Kwa sasa sipo tayari kuolewa, nahitaji kufanya mambo yangu

Hivi kwanini mkishashindwa hoja huwa mnakimbila kusema kwamba tunashindana nani atafute ushindi humu mkuu humu huwa tunajadiliana tu kama ninyi mnatafuta ushindi basi ni ninyi ila mimi najadili uhalisia tu, sasa kama ndoa ni muhimu kwa mwanamke tu na siyo kwa mwanaume kwanini wanaume mnaendelea kuoa pamoja na maovu yote haya ya wanawake ilihali mna uwezo wa kuacha kuwaoa na msipungukiwe na chochote, hayo ya kusema kwamba eti mwanamke akifika umri fulani anapata shida kuolewa je ni nature au ni mitazamo ya kipumbavu ya jamii za kiafrika, na kama ni nature mbona kwenye jamii nyingine mfano za wazungu wapo wanawake wengi tu wanaoolewa katika umri wowote haijalishi wana watoto au la na ndoa zao zinadumu vizuri tu, na hata huku afrika tu wanawake pamoja na maovu yao yote ila bado wanaolewa kila siku
Yani unavyoongelea hayo majukumu ya kupambana na majambazi ni kama vile ni majukumu ya kila siku na ni kama vile wanaume wote ni lazima wapitie hayo wakati kuna wanaume wengi tu toka wanazaliwa hadi wanakufa uzeeni hawajawahi kukumbana na madhila hayo, hebu acheni kujificha kwenye majukumu ambayo yako based on uncertainties na they are not likely to happen in daily life msiyafananishe na majukumu ya kila siku ambayo yanaconsume time na energy ya mhusika na kumfanya achoke kila siku, hayo majukumu ambayo mnatimiza wanaume si kwamba mnayafurahia ila ni kwa sababu tu kuna vitu mnategemea kuvipata in return toka kwa hao wanawake mnaowahudumia mfano kufanyiwa kazi za ndani, kulelewa watoto, kupewa heshima na utii pamoja na kuliwazwa hakuna mwanaume mwenye moyo wa kuhudumia mwanamke ambaye hatimizi hayo majukumu
Unaona sasa jinsi mlivyo wanafiki yani mnadai kwamba ni kazi yenu kulinda ustawi wa jamii wakati huo huo mkiambiwa muache kuchezea wanawake ili wajitunze mnaleta visingizio vya kipumbavu eti oo ni wao wanaoumia zaidi hivyo wao ndio wanatakiwa wajitunze, haya sasa kwa kuangalia uhalisia uliopo kwenye jamii ni jinsia gani inayoumia zaidi kwa kukosa wenza wenye maadili mema kama siyo ninyi wenyewe hadi mnafikia hatua ya kujifanya mnakataa ndoa kumbe ni sizitaki mbichi hizi tu, kama kweli mmeamua kulinda the so called ustawi wa jamii basi anzeni ninyi kubadilika acheni kuwachezea na kuwaharibu mabinti hovyo kwa kisingizio kwamba ni nature yenu, then wanawake wakishaona mko serious kwenye hilo nao wataanza kutambaa na beat taratibu na hatimaye mambo yatakaa sawa na kuenda vile mnavyotaka, ninyi si ndio viongozi bana sasa mbona kwenye hili suala la ustawi wa jamii hamtaki kuongoza njia mnabaki kuwatukana na kuwadhalilisha wanawake kwa upumbavu wenu
 
Uwe na fixed assets, nyumba za biashara, mashamba na nyumba yako ya kuishi, uwe na gari na uwezo wa kumfadhili mwanamke kwa mahitaji yake yote, jumlisha outings na vacations za ndani na nje ya nchi
 
Uwe na fixed assets, nyumba za biashara, mashamba na nyumba yako ya kuishi, uwe na gari na uwezo wa kumfadhili mwanamke kwa mahitaji yake yote, jumlisha outings na vacations za ndani na nje ya nchi
Wakati huo uyo mwanamke anamiliki nini na anaongeza thamani gani kwenye mahusiano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…