutelekeza mtoto huo ni ujinga, na ujinga huu upo hata kwa wanawake tena wao wanaua kabisa watoto, mfano kutoa mimba, hamuelewi uhai wa mtoto unaanzia tumboni, kutoa mimba ni ukatili, au mtu anajifungua ananyonga mtoto, au anamtupa jalalani, haya matukio ni mengi, mnanyofoa mimba kama hamna akili vizuri, ujinga mwingine kubambika mwanaume mtoto si wake, unajua kabisa hio mimba ni fulani unambambika mwingine, mna roho ngumu sana.
Ndio maana wanaume wengine wanakataa mnasema mmetelekezwa.
Kuhusu single mother kulea watoto.
Kwani ni wanaume wangapi wanalea watoto si wao, unakuta mwanaume hana mtoto anaoa mwanamke ana watoto wawili, mwanaume anawatunza watoto kama wake na kuwahudumia bila neno, shida ni mwanamke amkute mwanaume ana watoto na mwanamke aliyeachana nae, au mkewe alifariki, aisee kwa asilimia kubwa mwanamke atalea watoto kwa ubaguzi mara nyingine kuwatesa, tumeshasikia sana kuhusu mama wa kambo. Sijui aina hii ya wanawake wanakuwaga na roho ya aina gani, watoto wanaanza kumchukia mama wa kambo, familia nyingi ipo hivyo.
Unakuta mwanaume anasomesha ndugu wa mwanamke, anahudumia familia ya mwanamke kama yake kuanzia mama hadi mzee, nyumbani anakaa anakaa na ndugu wa mwanamke vizuri.
Hio nyie mnaweza? Hata kama una pesa unaweza kusomesha ndugu wa mwanaume na nikisema kusomesha unaelewa mziki wake, mnaweza kukaa kistaarabu na mama mkwe nyumbani kwa amani na heshima?
Hilo kwa asilimia kubwa hamuwezi, lazima chokochoko zianze. Fanya research hata nyuzi za hapa jf utathibitisha hili. Fanya research uangalie kuna vijana wangapi wamesomeshwa na shemeji zao wa kiume.
Kuna rafiki yangu kasomeshwa na shemeji yake toka utoto, akampeleka China akarudi, akampeleaka kwenye kampuni yake hivi sasa anafanya kazi hapo, jamaa kaachana na dada yake lakini bado msela anafanya kazi kwake, jamaa(huyo mwanangu) hadi kanunua gari na ghorofa Dodoma kwa kazi hio shemeji yake kampa, wanawake mnaweza? Acheni nyie, wanaume wangapi wamejenga kwa mwanamke, kuuguza wazazi wa mwanamke, nyie mnaweza?
Wanaume wanaojielewa wana roho za kizungu sana, wanaume mnawahitaji tena sana tu.