Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 9,016
- 24,650
Kwenye suala la kumiliki mpira na kucheza kandanda safi kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, sioni timu ya kuwashinda wananchiwananchi. Tumaini pekee la wapinzani wanaokutana na Yanga ni kupaki basi na kucheza kaunta attack.
Mtihani wa benchi la ufundi kwa sasa ni kuja na mbinu za kuwafunua wapinzani, maana mara zote wanapaki, basi hii inapelekea kutengeneza nafasi chache sana za kufunga.
Watu wanawasema Al Hilal kwa mpira waliocheza, lakini siyo kwamba ule ndiyo mpira wao wa kila siku. Pale wanapokutana na timu wanazozimudu huwa wanamiliki mpira. Mfano mechi ya kirafiki dhidi ya Makolo na michezo yote miwili dhidi ya St. George, ila dhidi ya wananchi Ibenge hakuwa mjinga kupaki basi dakika zote 180, ni wazi alijua akiweka mpira chini hatoweza kushindana na Yanga.
Kitu pekee ambacho Pogba amemzidi Fei Toto ni uchawi tu. Kuna muda Dunia haina usawa, inasikitisha sana kuona Fred anakipiga Man UTD wakati aucho yupo Yanga. Mwangalie Aziz Ki anavyotembeza mpira, mtu unapata ile radha halisi ya soka. Nipe tofauti moja tu ya Sure Boy na Iniesta, nami nitakuonesha bucha la kitimoto kwenye kambi ya Al Qaeda!
Kuliko kupotezeana muda na nguvu hili kombe la CAF Confederation, ni bora wapewe tu wananchi.